Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

Bibilia inasisitiza watu wasome, ila ikitokea taasisi inataka wasomewe na viongozi ni kinyume na bibilia ndio maana napongeza juhudi hizi za Sala na Kazi za kuwataka msome bibilia kikatoliki angalau.
mpendwa katika kristo ni nani au ni taasisi gani iliokataza waumini wake wasisome biblia ila wasomewe ?? iliokataza waumini wake wasijifunze biblia ila wasubiri kufundishwa ? ni nani ni tasisi ipi iyo ?

kwa upande wako kipi ni kibaya au ni makosa

je, ni kuanzishwa kwa kituo cha kutoa elimu ya biblia kwa marefu na mapana (usichanganye na kujifunza mapenzi ya Mungu kwa ajilivya utakatifu wa maisha) ?

je, ni kwa sababu kituo kinafundisha biblia KIKATOLIKI ?

je, ukiacha elimu ya biblia, vipi kuhusu elimu zingine zihusuzo taaluma zetu za kawaida hizo zinaongozwa na roho yupi ? na kama ni kwa roho mtakatifu ni kwa nini tutumie zaidi ya miaka 15 shuleni ? na sio roho pekee ??
 

Tunasoma kutoka Injili ya Luka 2:52 hivi:
" Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu."

Hekima inafunua wazo la maarifa. Je,maarifa hayo aliyapata wapi Yesu? Kuna namna mbili Yesu alifundishwa:

1. Na wazazi wake kama ilivyokuwa desturi ya watoto Wa kiume Wa Kiyahudi kufundishwa Maandiko Matakatifu,Agano la Kale

2. Watoto Wa Kiyahudi katika Karne ya Kwanza AD walikuwa wanasomeshwa bure.

Ukiachana na suala la Yesu kufundishwa nyumbani na wazazi wake, vile vile Yesu kama mtoto Wa kiume Wa Jamii ya Kiyahudi alipata fursa ya kusoma bure. Watoto wote Wa Kiume Wa jamii ya Kiyahudi katika Karne ya kwanza walikuwa wanasoma bure. Walisomeshwa Scripture na law. Walifundishwa pia kusoma, kuandika, historia, elementary sciences and mathematics. Na Fursa hii ilitolewa kwa kila mtoto wa kiume wa Kiyahudi bila kujali hadhi ya familia anayotokea au social standing.

Kwa hiyo,ile pointi kwamba wazazi wake YESU walikuwa maskini na hivi wasingaliweza kumudu gharama za masomo sio kweli. Na kupitia fursa hii Paulo na Timetheo nao walisoma.

Ushahidi kwamba Yesu alisoma.

"16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa," (Luke 4:16-17)


"7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi." (Yohana 8: 7-8).

Kwa hiyo, haya yote yanathibitisha kwamba Yesu aliingia darasani na ndio kisa alijua kusoma na kuandika na hata kutafsiri maandiko mbalimbali Matakatifu.
 
Umeshaambiwa utafundishwa kigiriki na kiebrania ili ukasome biblia halisi... Unataka nini tena?
Nenda wewe mkuu; mimi siwezi kufungamana na watu hao hata siku moja; najua ni kwa nini nasema hivyo! ogopa sana mtu mnafiki; bora adui.
 
34Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo,

ninachokataa ni kisema hakuna farisayo aliyekuwa mjuzi wa maandiko. Gamalieli alikuwa ni farisayo. Paulo anasisitiza Alikuwa farisayo, Pia kwa yeye kuwa mwalimu wa Sheria ni uthibitisho kuwa mafarisayo walijua neno. au unaweza kuwa farisayo na hapohapo ukawa mwalimu.

Uthibitisho mwingine.


Wafilipi 3:5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

Matendo 23:6
Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.

Kauli hii iliibua mgogoro wa kitheolojia kati ya mafarisayo na masadukayo. Sio waandishi. hivyo ujue kuwa hawakuwa vilaza wa maandiko. Hii inaonyesha wahusika walikuwa na uelewa wa maandiko.

Usipinge vitu vilivyowazi otherwise uonyeshe mstari kuwa walikuwa hawajui chochote sio story mkuu.
Kuhusu waandishi na waalimu nakubaliana na wewe.
 
Nenda wewe mkuu; mimi siwezi kufungamana na watu hao hata siku moja; najua ni kwa nini nasema hivyo! ogopa sana mtu mnafiki; bora adui.

Ndio maana tunawaambia ukristo wenu ni mpya kabisa tofauti na ule alioufundisha Yesu Kristu. Kristu aliwatafuta wadhambi kokote walikokuwa na alijichanganya nao. Je,ninyi mbona mnawakimbia "waabudu sanamu" na "wapagani" (wakatoliki)? Mbinguni mnataka muingie Wasabato pekee tu ili muendeleze maadhimisho ya sabato na Mungu peke yenu?
 
