Karma Haipo, Karma ni dhana ya kimaskini kuwafariji maskini

Karma Haipo, Karma ni dhana ya kimaskini kuwafariji maskini

Infropreneur

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2022
Posts
9,830
Reaction score
20,686
Karma Doesn't exist.

Karma ni dhana ya kimaskini inayowapa matumaini uchwara watu maskini kujifariji na matatizo yao dhidi ya watesi wao.

Mababu zetu waliteswa sana na kusulubishwa ipasavyo wakati wa utumwa na ukoloni, Lakini hiyo karma haijawahi kufanya, haijafanya na haitakaa ifanye chochote dhidi ya wazungu.

Waafrika wamebaki maskini na wazungu wanazidi kuwa matajiri.

Unafikiri matajiri watateseka kwa sababu ya kudhulumu maskini kisa eti kuna karma?

Haitakaa itokee, Sahau na futa hii dhana kabisa akilini mwako.

Tuanze tu hapa Afrika. Watawala wengi na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwahujumu wananchi wao kwa ufisadi, wizi wa fedha za umma, ubadhirifu wa mali za umma na kuwasulubu raia wao kwa kuwatwanga kodi kubwa.

Wananchi wanabaki kulia lia tu, Mara oooh! Tunamwachia Mungu, Mungu atatenda, Mungu atafanya, Mungu atatulipia, Wengine wanajifariji Karma itawafunza viongozi wao!! Na maneno mengi ya kujifariji. Lakini mwisho wa siku hakuna kinacho tokea.

Watawala na vizazi vyao wanazidi kuneemeka na kutajirika huku wananchi walala hoi na vizazi vyao wanazidi kuwa makapuku, makabwela, mafukara na maskini choka mbaya pangu pakavu tia mchuzi.

The rich goes richer, the poor goes poorer.

Kama karma ingekuwa inafanya kazi kweli, Manung'uniko yote ya wananchi maskini kudhulumiwa na wanasiasa matajiri yangefanya karma iwafikie wanasiasa wote na kuwafanya wabadilike.

Lakini hakuna kinachotokea na karma haionekani kusaidia chochote zaidi ya kuwapa matumaini uchwara tu, wadhulumiwa watu maskini.

Maskini wanazidi kuwa maskini na manung'uniko yao na matajiri wanazidi kuwa matajiri licha ya kuwadhulumu maskini.

Karma is an illusion.

Forget about karma, Make your own money live the best life you can live. Stop hoping that karma will catch up with your oppressors. It won't.

Never think that the rich will suffer because they oppress the poor. Never they won't.

Mababu zetu waliteswa sana na wakoloni na hiyo karma haikufanya chochote.

Watawala na viongozi wa Afrika wanazidi kuwatesa waafrika na hiyo karma haifanyi chochote.

Karma doesn't exist. In the jungle of life salvation is largely on your hands.

I'm out.
 
Kuna jambo lipo hivi....tujaribu kuwaza hao wanaotenda ubaya dhulma Kuna eneo la pili husaidia watu na huo upande wanaonekana ni malaika so sisi waliotudhulum tukiwaombea mabaya Kuna upande wanaombew mema...then hata sisi ambao tunatendew ubaya Kuna angle pia tunafanya mazito ya kuumizan
 
Kuna jambo lipo hivi....tujaribu kuwaza hao wanaotenda ubaya dhulma Kuna eneo la pili husaidia watu na huo upande wanaonekana ni malaika so sisi waliotudhulum tukiwaombea mabaya Kuna upande wanaombew mema...then hata sisi ambao tunatendew ubaya Kuna angle pia tunafanya mazito ya kuumizan
Maombi ni illusion tu.

Hayana impact yeyote kwa watu. Zaidi ya kujifariji na kujipa matumaini uchwara tu.
 
Mkuu,
Hujaona uzao wa akina Tip Tip wanavyoteseka pale Mashariki ya Kati?!

Ule ukatili wa kubebesha watumwa mizigo mizito, ikiwemo ya pembe za ndovu, nk, huku wamefungwa minyororo na kutembea umbali mrefu sana, kutoka Kigoma, Tabora.. hadi Pwani usingepita hivi hivi
 
Mkuu,
Hujaona uzao wa Tip Tip wanavyoteseka pale Mashariki ya Kati?!

Ule ukatili wa kubebesha watumwa mizigo ya pembe za ndovu, nk, huku wamefungwa monyororo, kutoka Kigoma, Tabora.. hadi Pwani usingepita hivi hivi
Watu hawateseki kwa sababu ya karma.

Watu wanateseka kutokana na ujinga na umaskini wao.
 
Hakuna mkuu.

Cha msingi watu wajifunze na wajue hakuna karma itakuja kuwasaidia.

Waache kujipa matumaini feki ya kwamba kuna karma itawapiga watesi wao.

Kila mtu ajipambanie, Asidhani kuna karma itawapiga watesi wake.
Sikupingi mkongwe. Japo tunaomba ungetupumzisha kidogo, ukweli wako unatuumiza kiasi.

Maana kama watoto tunao wa kutosha kuunda kampuni. Viapo vya karma ndio sehemu ya maisha yetu ndugu na rafiki wakitutendea mambo ambayo hayatupi nafuu ya maisha tuliyoyachagua.
 
Karma is real alafu karma inavyofanya kazi inakuwa personal malipo unayalipa personal kama ulivyokuwa unatenda personal basi na malipo yanakuwa personal, alafu malipo ya karma hayana kelele kabisa hata wewe unalipa hayo malipo unakuwa haujui kama unalipa.
 
Kwan unadhani UKIUA KWA UPANGA nawe utauwawa kwa UPANGA ndo itimie karma
Ama unadhani ukiwa unapenda kutembea na wake za watu basi unadhani Karma ni lazima iwe kma hvyo watu waje watembee na mke wako pia

Big NO MWENYEZIMUNGU atakulipa karma yako kwa mtindo wowote mpk MOYONI mwako mwenyewe utang'amua na kujisemea moyoni HAKIKA HAYA NDIO MALIPO YA UBAYA WANGU

karma inalipwa katika MOYO wako kwa misukosuko itakayokutesa mpk utalia mwenyewe na kujutia kuwa haya sasa ni malipo yangu kwa mabaya yangu niliyoyatenda

Kila mja mfanya maovu atalipwa kwa namna yoyote hapa DUNIANI kwa yale mabaya aliyoyatenda na si lazima mpk watu waone kuwa amelipwa kwa ubaya wake lah ni NAFSI yake mwenyewe ndio itaweweseka kwa kihoro namna mambo yanavyomuendea si lazima mpk pesa alozipata kwa damu zimuondoke kuwa masikini lah anaweza kuwa nazo zaidi na zikawa Zinaongezeka ila SHIDAna majuto yanayomsonga hata hizo fedha hazitamani tena wala kuona faida yake
Hujawai sikia msemo wa kiswahili KUFA HAFI ILA CHAMOTO ANAKIONA

MALIPO NI DUNIANI AKHERA HUESABIWA KATI YA DHAMBI NA MEMA YAKO THEN UTATUPWA UNAKOSTAHILI
 
Back
Top Bottom