Mzee Nyani,
Lovely, hao jamaa wa US ilikuwa ni uadui wa kisiasa, je huoni waziri wa ccm kumuandikia mume wa mbunge wetu barua kwa Spika kuwa ni uadui kama huo wa US?
Huyo waziri au naibu waziri kuandika barua kwa niaba ya mume mtu kwa spika, kama ni kweli, ni ujinga na upumbavu. Kama ni kweli na kama aliiandika hiyo barua kama waziri au naibu waziri na sio kama mtu binafsi afukuzwe kazi mara moja au ajiuzulu maana hajui alifanyalo na hiyo ni ushahidi tosha kazi imemshinda
Hivi huoni kuwa hii ishu ikiendelea kujadiliwa tutaishia kuvua samaki kibao katika viongozi wetu ambao nao pia ni washiriki wa uzinzi wa wake za watu?
Mzee Es, kwa mtaji huu nani atabaki sio muovu? Uzinzi upo na utaendelea kuwepo, na kwa vile mtu ni kiongozi haina maana yeye ni timilifu. Wote tuna kasoro. Sasa tunapoanza kusema kwa vile fulani ni kiongozi ooh basi ni lazima timilifu tutakuwa hatutendi haki. Hivi humu foramuni hatuna WAZINZI?
Hiii ishu mzee wangu ukiiiangalai kwa mbali unaweza ukaiona kuwa ni upuuuzi, lakini ninakuhakikishia kuwa huuu ni mwiba mkali unaoweza kuwachoma viongozi wetu wengi tu, maana in the big picture tutagundua mambo mengi sana, kwa mfano je waziri aliyemuandikia barua mume wa mbunge kwa Spika naye hana haya matatizo? je ni kitu gani kilichom-motivate mpaka kumuandikia barua huyu mume wa mbunge na pia kumuonyesha video ya mkewe akiwa in a compromise state? wazirir huyu anayetajwa anashukiwa kuhusika na kutaka kumuweka mtu wake kwenye uchaguzi wa UVccm je ni kweli? Kama ni kweli anataka nini?
I mean I can go on and on, my point ni kwamba hiii ni very interesting ishu kwa taifa na ni muhimu tukaijadili ipasavyo, I understand your concern na heshima ya forum, lakini ninaamini kabisa kuwa ndani ya hii ishu kuna ishu muhimu sana kwetu wananchi kujua tunaongozwa na viongozi wa aina gani, especially katika kipindi hiki ambacho tunaaanza kufikia hatua ya kutumia hela za walipa kodi, yaani wananchi kwa ajili ya kununulia madawa ya ukimwi,
Hakuna ubishi kuwa habari hii inavutia lakini with all due respect sir, sikubaliani na wewe kwamba ni habari muhimu kwa taifa inayostahili kujadiliwa 'ipasavyo'. Labda ungeniambia ni habari ambayo inatawala kwenye mazungumzo ya kwenye vibanda vya kunywea kahawa na kwenye saluni za kutengeneza nywele ningekubaliana na wewe. Tayari tunajua viongozi wanaotuongoza ni binadamu kama sisi, mimi na wewe na wenye kasoro kama sisi sote na sio watakatifu. Sasa kuijadili hii habari kutatufanya tuwajue kivipi ambapo hatuwajui sasa?!?!?
Mzee Nyani, hivi unajua kuwa taifa letu so far limeshatumia hela ngapi za walipa kodi yaani sisi wananchi kuwasafirisha viongozi wetu wa taifa ambao ni wagonjwa wa ukimwi kutibiwa nje? Sio siri kwa mfano viongozi kama Nyanda aliyekuwa waziri na Mungu amuweke mahali pema peponi kuwa alitutoka kutokana na huo ugonjwa ambao chanzo chake ni hiii ishu ya wabunge kuhusiana kimapenzi wakiwa kazini, na taifa lilimgharamia sana kujaribu kumtibu, aliyekuwa RC Kasapila, Mzee wa kazi Marehemu Kinyondo, I mean tunahitaji kuamuka wananchi na huuu ugonjwa, sasa kama viongozi wetu ambao ndio hasa tunawategemea kuhimiza wananchi kuacha huuu ujinga, ndio kwanza wanamalizana huko bungeni je wananchi itakuwaje?
Mimi nadhani ni wajibu wetu sisi sote kama wananchi kuwa waangalifu hasa na hili gonjwa la ukimwi kwani linatumaliza. Lakini kwa wakati huo huo, haina maana eti kwa vile tu wanaotuhumiwa kulana uroda ni wabunge ndio imekuwa nongwa na ni sababu ya sisi kuamka. Kama kuamka inabidi tuamke kutoka kwenye usingizi mzito wa kutawaliwa na viongozi walafi, wezi wa mali zetu (umma), wasioweza kazi, na wasiojali. Ingekuwa watuhumiwa wametumia vibaya nyadhifa zao, kwa mfano kulana uroda ndani ya ofisi ya bunge au kutumia hela za miradi ya maendeleo kwenda ma -shoping na kadhalika, hapo ningesema kweli wamekiuka maadili ya uongozi na ya nafasi zao za kazi na ni jambo linalostahili kujadiliwa kwa mapana na marefu. Lakini eti mtu anatuhumiwa kulala na mke wa mtu eti ni muhimu kwa taifa, mmhhhh.....
Waache wananchi wajadili mzee, kuna elimu kubwa ya bure hapa kwenye hii ishu!