Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 134
Mumewe Amina hoi!
2007-05-09 16:44:36
Na Badru Kimwaga, Jijini
Siku chache tu baada ya `kumlima` talaka mkewe kwa tuhuma za kutokuwa muaminifu, katika ndoa, mfanyabiashara maarufu nchini, Bwana Mohammed Mpakanjia almaarufu kama `Meddy` imedaiwa kuwa hivi sasa yuko hoi bin taaban kitandani.
Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu mapema leo asubuhi, mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mkandarasi wa kutengeneza barabara, amesema hivi sasa yu hoi kitandani kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hakuweza kuyafichua.
Meddy ametoa taarifa hizo alipoulizwa juu ya tetesi zilizozagaa mitaani kwamba kumpa kwake talaka mkewe ni kutaka kutikisa kiberiti na kwamba wakati wowote huenda akamrejea mama watoto wake na kuendelea na maisha yao kama kawaida.
Mpakanjia ametengana na mkewe, mbunge wa Viti Maalum-UVCCM, Bi.Amina Chifupa kwa kile kinachodaiwa kuwa bibie huyo alikuwa na mahusiano yasiyo rasmi na mbunge mwenzie toka chama cha upinzani cha CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe.
`Iwe natikisa kiberiti...kibatari...ama vyovyote, siwezi kusema kwa sasa, kwa kuwa nimechoshwa kuzungumza na magazeti, pia hapa nazungumza na wewe nikiwa mgonjwa, hivyo niache nipumzike,` Mpakanjia akasema kwa upole.
Hata hivyo pamoja na kutoweza kusema anaugua kitu gani, mfanyabiashara huyo hivi karibuni kabla ya kumpa talaka mkewe alipata ajali ya kuunguliwa na gari na kujeruhiwa sehemu kadhaa za mwili wake.
Ajali hiyo ilimtokea mjini Morogoro wakati wa akielekea Dodoma kwenye shughuli zake za kikandarasi na kupelekea kulazwa hospitali kabla ya kuruhusiwa baadaye.
`Sisi tumeshawazoea wanapeana talaka na kurudiana, na hata hivi sasa pamoja na Meddy kuonekana yupo `siriasi`, lakini ukweli ni kwamba anatikisa kiberiti na wakati wowote atamrejea mkewe kama siku za nyuma,` chanzo chetu cha habari kilisema.
Chanzo hicho kimesema kuwa, wawili hao wanapendana mno na kuachana kwao si rahisi ukizingatia kuwa wana mtoto wanayempenda na kumuona kama `lulu` AbdulRahman `Rahmanino`.
Mtoa habari huyo amesema si mara ya kwanza kwa Meddy na Amina 'kumwagana' na kisha kurejeana mara panapotokea tatizo baina yao.
`Kwani unadhani ni mara ya kwanza kwa Meddy kumuacha Amina na kuapa kutorudiana naye ni kama mara mbili ameshafanya hivyo na hata hii ya safari hii ni geresha tu na ukweli muda si mrefu watarejeana na kuishi kama zamani,` kikasisitiza.
Ndipo Alasiri lilipoamua kumsaka mfanyabiashara huyo kwa njia ya simu na yeye kusema hawezi kusema kama atamrejea mkewe au la kwa vile anaumwa.
Mpaka sasa hakuna uthibitisho rasmi juu ya tuhuma hizo za mauhusiano yasiyo rasmi na haramu baina ya wabunge hao vijana, ingawa juu ya talaka imethibitishwa hata na baba mzazi wa Amina.
SOURCE: Alasiri