Karne ya 21 Katibu Mkuu wa CWT alikuwa mwalimu wa Daraja la 3A?

Karne ya 21 Katibu Mkuu wa CWT alikuwa mwalimu wa Daraja la 3A?

Wewe.ni mpiga majungu, ungeanza kuelezea elimu yako kabla ya huyo mwalimu, ya matokeo yangu ya form four nilipata division four ya D 2 ya kiswahili na siasa.
 
Attachments

  • 93CC1BAC-3A3D-4859-B0C1-99C5CCCB4927.jpeg
    93CC1BAC-3A3D-4859-B0C1-99C5CCCB4927.jpeg
    16.5 KB · Views: 2
Uongozi ni Zaidi ya Elimu, wakati tunapata uhuru , tuliongozwa na viongozi wengi wenye elimu za kawaida kabisa, na kwa kiasi tulienda vizuri.
Hii Imani ya kuamini ili mtu awe kiongozi mzuri, ni lazima awe na cheti kikibwa, imetuletea majanga makubwa katika nchi yetu na Africa kwa ujumla.
Watu wanapambana huko vyuoni kwa kila njia, nzuri na mbaya kuhakikisha anapata cheti ili kimsadie kuiaminisha jamii, kuwa ni msomi na anafaa kuongoza watu.
Tumeona Maprofesa na PhD wengi wakipewa nafasi za uongozi na kishindwa kuonnyesha ubora wa vyeti vyao.
 
alifanyiwa staha ya kufukuzwa kistaarabu CWT akakataa, ulitaka Mamlaka ifanyaje ?…imemheshimu sana na kama ingekuwa zama za JPM halafu akatae heshma aliyopewa na Rais …

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Mbona masoud maswanya alikataa ukuu wa wilaya ya mbozi(2016) wakati wa JPM. Akaendelea kuwa meneja wa kampuni ya Tigo Kanda ya ziwa.
 
Hilo unalisema wewe, kama unafahamu hayo tueleze vizuri na ubandike matokeo yao hapa tuyaone
Muda mwingine ujinga wa mtu ni ngumu kujificha, kama wewe unayo hata hiyo stashahada au shahada basi haijakusaidia na pengine ndiyo zile za kununua,

Unaongelea kitu usichokijua halafu unakomaa kana kwamba ni kweli huu ni zaidi ya ujinga.

Ktk tangazo hawajaandika elimu yake bali wameandika cheo "mwalimu mwandamizi daraja A" na siyo "mwalimu daraja 3A"

Msomi wa kweli hujiridhisha na taarifa kabla ya kukurupuka kunakopelekea kuwa mpumbavu.
 
Hao wasomi wakina chenge,kabudi,mdee,bulaya,mwigulu,nape,januar makamba wamelisaidia nini taifa? Bora babu yangu ambaye hakujua kusoma wala kuandika alikuwa mzalendo wa taifa lake hadi akatoa shamba lake kwa ajili wajenge shule na zahanati
Babu yako Hana uzalendo wowote, ardhi Mali ya jamhuri aliirudisha Kwa wamiliki waifanyie kazi.
 
Mada za namna hii usilete tena JF. Humu wengi ni vilaza na wala umuhimu wa kuongozwa na watu wenye elimu kubwa hawauoni.

Kwanza wengi ni failures kwahiyo wanachukia wanaposikia mapendekezo ya kuhitaji wenye elimu kubwa kua viongozi. Hii nchi ni kama imelaanika vijana wanaona ufahari kuongozwa na kina ngumbalo.

Wanapenda kubeba weakness za wachache na kuzikuza. Utaskia "tulikua na baadhi ya viongozi wenye elimu kubwa lkn hakuna jema walilofanya". Yani comment za kiwaki kabisa...
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Ni ulimbukeni kuangalia elimu yake au grade yake ya kitaaluma badala ya agrissiveness yake, inherent ability,influence and confidence. Ana values kuliko hata mapropesa wengi wa nchi hii.
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Kuwa na "master" au "doctorate" digrii hakukufanyi uwe Kiongozi bora! Uongozi wa kufundishwa na kuzaliwa nao ni vitu viwili tofauti. Uongozi unahitaji mtu anayejua - mawasiliano, mahusiano na utayari wake wa kujitoa katika jamii . Uongozi hautegemei akili yake ya vyeti.
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Mchechu ana digrii moja tu ila Mwigulu ana PHD , kuwa Kiongozi ni kipaji na sio madarasa.
 
CWT ni laana!!

Walimu wapo darasani wana Masters kiongozi wao mkuu kama Katibu mkuu ni form four grade 3A?

Tena anateuliwa kuwa mkuu wa Wilaya akaringa!!
Ile ni nafasi ya utawala siyo professional ndugu yangu . Mbona kuna maraisi wana degree moja na chini yao kuna maprof????
 
alifanyiwa staha ya kufukuzwa kistaarabu CWT akakataa, ulitaka Mamlaka ifanyaje ?…imemheshimu sana na kama ingekuwa zama za JPM halafu akatae heshma aliyopewa na Rais …

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Ndio maana tunapenda katiba mpya kuondoa mamlaka za kifara kama hizo,wewe uneniteua kufanya kazi yako sio lazima kama najiona siwezi
 
alifanyiwa staha ya kufukuzwa kistaarabu CWT akakataa, ulitaka Mamlaka ifanyaje ?…imemheshimu sana na kama ingekuwa zama za JPM halafu akatae heshma aliyopewa na Rais …

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Mnaoongea nje ya utaratibu mnashangaza sana, kuna sehemu imeandikwa kuwa ukiteuliwa lazima ukubali? Na kuteuliwa na Mh. Rais ndiyo njia ya kufukuzwa huko CWT? Alafu mnajidai eti ni wasomi....kila wakati mnawazatu kukomoa watu siyo ustawi wa jamii kwa faida ya wengi.
 
Una Masters sawa, hiyo ni certificate tu. Je umeelimika? Ukiwa umeelimika huwezi kusoteshwa na mtu. Jitafakari!
chuo gani kwa unavyofikilia kinawezatoa masters hujaelimika?? Hivi unafikiri masters ni kitu chepesiee??
 
Ufafanuzi tafadhali maana wengine hatuelewi kwenye hizo kada za ualimu madaraja yake yapoje, labda kwa kifupi inakuwaje maana barua inaonesha ni mwandamizi daraja A, si wengine tukiona mwandamizi ndio tunajua mbobezi

Labda tugusie kidogo madaraja ya ualimu yapoje walau kwa ufupi tu, utatusaidia wengi humu

Mwalimu mwenye degree ni mwalimu daraja C
Atakuwa daraja 1C,2C, 3C nk kutegemea na muda wa utumishi wake

Mwalimu mwenye diploma ni mwalimu daraja B
Atakuwa daraja 1B,2B, 3B nk kutegemea na muda wa utumishi wake

Mwalimu mwenye cheti (grade A)ni mwalimu daraja A
Atakuwa daraja 1A,2A, 3A nk kutegemea na muda wa utumishi wake
 
Back
Top Bottom