Karibuni kwenye Kazi ya ualimu, lakini usiwe na matarajio makubwa

Karibuni kwenye Kazi ya ualimu, lakini usiwe na matarajio makubwa

Huko Sumbawanga unakosemea nimekutana na waalimu wana maendeleo ya juu sana kuliko watu walioko TRA na hawa niliowaona ni walimu wa shule za Msingi na wengi ni vijana hata miaka 10 kazini bado.

Kama watu wakiwa na utashi wa kufanya maendeleo na wakapambana na kuhakikishia wanaitumia hii ni njia kutoka kimaisha basi kwa muda mfupi haswa watafanikiwa endapo wakipelekwa Mazingira yenye fursa za Kilimo na ufugaji.

Kwa Mazingira ya Dar kiukweli ni changamoto sana mana wengi hawana option. pesa inatumika kwenye matumizi zaidi.
 
Sisi kamati ya roho mbaya tupo nje ya uwanja tunawaombea kiwakute kama kilichowakuta wale wa USAID kuna jamaa ameitwa hapa mtaani sasa hivi anajifanya hataki tena kukaa na sisi kijiweni anasema eti utumishi wa umma kuna "standards" inabidi azifuate🐼
 
Sure, lakini Mungu akutuweka duniani kufanya vitu vidogo vidogo, Bora kupambana Mimi nipo humu ndani naowaona hawana matumani kabisa.
Nilipofika sometimes naona kheri uishi tu maisha ya kawaida. Dreaming big ni mzigo, na kheri waalimu ambao hawatarajii mengi kuliko wengine ambao wasipopata walivyotaraji wanaweza hata kujiua.

Hata mimi ndoto yangu nikifika pahala flani, niishi maisha tu ya utulivu mikoani huko. Fresh food, fresh air na hakuna mahangaiko
 
Umeongea kweli, kila mtu duniani yupo na malengo yake kwa mfano Mimi sipendi kua chini ya mtu, na hii kazi lazima uwe chini ya watu, madharau n.k mpaka diwani, au mwenyekiti wa mtaa anaweza kukutukana na kukupelekesha.
 
Sisi kamati ya roho mbaya tupo nje ya uwanja tunawaombea kiwakute kama kilichowakuta wale USAID kuna jamaa ameitwa hapa mtaani sasa hivi anajifanya hataki tena kukaa na sisi kijiweni anasema eti utumishi wa umma kuna "standards" inabidi azifuate🐼

Ndio shida za vijiweni mkuu, hakuna urafiki zaidi ya mob psychology.. Binafsi yangu rafiki akinizidi level na akaonesha kuwa hawezi kaa na mimi meza moja nitabalance shobo ila siwezi kumuombea ubaya kwa sababu si ubinadamu na pengine alichokifanya ni kufungua akili kuwa natakiwa kuwa zaidi ya nilipo..
 
Umeongea kweli, kila mtu duniani yupo na malengo yake kwa mfano Mimi sipendi kua chini ya mtu, na hii kazi lazima uwe chini ya watu, madharau n.k mpaka diwani, au mwenyekiti wa mtaa anaweza kukutukana na kukupelekesha.
Hujaingia private sector ukutane na boss anaejua kupelekesha watu. Kiufupi hakuna hiyo freedom na kama umekaa miaka miwili kazini bhasi inabidi jangalee options zako.

Aidha uswitch kwenye NGO's za masuala ya elimu au ujiandae kufungua shule yako mwenyewe ama utoke kabisa katika hiyo kada yako. Lakini katika yote usisahau kila kitu ni mchakato na pengine hata hapo ulipo panaweza kukufikisha sehemu

Achana na kuangalia issue yako collectively kama "waalimu".. Angalia wewe kama wewe utafanya nini
 
Asante mkuu, kwa upande wangu ni kutoka hapa na kusoma kada nyingine, au kujiajiri tu, nimeshaanza upande wa kujiajiri ninamiliki ekari nyingi , na kati ya hizo chache nimeanza kupanda zao la kudumu, mawazo ya kufanya yoote hayo nimeyapata baada ya kuona hali halisi kwenye kada hii,.
 
Back
Top Bottom