Mlalahoi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2006
- 2,182
- 885
na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zubeir Zitto (CHADEMA) amesema anajiandaa vilivyo kukabiliana kisheria na wimbi la tuhuma zinazoelekezwa kwake zikimhusisha kuwa na uhusiano usiofaa na mbunge mwenzake, Amina Chifupa Mpakanjia (CCM).
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jimboni kwake Kigoma jana, Zitto alisema amesikitishwa kwa kiwango kikubwa na namna vyombo kadhaa vya habari vilivyofikia hatua ya kuandika habari hiyo kwa namna inayoingilia uhuru wake binafsi.
"Nimekuwa mpiganaji siku zote. Ninakuhakikishia nitapambana kutetea haki yangu na nitashinda. Nimeshaanza kujiandaa kuchukua mkondo wa sheria dhidi ya wale wote ambao wamefikia hatua ya kuingilia uhuru wangu binafsi kwa kiwango ambacho hakiwezi kuvimilika tena," alisema Zitto katika hali ya kujiamini kabisa.
Akitoa mfano, mbunge huyo machachari aliyeingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005 alisema ameshtushwa kubaini kuwapo kwa masuala yanayoingizwa katika tuhuma dhidi yake ambayo hayana ukweli hata kidogo.
Mbunge huyo aliliambia gazeti hili kwamba, tayari ameshawasiliana na wakili wake, aliyeko jijini Dar es Salaam ili aanze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya vyombo vya habari na wale wote watakaoamua kuingilia uhuru wake katika hali ya kuvuka mipaka.
"Mimi si mtu wa kuacha privacy yangu ikaingiliwa kwa kiwango hicho. Nitapambana na nitashinda. Nimeshawasiliana na wakili wangu ili aanze kulifanyia kazi suala hilo," alisema Zitto.
Mbunge huyo anatoa kauli hiyo baada ya gazeti moja kuahidi kuchapisha ujumbe wa maandishi wa kupitia katika simu ya mkononi unaoonyesha kuwapo kwa mawasiliano yasiyofaa kati yake na Amina Chifupa ambaye sasa ametalikiwa na mumewe.
Aidha, kauli hiyo ya Zitto inakuja siku mbili tu baada ya yeye mwenyewe kulihakikishia gazeti hili kwamba, uhusiano wake na Chifupa umekuwa ni wa kikazi tu na si zaidi ya hapo.
Taarifa nyingine ambazo gazeti hili lilizipata jana zinaeleza kuwa, miongoni mwa masuala yaliyomshtua Zitto ni kuhusishwa kwake na ujumbe mmoja wa maandishi wa kupitia katika simu ya mkononi (SMS) anaodaiwa kuutuma kwa Amina Chifupa.
"Zitto ameshtushwa na ujumbe huo wa SMS anaodaiwa kuwa aliutuma kwa Amina Chifupa ambao mbali ya kuukana ameshaweka bayana kwamba una maneno ambayo si ya mtu wa aina yake," kilisema chanzo chetu cha habari ambacho kiko karibu na Zitto.
Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, Zitto mwenyewe alipatwa na mshtuko mkubwa alipoonyeshwa ujumbe huo ambao hakumbuki kuwahi kuutuma kwa Amina.
Kwa mara ya kwanza suala hili linalomhusisha Zitto na Amina Chifupa liliandikwa na gazeti moja la kila siku Jumapili iliyopita, ingawa jina la mbunge huyo wa CHADEMA halikutajwa.
Hata hivyo, siku hiyo ya Jumapili, Tanzania Daima ilifanikiwa kuiona barua ya Mohammed Mpakanjia, aliyekuwa mume wa Chifupa aliyoiandika kwenda kwa Spika akilalamika kuhusu kuwapo kwa uhusiano usiofaa kati ya mkewe na mbunge huyo wa CHADEMA.
Tanzania Daima ilipowasiliana na wabunge wote hao wawili kwa nyakati tofauti, walikanusha kuwapo kwa uhusiano huo kati yao na Amina akafikia hatua ya kuhusisha kuachwa kwake na mumewe na ushawishi wa kiongozi mmoja wa juu wa CCM ambaye pia ni Naibu Waziri katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Kutokana na jambo hilo kufikishwa katika vyombo vya habari, Amina Chifupa aliahidi kuitisha mkutano wa waandishi wa habari juzi Jumatatu ambao angetumia kukata mzizi wa fitina kwa kumtaja kiongozi huyo wa CCM ambaye inadaiwa anafanya hivyo ili kumzuia yeye (Chifupa) kugombea nafasi ya uenyekiti wa taifa wa Vijana wa CCM (UV-CCM).
Hata hivyo katika hali isiyotarajiwa, Amina Chifupa (26) alishindwa kutimiza ahadi yake hiyo na badala yake akatokea baba yake mzazi aliyewaeleza waandishi wa habari kuwa, familia ilikuwa imeamua kumzuia mwanawe kuzungumza hadharani masuala yake.
Mzee Chifupa alisema walifikia uamuzi huo wa kumzuia binti yake kuzungumza na waandishi wa habari baada ya kubaini kuwa, masuala yake yangeweza kumalizwa ama ndani ya familia au katika vikao rasmi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Nimekuja hapa kwa niaba ya Mheshimiwa Amina, kuwaomba radhi kwamba familia imesitisha mkutano na waandishi wa habari… ni kweli amepewa talaka moja.
"Sisi ndio wenye jukumu na mtoto wetu. Watoto ni pensheni zetu sisi wazee, hatutaki kuharibu. Tutashughulikia kichama. Kulinda pensheni ni muhimu," alisema mzee Chifupa mbele ya umati mkubwa wa wanahabari.
Pia alisema iwapo Amina anahitaji kuzungumzia suala hilo, atapaswa kufanya hivyo ndani ya vikao vya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na si kuzungumza mbele ya umma.
Tanzania Daima