Karma Haipo, Karma ni dhana ya kimaskini kuwafariji maskini

Karma Haipo, Karma ni dhana ya kimaskini kuwafariji maskini

Haya mambo ya kusema eti tunamwachia Mungu ni upumbavu wa hali ya juu.

Mungu hajishughulishi wala hajihusishi na kulipa visasi. Mungu hawezi kamwe kumuuwa mtu eti kwa sababu mtu huyo aliuwa au kudhulumu watu wengine, hakuna jambo kama hilo.

Mtu anaweza kujiuwa mwenyewe. Anaweza kuuawa na watu wengine. Anaweza kufa kifo cha asili.

Uovu unafanywa na binadamu. Kwa sababu hiyo wao ndiyo wana jukumu la kuuondoa.

Mungu hafanyi uovu na hachangamani nao.

Watu hawateseki eti kwa sababu Mungu analipiza kisasi kutokana na matendo yao, hapana.

Watu wanateseka na shida mbalimbali kwa sababu wanakataa Mungu: Kwa sababu wanakataa ukweli; kwa sababu wanakataa kufanya jitihada zinazofaa kuondoa uharibifu uliotokea kutokana na makosa.
 
Kwanza huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Karma Doesn't exist.

Karma ni dhana ya kimaskini inayowapa matumaini uchwara watu maskini kujifariji na matatizo yao dhidi ya watesi wao.

Mababu zetu waliteswa sana na kusulubishwa ipasavyo wakati wa utumwa na ukoloni, Lakini hiyo karma haijawahi kufanya, haijafanya na haitakaa ifanye chochote dhidi ya wazungu.

Waafrika wamebaki maskini na wazungu wanazidi kuwa matajiri.

Unafikiri matajiri watateseka kwa sababu ya kudhulumu maskini kisa eti kuna karma?

Haitakaa itokee, Sahau na futa hii dhana kabisa akilini mwako.

Tuanze tu hapa Afrika. Watawala wengi na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwahujumu wananchi wao kwa ufisadi, wizi wa fedha za umma, ubadhirifu wa mali za umma na kuwasulubu raia wao kwa kuwatwanga kodi kubwa.

Wananchi wanabaki kulia lia tu, Mara oooh! Tunamwachia Mungu, Mungu atatenda, Mungu atafanya, Mungu atatulipia, Wengine wanajifariji Karma itawafunza viongozi wao!! Na maneno mengi ya kujifariji. Lakini mwisho wa siku hakuna kinacho tokea.

Watawala na vizazi vyao wanazidi kuneemeka na kutajirika huku wananchi walala hoi na vizazi vyao wanazidi kuwa makapuku, makabwela, mafukara na maskini choka mbaya pangu pakavu tia mchuzi.

The rich goes richer, the poor goes poorer.

Kama karma ingekuwa inafanya kazi kweli, Manung'uniko yote ya wananchi maskini kudhulumiwa na wanasiasa matajiri yangefanya karma iwafikie wanasiasa wote na kuwafanya wabadilike.

Lakini hakuna kinachotokea na karma haionekani kusaidia chochote zaidi ya kuwapa matumaini uchwara tu, wadhulumiwa watu maskini.

Maskini wanazidi kuwa maskini na manung'uniko yao na matajiri wanazidi kuwa matajiri licha ya kuwadhulumu maskini.

Karma is an illusion.

Forget about karma, Make your own money live the best life you can live. Stop hoping that karma will catch up with your oppressors. It won't.

Never think that the rich will suffer because they oppress the poor. Never they won't.

Mababu zetu waliteswa sana na wakoloni na hiyo karma haikufanya chochote.

Watawala na viongozi wa Afrika wanazidi kuwatesa waafrika na hiyo karma haifanyi chochote.

Karma doesn't exist. In the jungle of life salvation is largely on your hands.

I'm out.
Dhana ya karma ni moja wapo ya imani za kiroho zinazotofautiana kati ya tamaduni na dini, na mitazamo kuhusu uwepo wake au kutoonekana kwake ni jambo linalovutia mijadala. Hapa nitachambua mada yako kwa mtazamo wa usawa, ikijumuisha changamoto unazozungumzia pamoja na mapendekezo ya hatua.

