DOKEZO Kashfa kubwa kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Kanisa latumika kuwauzia mashamba hewa waumini wake. Ekari feki 15,000 ziliuzwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Mashariki na Pwani limeingia kwenye kashfa kubwa ya utapeli baada ya makanisa yake ya Kijitonyama, Salasala, Mwenge, Ubungo na Mbezi Beach kuwauzià waumini wake mashamba feki yaliyopo Bagamoyo.
Huko Bagamoyo zamani ilikuwa Mwenyekiti wa kijiji fake, mihuri fake, balozi fake, makaratasi fake wajumbe fake, kumbe haikuishia hapo hata makanisa nayo yamenasa kwenye mtego wa fake, yameacha kazi zake za msingi yanajiingiza kutafuta fedha haramu
 
Kanisani Naamini Angepata Ufafanuzi
Kanisa linasema halihusiki, lakini kanisa ndilo lilitafuta mashamba, ndilo lilikuwa ninayauza, na malipo yalikuwa yanaingia kwenye account ya kanisa. Risiti ambazo watu wamelipa kupitia benki zipo.
 
Kwa hiyo hizo sharika tano za Dar ndio zinakufanya uipakazie Dayosisi nzima ya Mashariki na Pwani? It's not fair.
 
Mada ingeeleweka bila kuingiza lugha za mtaani sijui utapeli mara feki
 
Daah.
 
Heka? Heka ni kitu gani jamani tena? Dah! Tunayo kazi kubwa kwenye lugha zetu hizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…