Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Nyani Ngabu,

Umefunga baraza!...huu ndio ukweli na tunapoteza muda na akili zetu kuzama ktk maswala yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Isitoshe hawa Zitto na Chifupa kweli ni akina nani hasa ktk maisha yetu kiasi kwamba tupoteze muda wote kuwajadili.
Kusema kweli tumejiweka ktk fungu la wale waitwao simple minded.
 
Mzee Bob,

Heshima mbele, ishu kama hiii ilifanya bunge la US, kutumia dola $ 75,000,000, yaani US dola millioni 75 kwa ajili ya kumchunguza rais wao Clinton, walianzia na ishu ya Whitewater, baadaye ikaishia kuhusu Clinton na mapenzi ya Monica Lewinsky, ikawa sio tena Whitewater,

The most powerful man on the earth, akaishia kuwa-impeached kwa sababu ya kusema uongo kuhusu kufanya mapenzi na Monica,

sisi ni simple minded sasa hawa watawala wa dunia unawaitaje?

Mzee Nyani,

With all due respect, Zeeee na ac ni wabunge wa taifa letu tukufu la jamhuri, ni viongozi wa taifa letu kwa maneno mengine, wanatakiwa kuwa mfano kwa taifa na hasa vijana na watoto, sasa wanapofikia hatua ya kuhusiana kimapenzi, na huku ac mbinge na mke wa mtu, na hata kufikia hatua ya kuachwa na mume wake wa ndoa kwa sababu ya kushiriki katika mapenzi akiwa kazini, yaani bungeni, sasa hawa wawili tutawaamini vipi katika kusimamia ishu muhimu za taifa letu? Halafu ni mfano gani hapa wa kuigwa na wanachi kutoka kwa hawa wabunge wetu wawili?

Wakati taifa letu sasa hivi linaangamia na gonjwa la ukimwi huoni umuhimu kwa wananchi kujua kama Mheshimiwa Zeee na huyu mbunge ac, walitumia condom, maana siku hizi kuna condom za wanawake na waume pia what kama mmoja wao anao huo ugonjwa? Hivi huoni kwamba hata wewe leo hii ukikutana na huyo mwana mama utakuwa careful maana umepata habari hapa?

Barua imeandikwa rasmi na mume wa mbunge kumuarifu kuwa amemtaliki, kutokana na tuhuma za kufanya mapenzi na mbunge mwingine, tenma barua hiyo ameandikiwa na waziri wa serikali, hivi kweli ni makosa sisi wananchi kulijadili na kutaka kujua kinachoendelea hapa?

Sasa ac anapodai kuwa kuna waziri anayemuonea wivu na ndiye chanzo cha kutolewa hizi habari, kweli wananchi tunakuwa na makosa kutaka kujua huyu waziri ni nani na ana interest gani na hii ishu?

Hapana, wananchi tunayo haki ya kujadili hiii ishu na kuikata to the borne, mbunge wa taifa letu anapopewa talaka kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi huko bungeni, ni wajibu wetu wananchi kujadili yaliyojiri mpaka kufikia taifa kufahamishwa na media yetu, ambayo tunaiamini kuwa inajua inachofanya professionally, kazi yao ni kutuarifu kinachoendelea katika taifa letu, na ni wajibu wetu kujadili regardless of how big, small of the ishu, lakini kujadili hii ishu ni haki yetu wananchi kwa sababu inawahusu viongozi tuliowachagua kuwa viongozi wetu wa taifa!
 
Mzee Bob,

Heshima mbele, ishu kama hiii ilifanya bunge la US, kutumia dola $ 75,000,000, yaani US dola millioni 75 kwa ajili ya kumchunguza rais wao Clinton, walianzia na ishu ya Whitewater, baadaye ikaishia kuhusu Clinton na mapenzi ya Monica Lewinsky, ikawa sio tena Whitewater,

The most powerful man on the earth, akaishia kuwa-impeached kwa sababu ya kusema uongo kuhusu kufanya mapenzi na Monica,

sisi ni simple minded sasa hawa watawala wa dunia unawaitaje?