1. Kuelewa Karma

  • Kihistoria na Kiimani:
    Karma ni dhana inayotokana na dini za Mashariki kama Hinduism, Buddhism, na Jainism. Kwa mtazamo huu, karma hurejelea matokeo ya matendo ya mtu—mazuri au mabaya—ambayo yanaweza kujitokeza katika maisha haya au yajayo.
  • Kama Mfumo wa Kimantiki:
    Kwa wengine, karma ni mfano wa kimaadili unaoonyesha kwamba matendo yetu yana athari, ingawa si lazima athari hizo ziwe za moja kwa moja au za haraka.

2. Changamoto Unazotaja

  • Uonevu na Ukandamizaji wa Wanyonge:
    Historia ya ukoloni na ukandamizaji wa mataifa maskini ni ushahidi wa dhuluma zilizofanywa bila kuonekana "malipo ya karma" ya haraka kwa wanyonyaji. Hii imechangia mtazamo kuwa karma haifanyi kazi.
  • Ufisadi na Ubaguzi wa Kijamii:
    Katika nchi nyingi, viongozi wanaotumia vibaya mamlaka zao mara nyingi hawaonekani kupata adhabu kwa vitendo vyao, na hali hii inawakatisha tamaa wengi.

3. Hoja ya Kwamba Karma Ni "Dhana ya Maskini"

  • Matumaini na Faraja:
    Kwa wanyonge, dhana ya karma mara nyingi hutumika kama faraja ya kiroho. Hii si mbaya kwa dhana, bali inaweza kuwa hatari ikiwa itatumika kama kisingizio cha kutochukua hatua.
  • Ukosefu wa Nguvu:
    Wakati watu hawana njia ya moja kwa moja ya kupambana na dhuluma, wanaweza kugeukia dhana kama karma au imani za kidini ili kupata matumaini na subira.

4. Kwa Nini Hali Haiwezi Kugeuka Papo Hapo?

  • Mfumo wa Kijamii:
    Athari za dhuluma za kihistoria, kama ukoloni, zimerithiwa kupitia mifumo ya kiuchumi na kijamii inayodumisha ukosefu wa usawa. Kubadilisha hali hii kunahitaji juhudi za pamoja na muda mrefu.
  • Kukosekana kwa Uwajibikaji:
    Wakati viongozi wanapokosa uwajibikaji na mifumo ya kisheria haifanyi kazi, athari za matendo yao hazionekani mara moja. Lakini hii haimaanishi kwamba malipo hayawezi kuja kwa njia nyingine.

5. Njia za Kupambana na Dhuluma

  • Kuchukua Hatua za Moja kwa Moja:
    Badala ya kusubiri karma, jamii inaweza kuchukua hatua za kupambana na dhuluma, kama kudai uwajibikaji, kuimarisha mifumo ya kisheria, na kuwekeza katika elimu na maendeleo.
  • Kujenga Nguvu za Kijamii:
    Umoja wa kijamii na ushawishi wa pamoja vinaweza kuwa chombo bora cha kuleta mabadiliko, badala ya kutegemea dhana za kiroho pekee.

6. Hitimisho

Dhana ya karma inaweza kuwa na maana kwa baadhi ya watu kama njia ya kuelewa maisha na maadili, lakini si lazima iwe msingi pekee wa matumaini ya kupambana na dhuluma. Dunia yetu inahitaji hatua za dhati, mshikamano wa kijamii, na mabadiliko ya mifumo ya kijamii na kiuchumi ili kuleta usawa.

Kama ulivyosema, maisha ni msitu, na wokovu mara nyingi uko mikononi mwa kila mtu. Hata hivyo, matumaini na juhudi vinaweza kuunganishwa ili kuleta mabadiliko halisi.
 
Haya mambo ya kusema eti tunamwachia Mungu ni upumbavu wa hali ya juu.

Mungu hajishughulishi wala hajihusishi na kulipa visasi. Mungu hawezi kamwe kumuuwa mtu eti kwa sababu mtu huyo aliuwa au kudhulumu watu wengine, hakuna jambo kama hilo.
Mkuu ukisikia mtu anakwambia anamwachia Mungu ogopa Sana...Kama unaweza mwombe radhi mapema maana anaenda kukutengenezea majanga Yeye mwenyewe.
 
Karma Doesn't exist.

Karma ni dhana ya kimaskini inayowapa matumaini uchwara watu maskini kujifariji na matatizo yao dhidi ya watesi wao.

