Karne ya 21 Katibu Mkuu wa CWT alikuwa mwalimu wa Daraja la 3A?

Karne ya 21 Katibu Mkuu wa CWT alikuwa mwalimu wa Daraja la 3A?

95% ya members wa Congress pale US wana college degrees. 90% ya members wa House of Commons Uingereza wana college degrees.
Alafu kwetu tunaopokea misaada ya kujenga vyoo mtu anataka darasa la saba wawe wagombea. Haohao ndio wajadili mikataba ya madini, gesi, bandari na kupitisha sheria za uwekezaji na miradi.

Kila kitu kina standards. Mbona kwenye uchaguzi hawaruhusiwi watoto, wageni, wasiojua kusoma na kuandika na wanajeshi ili wananchi waamue wenyewe wanamchagua nani.
Wewe kagombee na hao wa la Saba uwashinde kwa kutumia elimu yako, kama huwezi kuwashinda Wajinga wajinga wa la Saba kwny uchaguzi unaweza ukayashinda matatizo ya watanzania ?

au wasomi mnataka mpate mseleleko wa viti maalum kama walemavu na wanawake?

Bunge letu lina graduate wengi tu wa kutosha, mbona kwny kujenga hoja na kujiamini huko huko Bungeni wanazidiwa kwa mbali tu na hao wa la saba?

inaonekana umekariri sana formal Education. kwa hiyo kwny mambo ya uwekezaji na biashara tumuamini Lecturer kwny ma PhD na ma Presentation Lukuki ya kibiashara wakati hana biashara hata ya kuuza pipi ili atupe uhalisia tuache kumuamini Jumanne Kishimba ambae hata Supermarket ya Kwanza nchini kuleta yeye miaka zaid ya 40 iliyopita ( Imalaseko Super market) wakati huo watu walikuwa wanakariri tu Supermarket darasani?

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Kwa mawazo yenu haya, vijana mna safari ndefu sana. Uongozi ni kipaji kisichoitaji PhD ili kuongoza watu. Niambieni, ni Rais yupi hasa wa nchi zilizoendelea anaejinasibu kwa U-udoctor au u-professor wake? Hii kasumba ya kuchaguana na kuteuana kwa misingi ya vyeti tu na uchawa iko hapa kwetu. Kwingineko kinachoangaliwa pamoja na academic qualifications ni professionalism, experience na integrity ya mtu.

Kuongoza chama Cha walimu hakuitaji hiyo Masters yako.

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania ili upate cheo kikubwa kuwa na number nyingi za waganga
 
Umeniteua sitaki, sasa kosa lake nini? Akafanye kazi ambayo hakuitaka? Huenda ndoto yake haijawahi kuwa ukuu wa wilaya.
Mbona hushangai wabunge wapitisha mikataba na sheria kuwa darasa la 7 tu?
Kwani kuna shida gani si karudishwa kwenye kazi yake aliyoajiriwa nayo serikalini?

Angefukuzwa kazi ya ualimu hapo sawa tungekuwa na mjadala.
 
Nadhani humjui huyo jamaa umekurupuka tu,kifupi ana degree ya mlimani na ana CPA,nimesoma naye darasa moja namfahamu ni mtu smart!
Kwahiyo kati ya wewe usiyefahamika humu jukwaani hata utambulisho wako na serikali ambaye ni mwajiri wake tumuamini nani?

Kwahiyo awe na degree halafu awe mwalimu wa darasa la 3A?
 
Hao wasomi wakina chenge,kabudi,mdee,bulaya,mwigulu,nape,januar makamba wamelisaidia nini taifa? Bora babu yangu ambaye hakujua kusoma wala kuandika alikuwa mzalendo wa taifa lake hadi akatoa shamba lake kwa ajili wajenge shule na zahanati
hebu muondoe kwanza Nape kwenye hiyo orodha ndio tuendelee. mtu amesoma MEMKWA unamwita msomi?? kivipi??
 