Mzee Es hapa sasa unaboogie yakhe!!! Hayo ya Klintoni yalikuwa motivated na uadui au ushindani wa kisiasa. Asilimia kubwa ya Wamarekani hawakuona mantiki ya yeye kuchunguzwa kwa sababu eti alilambwa koni na Monica. Ndio alidanganya danganya hata kwenye kiapo (?) lakini motive ilikuwa ni kumuangusha kisiasa. Wewe umeona wapi hata wale waliokuwa mstari wa mbele kum-impeach....Newt Gingrich (R-Ga, Speaker at the time) na Bob Livingstone, (R- La) nao kumbe walikuwa ni wazinifu tena wakati huo huo wa skandali. Huo kama sio unafiki ni nini?

Halafu, hii ya kusema...oooh mbona wao walifanya sembuse sisi is lame man. Mambo mengine si ya kuiga ndugu yangu hata kama tajiri au mkubwa anafanya. Huwezi kuhalalisha ujinga, upumbavu n.k eti kwa vile tu fulani naye yuko hivyo.
 
Nyani Ngabu,

Umefunga baraza!...huu ndio ukweli na tunapoteza muda na akili zetu kuzama ktk maswala yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Isitoshe hawa Zitto na Chifupa kweli ni akina nani hasa ktk maisha yetu kiasi kwamba tupoteze muda wote kuwajadili.
Kusema kweli tumejiweka ktk fungu la wale waitwao simple minded.

Ningependa kuamini hivyo!

Na kama ndivyo, ninategemea kiongozi anayeniwakilisha awe na wasifu unaotofautiana na vitendo vilivyowakilishwa na mfano huu.

Hii ni sababu inayotosheleza kabisa kuwepo kwa mjadala huu.
 
Wanabodi
Kwa wanaotaka nichangie issue ya AC na Zitto sitafanya hivyo kwa sasa, kwangu mimi haina maana yoyote. Nikifanya hivyo nitakuwa nimejiingiza kwenye kundi la EN ambaye badala ya kufanya kazi anachunguza wakina anani wanamahusiano wa kimapenzi. Ni upuuzi mtu. Hata huyu EN itabidi nimuache kidogo mafaili yake bado nimeyatunza. Tutaonana mungu akipenda. Mugongo Mugongo come back bro. ukumbi ni wako. Mkandara habari za bongo mzee siamini ulienda baa kunywa fanta.
 
Mzee Nyani,

Lovely, hao jamaa wa US ilikuwa ni uadui wa kisiasa, je huoni waziri wa ccm kumuandikia mume wa mbunge wetu barua kwa Spika kuwa ni uadui kama huo wa US?

Hivi huoni kuwa hii ishu ikiendelea kujadiliwa tutaishia kuvua samaki kibao katika viongozi wetu ambao nao pia ni washiriki wa uzinzi wa wake za watu?

Hiii ishu mzee wangu ukiiiangalai kwa mbali unaweza ukaiona kuwa ni upuuuzi, lakini ninakuhakikishia kuwa huuu ni mwiba mkali unaoweza kuwachoma viongozi wetu wengi tu, maana in the big picture tutagundua mambo mengi sana, kwa mfano je waziri aliyemuandikia barua mume wa mbunge kwa Spika naye hana haya matatizo? je ni kitu gani kilichom-motivate mpaka kumuandikia barua huyu mume wa mbunge na pia kumuonyesha video ya mkewe akiwa in a compromise state? wazirir huyu anayetajwa anashukiwa kuhusika na kutaka kumuweka mtu wake kwenye uchaguzi wa UVccm je ni kweli? Kama ni kweli anataka nini?