Mababu zetu waliteswa sana na kusulubishwa ipasavyo wakati wa utumwa na ukoloni, Lakini hiyo karma haijawahi kufanya, haijafanya na haitakaa ifanye chochote dhidi ya wazungu.

Waafrika wamebaki maskini na wazungu wanazidi kuwa matajiri.

Unafikiri matajiri watateseka kwa sababu ya kudhulumu maskini kisa eti kuna karma?

Haitakaa itokee, Sahau na futa hii dhana kabisa akilini mwako.

Tuanze tu hapa Afrika. Watawala wengi na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwahujumu wananchi wao kwa ufisadi, wizi wa fedha za umma, ubadhirifu wa mali za umma na kuwasulubu raia wao kwa kuwatwanga kodi kubwa.

Wananchi wanabaki kulia lia tu, Mara oooh! Tunamwachia Mungu, Mungu atatenda, Mungu atafanya, Mungu atatulipia, Wengine wanajifariji Karma itawafunza viongozi wao!! Na maneno mengi ya kujifariji. Lakini mwisho wa siku hakuna kinacho tokea.

Watawala na vizazi vyao wanazidi kuneemeka na kutajirika huku wananchi walala hoi na vizazi vyao wanazidi kuwa makapuku, makabwela, mafukara na maskini choka mbaya pangu pakavu tia mchuzi.

The rich goes richer, the poor goes poorer.

Kama karma ingekuwa inafanya kazi kweli, Manung'uniko yote ya wananchi maskini kudhulumiwa na wanasiasa matajiri yangefanya karma iwafikie wanasiasa wote na kuwafanya wabadilike.

Lakini hakuna kinachotokea na karma haionekani kusaidia chochote zaidi ya kuwapa matumaini uchwara tu, wadhulumiwa watu maskini.

Maskini wanazidi kuwa maskini na manung'uniko yao na matajiri wanazidi kuwa matajiri licha ya kuwadhulumu maskini.

Karma is an illusion.

Forget about karma, Make your own money live the best life you can live. Stop hoping that karma will catch up with your oppressors. It won't.

Never think that the rich will suffer because they oppress the poor. Never they won't.

Mababu zetu waliteswa sana na wakoloni na hiyo karma haikufanya chochote.

Watawala na viongozi wa Afrika wanazidi kuwatesa waafrika na hiyo karma haifanyi chochote.

Karma doesn't exist. In the jungle of life salvation is largely on your hands.

I'm out.
karma ipo,wakati wazungu wakiwatesa waafrika,,,ikabuka vita za 1 na 2 za dunia baina yao,,,na ,nagasaki na hiroshima ikachapwa,kama unakumbuka magaidi wa kiislam waloua waafrika,leo hii wanachezea kichapo kutoka israil,wakati wamarekani wakitulazimsha tufirane,leo hii trump anasema wazi,,akiingia madarakani anapiga marufuku usenge<<<wazungu walipolipoa virusi vya KORONA walisema maiti zitaokotwa barabarani AFRIKA, kuja kustuka wao ndo wakawa wanakufa balaa,ikawalazimu kuanzisha chanjo,,,,ata HIV ivoivo,,,,wakati wamarekani na ulaya wakisponsa watu wauane afrka,,leo hii marekani inaongoza kwa raia wake kuuana wenyewe kwa wenyewe,,wakati wazungu wakikataa kutoa ela za tabia nchi,,kila siku tuanasikia wamarekani wakikumbwa na vimbunga vya mara kwa mara !!!,,,wakati wakisema waafrika hatuna akili sasa tunashuhudia vijana wa ulaya wakiwa hawana akili kwa ajili ya kubwia unga!!!,,,,walipotulazimisha haki sawa kati ya mwanamke na mwanaume,,wao sasa wameanza kuweka usawa kati yao na maroboti,,,,wakti wakisema afrika hamna ajira,,,wao ajira zinaongezeaka kwa maroboti wakati raia wakiwa benchi!
 
Lakini hiyo karma haijawahi kufanya, haijafanya na haitakaa ifanye chochote
Nakubaliana na wewe mleta mada, Karma haipo.