Kupata vyeo Tanzania hii uwe fundi wa ushirikina ettii hao wenye Elimu kubwa wanaona Nini Cha kufia, mfano mzuri angalia Elimu za wawakilishi wetu kwenye kilinge Cha taifa hapo jangwani DODOMA.

Wasomi asilimia kubwa wanaishia kwenye vikaango vya wajumbe na ukikuta msomi kapenya ujue kajiongeza upande wa pili kwanza.
Upo sahihi mkuu.
 
Unaweza kuta ni grade 3A lakini ana degree watu wanajiendeleza wanakuwa na malengo yao, asingeweza kuteuliwa kuwa DC. Na ndugu yangu ana masters ni trafic amekataa kupeleka vyeti polisi anaogopa ataondolewa barabarani ni zaidi ya miaka 3 sasa hataki
huyo ni mla rushwa mkubwa tunaomba jina lake na namba yake
 
95% ya members wa Congress pale US wana college degrees. 90% ya members wa House of Commons Uingereza wana college degrees.
Alafu kwetu tunaopokea misaada ya kujenga vyoo mtu anataka darasa la saba wawe wagombea. Haohao ndio wajadili mikataba ya madini, gesi, bandari na kupitisha sheria za uwekezaji na miradi.

Kila kitu kina standards. Mbona kwenye uchaguzi hawaruhusiwi watoto, wageni, wasiojua kusoma na kuandika na wanajeshi ili wananchi waamue wenyewe wanamchagua nani.

La kuongezea wengi wamesomea sheria
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Unafiki ni kushangaa katibu wa CWT kuwa mwalimu wa grade 3A wakati mbunge anapaswa tu kujua kusoma ma kuandika!

Tukianzia hapo ndio tutajua huyu mwalimu alikuwa shujaa wa kutoikimbia taaluma yake kwa rushwa ya ukuu wa wilaya....
 
Wewe kagombee na hao wa la Saba uwashinde kwa kutumia elimu yako, kama huwezi kuwashinda Wajinga wajinga wa la Saba kwny uchaguzi unaweza ukayashinda matatizo ya watanzania ?
Maamuzi ya kisiasa hayaishii kwenye kugombea na kampeni, hizi ni akili za kijima. Maamuzi ya kisiasa yana athari vizazi na vizazi. Sio ukipewa vitenge na pipi ukapiga kura mgombea wako akashinda unaona siasa imeisha.
au wasomi mnataka mpate mseleleko wa viti maalum kama walemavu na wanawake?
Kuwepo kwa vigezo sio mserereko, kama ni hivyo basi na wasiojua kusoma waruhusiwe kugombea. Kwanini kuruhusu kuanzia kusoma isiwe mserereko kwa wanaojua kusoma kisha kuanzia elimu ya juu iwe mserereko kwa wenye elimu hiyo.

Kwanini mwenye miaka 18 asiruhusiwe kugombea bali mwenye kuanzia 21, ina maana ni mserereko wa wenye 21+?
Bunge letu lina graduate wengi tu wa kutosha, mbona kwny kujenga hoja na kujiamini huko huko Bungeni wanazidiwa kwa mbali tu na hao wa la saba?
Kujenga hoja hata mwendawazimu anaweza. Ni upuuzi kuamini mtu anayeropoka sana ndio ana uwezo. Na kujiamini kwenyewe mtu anaweza jiamini kwenye ujinga, hata wakaa uchi hujiamini sana.
inaonekana umekariri sana formal Education. kwa hiyo kwny mambo ya uwekezaji na biashara tumuamini Lecturer kwny ma PhD na ma Presentation Lukuki ya kibiashara wakati hana biashara hata ya kuuza pipi ili atupe uhalisia tuache kumuamini Jumanne Kishimba ambae hata Supermarket ya Kwanza nchini kuleta yeye miaka zaid ya 40 iliyopita ( Imalaseko Super market) wakati huo watu walikuwa wanakariri tu Supermarket darasani?
Hao lecturers kazi yao kuanzisha supermarket au kufundisha kuhusu supermarket?
Sasa kama hujui utofauti wa kazi ya lecturer na kazi ya mwekezaji/mfanyabiashara una uhai kichwani kweli?

