kidole cha simba
JF-Expert Member
- Jun 3, 2022
- 1,994
- 2,510
ok!!
siwezi kueleza mambo mengi,,,ila ipo siku utujua ukweli>time will tell"Hata waafrika bado tunapigana vita na kuuana wenyewe kwa wenyewe.
Rejea mauaji ya kimbari Rwanda, Vita vya kagera, Biafran war Nigeria.
Vita mbalimbali bado zinaendelea Afrika huko Congo waasi wa ADF wanaua raia, Tigray Ethiopia watu wana uana sana, Cabo Delgado Msumbiji, Al Shabaab Somalia, Boko Haram,
Hata Tanzania tu watu wanauwawa na watu wasiojulikana.
Na vita vyote hivi si kwa sababu ya Karma, Bali ujinga wetu tu.
Watu weusi ndio wana ongoza kuuana wenyewe kwa wenyewe. Kushinda hata wazungu.
Marekani kukumbwa na vimbunga si Karma, Bali ni hali ya hewa na mabadiliko ya tabia ya nchi tu.
Hata hapa Afrika mbona tunapigwa na majanga ya asili mbalimbali.
Rejea tetemeko la ardhi la Kagera, mafuriko ya Libya, tetemeko la ardhi la Morocco. Mafuriko ya Kwa zulu Natal south Africa n.
Hata hapa Tanzania tu, Vijana wanabwia unga. Nenda kwa wadudu Arusha chuga ukajionee, Au nenda Nairobi Kenya mitaa ya Dandora au Kibera Slums ukajionee wala ngada.
Kwa hiyo vijana wa ulaya kubwia unga si Karma ni tabia zao tu kama ilivyo kwa vijana wetu wabwia unga hapa Afrika.
Kwa hiyo matendo yote haya si Karma.
Bali ni matendo ya kibinadamu na mengine ya kijiografia kama majanga ya asili vimbunga, mafuriko n.k