I mean I can go on and on, my point ni kwamba hiii ni very interesting ishu kwa taifa na ni muhimu tukaijadili ipasavyo, I understand your concern na heshima ya forum, lakini ninaamini kabisa kuwa ndani ya hii ishu kuna ishu muhimu sana kwetu wananchi kujua tunaongozwa na viongozi wa aina gani, especially katika kipindi hiki ambacho tunaaanza kufikia hatua ya kutumia hela za walipa kodi, yaani wananchi kwa ajili ya kununulia madawa ya ukimwi,

Mzee Nyani, hivi unajua kuwa taifa letu so far limeshatumia hela ngapi za walipa kodi yaani sisi wananchi kuwasafirisha viongozi wetu wa taifa ambao ni wagonjwa wa ukimwi kutibiwa nje? Sio siri kwa mfano viongozi kama Nyanda aliyekuwa waziri na Mungu amuweke mahali pema peponi kuwa alitutoka kutokana na huo ugonjwa ambao chanzo chake ni hiii ishu ya wabunge kuhusiana kimapenzi wakiwa kazini, na taifa lilimgharamia sana kujaribu kumtibu, aliyekuwa RC Kasapila, Mzee wa kazi Marehemu Kinyondo, I mean tunahitaji kuamuka wananchi na huuu ugonjwa, sasa kama viongozi wetu ambao ndio hasa tunawategemea kuhimiza wananchi kuacha huuu ujinga, ndio kwanza wanamalizana huko bungeni je wananchi itakuwaje?

Waache wananchi wajadili mzee, kuna elimu kubwa ya bure hapa kwenye hii ishu!

Halafu at the end of the day hii ni burudani katika bulogu
 
Na mie ningekuwa na langu la udaku nigeongeza chumvi kwa heading kama "Mbunge wa CHADEMA amruka ukuta mbunge wa CCM",halafu ningeweka na sub-heading "Yasemekana mbunge huyo wa CCM anapendelea sana kurukwa ukuta"

Mie ningesema " PENZI KITOVU CHA UZEMBE ZITTO KABWE ASAHAU YALIYOMPELEKA BUNGENI".

Nungwi.

Pole sana hujui kuwa Mwanakjj lolote la Chadema atalipamba kwa kila rangi? nimesikiliza kipindi chake anasema ni watoto hawa tuwasamehe. swali jee kama ni watoto bungeni wamekwenda kufanya nini? kucheza kombolela? au ukuti? huyu bwana kamshupalia Mpenda Kassim kwa kuwapa onyo gazeti lao kwa kutokufuata kanuni za kiandishi. maana siku hizi kila mtu mwandishi hata kama hajui kanuni za kiandishi lakini hili la Zitto kabwe anasema ni tetesi basi na onyo la Mpenda ni tetesi tupe evidence.

ZITTO Kabwe.

Nakushangaa sana kwani hujui kuwa Tambaza secondary school walimfukuza Chifupa? wewe mtu na akili yako unakwenda kuchukua mke wa mtu na bosi wako phillimon mikael anasema poa tu ngoma imejileta yenyewe. ukiletewa mali ya wizi utanunua? wake zetu wakija kwenye surgery yako na kukupa shida zao utawahudumia bila kutaka uroda?

wewe kukaa kimya haitoshi kaombe radhi kwa Medi Mpanjia. zinginevyo umemdhulumu na una dhima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. huko Dodoma kuna vyangudoa wengi wanakuja bungeni hukuwaona hao hadi mke wa mtu?

wanabodi.

Huyu bwana hakuna anayemsingizia kwanini asisingiziwe DR.Slaa? na wabunge wengine? jee wale wapemba wa Cuf walioa wasomali nao walipakaziwa na kampeni za Uvccm?
humu JF tunajadili baadhi ya watu tu? kina ZITTO kabwe tuwaache sababu ni watoto.
 
