Karne ya 21 Katibu Mkuu wa CWT alikuwa mwalimu wa Daraja la 3A?

Karne ya 21 Katibu Mkuu wa CWT alikuwa mwalimu wa Daraja la 3A?

CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Unaweza kuta ni grade 3A lakini ana degree watu wanajiendeleza wanakuwa na malengo yao, asingeweza kuteuliwa kuwa DC. Na ndugu yangu ana masters ni trafic amekataa kupeleka vyeti polisi anaogopa ataondolewa barabarani ni zaidi ya miaka 3 sasa hataki
 
Kupata vyeo Tanzania hii uwe fundi wa ushirikina ettii hao wenye Elimu kubwa wanaona Nini Cha kufia, mfano mzuri angalia Elimu za wawakilishi wetu kwenye kilinge Cha taifa hapo jangwani DODOMA.

Wasomi asilimia kubwa wanaishia kwenye vikaango vya wajumbe na ukikuta msomi kapenya ujue kajiongeza upande wa pili kwanza.
Bila god faza hutoboi nchi ya hovyo sn hii
 
chuo gani kwa unavyofikilia kinawezatoa masters hujaelimika?? Hivi unafikiri masters ni kitu chepesiee??
Kama degree zinatoka, masters inashindikana nini?
Ninachomaanisha ni kwamba ukiwa umeelimika huwezi kuchezewa na mtu yeyote.
 
Kauli za wahenga " KILA MTAKA NASABA ..........." mtamalizia
 
Mwalimu mwenye degree ni mwalimu daraja C
Atakuwa daraja 1C,2C, 3C nk kutegemea na muda wa utumishi wake

Mwalimu mwenye diploma ni mwalimu daraja B
Atakuwa daraja 1B,2B, 3B nk kutegemea na muda wa utumishi wake

Mwalimu mwenye cheti (grade A)ni mwalimu daraja A
Atakuwa daraja 1A,2A, 3A nk kutegemea na muda wa utumishi wake
Sahihi kabisa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Uongozi ni kipaji kutoka kwa Mungu,Elimu ni nyongeza.
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Rais Samia yeye ni Form Gani zaidi ya huyo Mwalimu unayemzodoa humu?
Je!
majukumu ya katibu mkuu wa CWT ni yapi?
Na yanahitaji kiwango gani cha elimu?
Hao ma-PHD's na Ma- DK's waliojazana Bungeni na Serikalini wana lipi la kujivunia kwa wananchi kiufanisi?

Uongozi ni "Karama" zaidi ya Elimu!
 
Mwalimu mwenye degree ni mwalimu daraja C
Atakuwa daraja 1C,2C, 3C nk kutegemea na muda wa utumishi wake

Mwalimu mwenye diploma ni mwalimu daraja B
Atakuwa daraja 1B,2B, 3B nk kutegemea na muda wa utumishi wake

Mwalimu mwenye cheti (grade A)ni mwalimu daraja A
Atakuwa daraja 1A,2A, 3A nk kutegemea na muda wa utumishi wake
Hongera braza, humu jf hakuna wasomi, walio wengi ni fomfoo feilia ndo wamejazana humu.
 
Hao wasomi wakina chenge,kabudi,mdee,bulaya,mwigulu,nape,januar makamba wamelisaidia nini taifa? Bora babu yangu ambaye hakujua kusoma wala kuandika alikuwa mzalendo wa taifa lake hadi akatoa shamba lake kwa ajili wajenge shule na zahanati

Ondoa nape na marope hapo. Kama kwako unawaona ndo wasomi basi kuna tatizo.
 
Unaweza kuta ni grade 3A lakini ana degree watu wanajiendeleza wanakuwa na malengo yao, asingeweza kuteuliwa kuwa DC. Na ndugu yangu ana masters ni trafic amekataa kupeleka vyeti polisi anaogopa ataondolewa barabarani ni zaidi ya miaka 3 sasa hataki
Huyo jamaa kiwango chake cha elimu ni form four according to his document ok, acheni umbea nchi imeoza hii, viongozi elimu hawana na ndio maana hawaoni umuhimu wa katiba mpya.

Kila kitu kinachoguswa kimeoza, kila sector, kila idara, nk, kujuana na kupeana vyeo, inaumiza nchi, miktaba mibovu na ya ajabu inayoingia serikali yetu chanzo ni elimu tu.

Taifa ambalo halitaki elimu ni Taifa lililokufa!!!!
 
Uozo wa nchi hii siyo issue ni elimu kwenye ofisi za umma % kubwa wana masters lakini utendaji ni zero, tuwekeze kwenye ujuzi na uzalendo, elimu zetu ni za kukariri(makaratasi tupu) mtu ukitoa cheti anabaki kama alivyozaliwa kichwani hana ujuzi wowote na uzalendo ni zero.
 
Mkuu Mleta mada, inakuwaje unashangaa Mwl mwenye sifa asiwe kiongozi wa wenzake, wakati sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika tu!
 
Wasomi wetu Tanzania wanagombea na kina Kishimba na Msukuma wanabwaga kwny masanduku ya kura wanakuja kulia lia wanataka Katiba mpya iwazuie la Saba kugombea, kwanini Wazuiwe wakati uchaguzi ni wa wote kama hao Wananchi hawawataki wasomi kwanini muwalazimishe ?

Wasomi badala ya kujiuliza kwanini hawauziki kwa Wapiga kura wanataka wapate mteremko kwa kuweka vizingiti kwa wale wa lasaba wazuiwe kugombea.

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
95% ya members wa Congress pale US wana college degrees. 90% ya members wa House of Commons Uingereza wana college degrees.
Alafu kwetu tunaopokea misaada ya kujenga vyoo mtu anataka darasa la saba wawe wagombea. Haohao ndio wajadili mikataba ya madini, gesi, bandari na kupitisha sheria za uwekezaji na miradi.

Kila kitu kina standards. Mbona kwenye uchaguzi hawaruhusiwi watoto, wageni, wasiojua kusoma na kuandika na wanajeshi ili wananchi waamue wenyewe wanamchagua nani.
 
Uongozi ni Zaidi ya Elimu, wakati tunapata uhuru , tuliongozwa na viongozi wengi wenye elimu za kawaida kabisa, na kwa kiasi tulienda vizuri.
Hii Imani ya kuamini ili mtu awe kiongozi mzuri, ni lazima awe na cheti kikibwa, imetuletea majanga makubwa katika nchi yetu na Africa kwa ujumla.
Watu wanapambana huko vyuoni kwa kila njia, nzuri na mbaya kuhakikisha anapata cheti ili kimsadie kuiaminisha jamii, kuwa ni msomi na anafaa kuongoza watu.
Tumeona Maprofesa na PhD wengi wakipewa nafasi za uongozi na kishindwa kuonnyesha ubora wa vyeti vyao.

Tatizo sio kuonyesha ubora wa elimu, mfumo uliopo unataka uendane na matakwa na expectation za siasa.
Ukiwa too professional unaondolewa, so hata iwe msomi vipi inakulazimu kucheza na biti.

How can you be professionaly efficient wkt mfumo hautaki? Ina demand uwe politicaly efficient
 
Back
Top Bottom