Lkn labda tuiweke hivi "endapo mtenda maovu ana hofu na atayaweka akilini maovu aliyoyatenda, ndipo huanza kuathiri saikolojia yake na hatimaye kuathiri afya na kupelekea kifo. Hiki ndicho watu huita Karma.

But for heartless and remorseless people karma is unrealistic and nonexistent thing.
 
karma ipo,wakati wazungu wakiwatesa waafrika,,,ikabuka vita za 1 na 2 za dunia baina yao,,,na ,nagasaki na hiroshima ikachapwa,kama unakumbuka magaidi wa kiislam waloua waafrika,leo hii wanachezea kichapo kutoka israil,
Hata waafrika bado tunapigana vita na kuuana wenyewe kwa wenyewe.

Rejea mauaji ya kimbari Rwanda, Vita vya kagera, Biafran war Nigeria.

Vita mbalimbali bado zinaendelea Afrika huko Congo waasi wa ADF wanaua raia, Tigray Ethiopia watu wana uana sana, Cabo Delgado Msumbiji, Al Shabaab Somalia, Boko Haram,

Hata Tanzania tu watu wanauwawa na watu wasiojulikana.

Na vita vyote hivi si kwa sababu ya Karma, Bali ujinga wetu tu.
wakati wamarekani wakitulazimsha tufirane,leo hii trump anasema wazi,,akiingia madarakani anapiga marufuku usenge<<<wazungu walipolipoa virusi vya KORONA walisema maiti zitaokotwa barabarani AFRIKA, kuja kustuka wao ndo wakawa wanakufa balaa,ikawalazimu kuanzisha chanjo,,,,ata HIV ivoivo,,,,wakati wamarekani na ulaya wakisponsa watu wauane afrka,,leo hii marekani inaongoza kwa raia wake kuuana wenyewe kwa wenyewe,,
Watu weusi ndio wana ongoza kuuana wenyewe kwa wenyewe. Kushinda hata wazungu.
wakati wazungu wakikataa kutoa ela za tabia nchi,,kila siku tuanasikia wamarekani wakikumbwa na vimbunga vya mara kwa mara !!!,
Marekani kukumbwa na vimbunga si Karma, Bali ni hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi tu.

Hata hapa Afrika mbona tunapigwa na majanga ya asili mbalimbali.

Rejea tetemeko la ardhi la Kagera, mafuriko ya Libya, tetemeko la ardhi la Morocco. Mafuriko ya Kwa zulu Natal south Africa n.k
,,wakati wakisema waafrika hatuna akili sasa tunashuhudia vijana wa ulaya wakiwa hawana akili kwa ajili ya kubwia unga!!!,
Hata hapa Tanzania tu, Vijana wanabwia unga. Nenda kwa wadudu Arusha chuga ukajionee, Au nenda Nairobi Kenya mitaa ya Dandora au Kibera Slums ukajionee wala ngada.

Kwa hiyo vijana wa ulaya kubwia unga si Karma ni tabia zao tu kama ilivyo kwa vijana wetu wabwia unga hapa Afrika.
,,,walipotulazimisha haki sawa kati ya mwanamke na mwanaume,,wao sasa wameanza kuweka usawa kati yao na maroboti,,,,wakti wakisema afrika hamna ajira,,,wao ajira zinaongezeaka kwa maroboti wakati raia wakiwa benchi!
Kwa hiyo matendo yote haya si Karma.

Bali ni matendo ya kibinadamu na mengine ya kijiografia kama majanga ya asili vimbunga, mafuriko n.k
 
Nakubaliana na wewe mleta mada, Karma haipo.

Lkn labda tuiweke hivi "endapo mtenda maovu ana hofu na atayaweka akilini maovu aliyoyatenda, ndipo huanza kuathiri saikolojia yake na hatimaye kuathiri afya na kupelekea kifo. Hiki ndicho watu huita Karma.

But for heartless and remorseless people karma is unrealistic and nonexistent thing.
Yeah sure.
 
Kuna jambo lipo hivi....tujaribu kuwaza hao wanaotenda ubaya dhulma Kuna eneo la pili husaidia watu na huo upande wanaonekana ni malaika so sisi waliotudhulum tukiwaombea mabaya Kuna upande wanaombew mema...then hata sisi ambao tunatendew ubaya Kuna angle pia tunafanya mazito ya kuumizan
Hili jibu lipo sawa kabisa
 
Back
Top Bottom