Vipi phd ya Nchimbi na masters yake kuna mwenye faili? au ndio Savimbi wa CCM na kolimba alimkolimba yeye? kama kuna faili zitolewa sasa huko mbele huyu (SAVIMBI) atatusumbua sana.
 
Ndugu wana Jambo Forums!
Naomba kuwakumbusha regulations za JF!
Ni marufuku kutumia Matusi katika kujenga hoja!

Natumaini tutashirikiana!
Thanks!
 
Mzee Nyani,

Lovely, hao jamaa wa US ilikuwa ni uadui wa kisiasa, je huoni waziri wa ccm kumuandikia mume wa mbunge wetu barua kwa Spika kuwa ni uadui kama huo wa US?

Huyo waziri au naibu waziri kuandika barua kwa niaba ya mume mtu kwa spika, kama ni kweli, ni ujinga na upumbavu. Kama ni kweli na kama aliiandika hiyo barua kama waziri au naibu waziri na sio kama mtu binafsi afukuzwe kazi mara moja au ajiuzulu maana hajui alifanyalo na hiyo ni ushahidi tosha kazi imemshinda

Hivi huoni kuwa hii ishu ikiendelea kujadiliwa tutaishia kuvua samaki kibao katika viongozi wetu ambao nao pia ni washiriki wa uzinzi wa wake za watu?

Mzee Es, kwa mtaji huu nani atabaki sio muovu? Uzinzi upo na utaendelea kuwepo, na kwa vile mtu ni kiongozi haina maana yeye ni timilifu. Wote tuna kasoro. Sasa tunapoanza kusema kwa vile fulani ni kiongozi ooh basi ni lazima timilifu tutakuwa hatutendi haki. Hivi humu foramuni hatuna WAZINZI?

Hiii ishu mzee wangu ukiiiangalai kwa mbali unaweza ukaiona kuwa ni upuuuzi, lakini ninakuhakikishia kuwa huuu ni mwiba mkali unaoweza kuwachoma viongozi wetu wengi tu, maana in the big picture tutagundua mambo mengi sana, kwa mfano je waziri aliyemuandikia barua mume wa mbunge kwa Spika naye hana haya matatizo? je ni kitu gani kilichom-motivate mpaka kumuandikia barua huyu mume wa mbunge na pia kumuonyesha video ya mkewe akiwa in a compromise state? wazirir huyu anayetajwa anashukiwa kuhusika na kutaka kumuweka mtu wake kwenye uchaguzi wa UVccm je ni kweli? Kama ni kweli anataka nini?

I mean I can go on and on, my point ni kwamba hiii ni very interesting ishu kwa taifa na ni muhimu tukaijadili ipasavyo, I understand your concern na heshima ya forum, lakini ninaamini kabisa kuwa ndani ya hii ishu kuna ishu muhimu sana kwetu wananchi kujua tunaongozwa na viongozi wa aina gani, especially katika kipindi hiki ambacho tunaaanza kufikia hatua ya kutumia hela za walipa kodi, yaani wananchi kwa ajili ya kununulia madawa ya ukimwi,

Hakuna ubishi kuwa habari hii inavutia lakini with all due respect sir, sikubaliani na wewe kwamba ni habari muhimu kwa taifa inayostahili kujadiliwa 'ipasavyo'. Labda ungeniambia ni habari ambayo inatawala kwenye mazungumzo ya kwenye vibanda vya kunywea kahawa na kwenye saluni za kutengeneza nywele ningekubaliana na wewe. Tayari tunajua viongozi wanaotuongoza ni binadamu kama sisi, mimi na wewe na wenye kasoro kama sisi sote na sio watakatifu. Sasa kuijadili hii habari kutatufanya tuwajue kivipi ambapo hatuwajui sasa?!?!?

