Wanabodi,
Kwa muda mrefu taifa letu limekuwa likisumbuliwa na kuhangaika na kundi la watu wanaitwa "wasiojulikana", wanaofanya vitendo viovu ikiwa ni pamoja na utekaji, utesaji, na mauaji, na miili kutoonekana, na mingingine kuiweka miili kwenye viroba, na kuitupa mtoni, ziwani au baharini, baadhi ya miili iliyofungwa vibaya, huibuka juu ya maji na kuonekana ikiwa imefungwa kwenye viroba.
Miongoni vya watu waliofanyiwa uhalifu huo ni pamoja na kiongozi wa mgomo wa madaktari, Dr. Ulimboka, Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Absolom Kibanda, Mwandishi wa habari wa Mwananchi, Azory Gwanda, mwana JF maarufu Ben Saanane, na wengine wengi. Vitendo hivi vilifika peak, pale Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa kumiminiwa marisasi ya kutosha, mchana kweupe akiwa katika makazi rasmi ya Wabunge, yenye ulinzi imara 24/7 jijini Dodoma.
Kwa vile mimi sio polisi bali tasnia yetu ya habari, ni Mhimili wa Nne, usio rasmi ambao una baadhi ya waandishi wenye uwezo wa kuandika stori za uchunguzi, Investigative Journalism, hivyo tunaweza kusaidia, na mimi ni mmoja wa waandishi wa kundi hili, hivyo tukajitolea kuwapa polisi lead ya pakuanzia,
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija
Paskali