Siku nyingine si utataka daktari mwanaume wa magonjwa ya kinamama naye abebe mimba.
Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Masters ni karatasi tu kama tu zilivyo PhD za kina Mwigulu Nchemba au Prof. Kabudi, Lipumba nk nk..

Kuwa na cheti cha Diploma au Shahada au Shahada mbili au Doctorate degree au PhD is just an added advantage ktk uongozi..

Uongozi ni uwezo wa ku - influence wengine positively ili kuleta matokeo tarajiwa...

Jesus Christ aliye bench mark ya ubinadamu wetu hakuwahi ku - graduate chuo chochote ili kupata cheti cha Shahada au masters au PhD lakini ndiye mtu pekee maarufu zaidi duniani na mbinguni na ndiye mtu aliyeupindua ulimwengu huu upside down..

Achana na mentality ya "vyeti vya.......". Mentality yako iwe kwenye deliverence of outcomes of what a person is doing..
 
Nadhani humjui huyo jamaa umekurupuka tu,kifupi ana degree ya mlimani na ana CPA,nimesoma naye darasa moja namfahamu ni mtu smart!
CPA si watu wa uhasibu?
Inakuaje afundishe Temeke shule ya msingi?
Au...?
 
Tatizo ni kuwa wasomi wengi toka utotoni tumeandaliwa kuwa mafisadi. Wazazi walituambia someni mje kupata kazi sehemu zenye marupurupu ambayo kwa maana nyingine ni rushwa na fedha zingine zitokanazo na uovu makazini. Kijana anayepata utajiri ghafla akiwa ndo kaanza kazi serikalini anaonekana mjanja. Hata baadhi ya wazazi kwa upumbavu wao huwalaumu vijana wao kwanini hawana maendeleo kama kijana wa mzee fulani. Mikataba yote mibovu na upigaji mkubwa wa pesa kwenye nchi hii umefanywa na wasomi wabobevu. Hili tatizo la uongozi mbovu litaisha ikiwa kila familia ikawa na uzalendo. Wazazi waache kuwaandaa mafisadi wa baadae.
 
Tatizo ni kuwa wasomi wengi toka utotoni tumeandaliwa kuwa mafisadi. Wazazi walituambia someni mje kupata kazi sehemu zenye marupurupu ambayo kwa maana nyingine ni rushwa na fedha zingine zitokanazo na uovu makazini. Kijana anayepata utajiri ghafla akiwa ndo kaanza kazi serikalini anaonekana mjanja. Hata baadhi ya wazazi kwa upumbavu wao huwalaumu vijana wao kwanini hawana maendeleo kama kijana wa mzee fulani. Mikataba yote mibovu na upigaji mkubwa wa pesa kwenye nchi hii umefanywa na wasomi wabobevu. Hili tatizo la uongozi mbovu litaisha ikiwa kila familia ikawa na Zalando. Wazazi waache kuwaandaa mafisadi wa baadae.
Tatizo linaanza na kiongozi wa juu, utakuwaje wewe mzalendo huku boss wako siyo mzalendo? ukionekana mwadilifu utaundiwa zengwe hata kufukuzwa kazi, taasisi za umma zimejaa TISS wanakazi gani kama wanashindwa kuzuia ufisadi? PM 2021 alikuta jamaa(Wizara ya fedha) wamepiga Extra duty 2B kwenye Mei mosi, akaaunda tume mpk leo umepewa mrejesho? kuna Afisa anaweza kutoa pesa nyingi hivyo bila KM na Waziri kujua? chain ya wizi inaanzia juu kushuka chini.
 
Back
Top Bottom