Wanabodi
leo asubuhi nimesoma post ya mwana jf huyu,nikaguswa,kuzungumzia hiki kitu kinachoitwa karma。Karma ni what goes around,comes around!
The Power of Karma- Ndio hukumu pekee ya haki kamili hapa Duniani. Unahukumiwa kwa matendo yako!
Hii karma is real na ipo kweli!,everything happens for a reason!, japo hakuna ajuaye kwanini yule alitwaliwa, lakini there was a reasons,kuna sababu fulani, sisi wa jicho la tatu,tuliziona,tukazisema, tukaziandika, tukapuuzwa, akatwaliwa!。
Kwa vile hakuna ajuaye sababu haswa ni nini zilizopelekea yeye kutwaliwa, lakini a bad karma inaweza kuwa imechangia!。
Sasa tunapoanza kuona zile sababu za bad karma kama za wakati ule,zinaanza kujirudia wakati huu, hatuwezi kunyamaza,
Wasaidizi wa Rais Samia,
mnawajibu wa kumsaidia Rais Samia na serikali yake kuepuka mambo yanayoweza kusababisha a bad karma!。
Kwa upande wangu,mambo yanayosababisha a bad karma kwa Rais wa JMT, ni mambo mawili
1. Vitendo viovu vya kusabasha watu waumie,walie na wavuje machozi,jasho na damu za Watanania,
2. Ukosekanaji wa haki ndani ya JMT,zikiwemo haki jinai,haki siasa,haki katiba,haki sheria,na haki uchaguzi kwa kutofanya uchaguzi huru na wa haki,bao la mkono na figisu figisu
Hapa naweka baadhi ya matukio ya bad karma ya awamu iliyopita,nikionyesha nilishauri nini awamu ile,na nimeshauri nini awamu hii。
Enzi ya JPM
Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Awamu ya SSH
Pre GE2025 - Baada ya Mtu Kusema Ukweli Kuhusu Uchaguzi Kuendeshwa kwa Mutatis Mutandis, Tunaomba Uchaguzi Mkuu wa 2025 Uendeshwe kwa Ceteris Peribus!
Kabla ya uchaguzi wa serikali, 2024,nikamsisitizia mtu wetu
Pre GE2025 - LGE2024 - Ombi Maalum, Kwa Mtu Maalum Achana na Hizi Mutatis Mutandis Kwenye Chaguzi za SM2024 & U/Mkuu2025, Tumia Ceteris Peribus, Utabarikiwa, Tutabarikiwa!
Ushauri huu,ulipuuzwa, tukafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mutatis mutandis zile zile kama za 2019, na sasa zimebaki siku 30 za mwisho kabla ya Bunge kuvunjwa,
https://www.jamiiforums.com/threads...r-tufanye-tu-illegal-elections.2346113/,hivyo tunakwenda kufanya tena uchaguzi mkuu wa 2025 kwa mutatis mutandis zile zile za uchaguzi wa 2020!,tukipata matokeo kama ya 2020, pia tuwe tayari kuyapokea na yatokanayo !。
Hitimisho
Tukiweza kuepuka bad karma,tuepuke,tusiipe karma sababu!
Paskali