Watu waandike maandiko kwa Bidii kwa Uongozi wa Roho mtakatifu miaka zaidi 1500 kabla na baada ya Yesu, kiibuke kikundi cha dini kijimilikishe hii ni KUFURU kwa MWENYEZI MUNGU.
Kituo hiko ndio kitatoa majibu nani ali-compile biblia...

Ukitaka kufahamu nani ni nani katika kukusanya biblia pitia mitaguso hii

Mtaguso wa Rome (Council of Rome)
Mtaguso wa Cathage

Halafu msome St Athanasius....halfu uje umsome St. Jerome

Sasa kama hiyo mitsguso ilikuwa ya Kisabato au kina Atanasi walikuwa ni wasabato tutaelewa
 
Kulikuwa hakuna shule eti unaweza mpeleka mtoto huko...


Kifupi Rabi alikuwa anachagua wanafunzi wake kisha anawafundisha kwa kipindi kirefu...


Hujui Historia wewe...kaaa kimya

Nimeshampatia verses za Biblia kuthibitisha kwamba Yesu alipiga shule na sababu za kihistoria kuthibitisha kwamba umaskini Wa wazazi Wa Yesu hakikuwa kikwazo cha kumfanya Yesu asihudhurie shule nimeshampatia
 
#
Kwa wayahudi Jukumu la kwanza kwa Elimunya Dini sio shuleni bali Nyumbani tangu akiwa mdogo.
Na Kusoma na Kuandika walijifunza Nyumbani, maana Agizo linasema wazazi wawafundishe watoto.
Utamfundishaje mtoto kama hujaanza kumfundisha kusoma na Kuandika. Tusifikiri kitanzania tufikiri Oriental mkuu.

Mstari. kumbukumbu la torati 6:6-9
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Ndio maana nikakupa mfano wa stephano ambaye Paulo anamshuhudia amejifunza kwa Mama na Bibi yake. Maana hata hivyo huko Listra walikukwa wanaishi hakukuwa na sinagohi walamhao wakufunzi, na ulikuwa ni mjimwa kipagani hadimwaliwaita paulo na barnaba kwa majina ya miungu yao.

##
Pia elimu nyingine ya dini kwa watoto ilitolewa kwa maswali na majibu siku ya sikukuu za dini, ni mkakati maalum.
Kutoka 12:26 Kisha itakuwa, hapo watoto wenu watakapowauliza, N'nini maana yake utumishi huu kwenu?

###
Kwa masimulizi nje ya BIBIBLIA maana mistari uliyotoa haionyeshi kama alipita katika rabbinical schools.
kulikuwa na mafunzo ya kawaida tu, kwenye masinagogi hasa kwa watoto wa miaka sita/saba .
Ila hapa nazungumzia zile Rabinical schools mfano enzi za Paulo kulikuwa na shule mbili maarufu na pinzani Shule ya Hillel na Shule ya Shammai (schools of theology) ambazo walihudhuria vijana miaka 13+ sio watoto na moja wapo alihudhulia Paulo.

Ila Uthibitisho wa Maandiko kuwa Yesu Hakupitia kwenye hayo mashule ya mascholers wa kiyahudi kama Paulo anavyosema.

Matendo ya Mitume 22:3
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Yesu alikuwa anapinga Sheria za mababa na mdesturi zote ambazo ndizo zilikuwa Core courses za shule hizo za mayahudi.

mfano
Mathayo 15:3,6
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.

Wanafunzi waliopitia Mfumo wa shule ya dini kama aliyowaachia wanafunzi wake, ni wale watoto wa wa vuvi vilaza ila waliposimama kutamka mambo ya Mungu walionekana Bora kuliko waalimu wa sheria na scholars wote wa wakati huo.

Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
Matendo 4:13
 
Nimeshampatia verses za Biblia kuthibitisha kwamba Yesu alipiga shule na sababu za kihistoria kuthibitisha kwamba umaskini Wa wazazi Wa Yesu hakikuwa kikwazo cha kumfanya Yesu asihudhurie shule.
Yesu kama myahudi mwingine yeyote alifuata na kuheshimu taratibu, mila na desturi za kiyahudi. hakupeleka mambo kibabe, kimiujiza na kibishi eti kwa sababu yeye ni Mungu

pamoja na kwamba yeye alikuwa Mungu na kufahamu kila kitu bado alheshimu taratibu zote alizozikuta katika jamii yake sasa hawa ndugu zetu wanaoltupia kila kitu kwenye ulimwengu wa roho na kumsukumia kila mzigo roho mtakatifu ni watu wa kuwahurumia na kuwaombea pua.

na matokeo yake ndio kuishi kwa maono, ndoto na unabii
 
uwe unaquote maelezo yote, kunyofoa kipengele ambacho kilipewa nguvu na maelezo ambayo umeyaacha ni dhambi inayoitwa " SIN OF OMISSION''.

wasabato hata kama wangeanza juzi.
wanasisitiza na kufundisha yale yaliyopo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu mkuu.
Wanasisitiza kweli za bibilia zenye umri mkubwa kuliko hata Dunia.

Bibilia inasisitiza watu wasome, ila ikitokea taasisi inataka wasomewe na viongozi ni kinyume na bibilia ndio maana napongeza juhudi hizi za Sala na Kazi za kuwataka msome bibilia kikatoliki angalau.

Maandiko yanapaswa kufundishwa kuanzia nyumbani, Ndilo agizo la Mungu Torati 6, Hutakiwi kuhadithiwa bibilia unatakiwa usome bibilia kuhakiki unachofundishwa na makasisi (waberoya wa kitabu ca matendo)
Timotheo anaandikiwa na Paulo afanye Bidii katika KUSOMA.
Ufunuo inaanza na '' HERI ASOMAYE''.

hivyo nawapongeza kwa juhudi ila mmechelewa, hiyo misisitizo ilianza tangu watunwa Mungu wako Jangwani. Ndio maana hadi kesho sisi wakosefu huwa tunashangaa ni kifungu gani mlitumia kuchoma bibilia na kushughulikia kila aliyeonyesha juhudi kutafsiri bibilia katika lugha za watu husika ili kuongeza spidi ya uinjirishaji. Isingekuwa Bidii za reformers kusingekuwa hata na hiyo Douay .
 
34Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo kidogo,
kuhusu kuwa either FARISAYO or MUANDISHI/MWALIMU au vyote pamoja nimekueleza mara mbili kirefu huko juu. so hapo ninaona labda ni kiburi tu na uoga wa kukiri kosa

na ndio maana nimekuuliza maswali hapo juu HUJANIJIBU zaidi ya kunipa qoutation. na zaidi ninaweza kuomba kujua kuwa je, kila aliyeitwa MUANDISHI/MUALIMU alikuwa ni FARISAYO ? au WAANDISHI waliweza kuwa wafuasi wa kikundi chochote ??
ninachokataa ni kisema hakuna farisayo aliyekuwa mjuzi wa maandiko
onesha ni wapi ambapo nimedai ivyo ?
jitahidi kusoma vizuri na kuelewa nilichoandika mwanzo
Kauli hii iliibua mgogoro wa kitheolojia kati ya mafarisayo na masadukayo. Sio waandishi. hivyo ujue kuwa hawakuwa vilaza wa maandiko. Hii inaonyesha wahusika walikuwa na uelewa wa maandiko.
kukosa/kutokuwa na elimu ya UANDIHI/SHERIA haina maana ya kuwa wewe ni kilaza wa torati au maandiko nq hakuna mahali nimedai ivo. ninachozungumzia mimi ni taaluma na sio kujua/ujuaji kama unavotaka ieleweke
Kuhusu waandishi na waalimu nakubaliana na wewe.
unakubaliana kwa lipi kwamba "waandishi na waalimu wa sheria" lilikuwa kundi moja au makundi mawili tofauti ?? na je walikuwa ni dhehebu la kidini kama madhebu mengine farisayo, sadukayo nk au walikuwa wanajitegemea ?
 

Naona una ubishi Wa kuzaliwa. Nitaleta mada spesheli kwa ajili ya suala la Elimu ya Yesu.
 
Usinihukumu mkuu; mimi sio msabato wala dhehebu lolote. Nitachokifanya ni kutafuta ukweli ili niwe huru. Kila dhehebu lina mapungufu yake.
 
maswal yangu yalikuwa ni haya hapa chini ninayarudia
kwenye uzi wangu hakuna mahali nimezungumzia WASABATO na REFORMERS so
tetea unachokidai juu ya uzi na sio hisia
 
Naona una ubishi Wa kuzaliw
kuna kundi la watu ambao furaha yao kubwa huwa ni kubisha. hata utumie muda na energy kubwa kiasi gani. hawezi acha kubisha sababu hapo ndipo furaha yake ilipo lala.

hata kitu kiwe obvious namna gani ni lazima abishe tu sababu hiyo ndio furaha yake. usipomgundua mtu wa kundi kama hilo utajikuta unajiumiza mwenyewe.

hao huwa tunawaita "SOPHIST" nature na tatizo lao sio ubishi ila ni ubishi bila logoc na sababu za msingi. yeye ilimradi kabisha basi imetoka iyo
 
Naona una ubishi Wa kuzaliwa. Nitaleta mada spesheli kwa ajili ya suala la Elimu ya Yesu.
Huyo kijana ndio tabia yake,usipo muelewa na kumchukulia alivyo utaumia,kule kwenye ule Uzi wako nitamrudia nikiwa na wakati Mzuri...,

Me sijaona sababu ya yeye kuanzisha ubishi kwenye huu Uzi,tumemkaribisha kwenye semina lkn anakuwa mbishi tuu...,ila nilishamgundua huyo bwana mdogo huwa ana allergy na Wakatoliki....,
 


πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna kitu wanaogopa.........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…