Mzee Nyani, hivi unajua kuwa taifa letu so far limeshatumia hela ngapi za walipa kodi yaani sisi wananchi kuwasafirisha viongozi wetu wa taifa ambao ni wagonjwa wa ukimwi kutibiwa nje? Sio siri kwa mfano viongozi kama Nyanda aliyekuwa waziri na Mungu amuweke mahali pema peponi kuwa alitutoka kutokana na huo ugonjwa ambao chanzo chake ni hiii ishu ya wabunge kuhusiana kimapenzi wakiwa kazini, na taifa lilimgharamia sana kujaribu kumtibu, aliyekuwa RC Kasapila, Mzee wa kazi Marehemu Kinyondo, I mean tunahitaji kuamuka wananchi na huuu ugonjwa, sasa kama viongozi wetu ambao ndio hasa tunawategemea kuhimiza wananchi kuacha huuu ujinga, ndio kwanza wanamalizana huko bungeni je wananchi itakuwaje?

Mimi nadhani ni wajibu wetu sisi sote kama wananchi kuwa waangalifu hasa na hili gonjwa la ukimwi kwani linatumaliza. Lakini kwa wakati huo huo, haina maana eti kwa vile tu wanaotuhumiwa kulana uroda ni wabunge ndio imekuwa nongwa na ni sababu ya sisi kuamka. Kama kuamka inabidi tuamke kutoka kwenye usingizi mzito wa kutawaliwa na viongozi walafi, wezi wa mali zetu (umma), wasioweza kazi, na wasiojali. Ingekuwa watuhumiwa wametumia vibaya nyadhifa zao, kwa mfano kulana uroda ndani ya ofisi ya bunge au kutumia hela za miradi ya maendeleo kwenda ma -shoping na kadhalika, hapo ningesema kweli wamekiuka maadili ya uongozi na ya nafasi zao za kazi na ni jambo linalostahili kujadiliwa kwa mapana na marefu. Lakini eti mtu anatuhumiwa kulala na mke wa mtu eti ni muhimu kwa taifa, mmhhhh.....

Waache wananchi wajadili mzee, kuna elimu kubwa ya bure hapa kwenye hii ishu!

Maoni yangu kwenye rangi nyekundu
 
Nyani umesema maneno mazito... na ukweli unabakia kama wanachodaiwa kufanya vijana hawa ni kweli, hilo ni kosa lao na nafsi zao! Sisi kama jamii tusilifanye kana kwamba ndio kosa kubwa zaidi mwanasiasa anaweza kufanya. NI kosa la aibu n.k lakini halilingani na uzito ambao baadhi ya watu wanataka kuuleta. Tuwaache washughulikie, kwanini kuna mtu hapa ana ubia na ndoa ya Medi na Chifupa? au ana ubia na maisha ya Zitto? Kama wameboronga bila ya shaka wameboronga, na hilo liwe funzo kwa wingine, hakikisha huachi ushahidi!!
 
Mzee Nyani,

Heshima mbele na strong points, lakini huyu waziri atafukuzwaje kama wananchi hatukuonyesha outrage yetu kwa kujadili hii ishu ipasavyo?

Halafu tutajuaje kuwa kuna wakati hao wabunge wawili waliwahi kufanya mapenzi ndani ya ofisi za bunge letu tukufu?

Kama haya mawili kwako ndio muhimu katika hiii deal nzima, basi lazima kufanyike majadiliano ya taifa baina ya wananchi ili kupata ukweli!

Mzee MMJ,

Ukweli ni kwamba tunajaribu kumpa some kind of heshima Mheshimiwa Zito so far, hasa kwa kuheshiku kuwa ni mjumbe wa hapa forum, na ni kiongozi kijana mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, na kwamba umri wake unampa nafasi ya ku-turn the ishu arround,

ila unazi wako utafikia mahali utatuondoa heshima yetu kwa mbunge na hii ishu, then tutatwanga mawe kweli!
 
Masikini Nchimbi a.k.a mpambanaji!

Lazima ajue kuwa kuna kitu kinaitwa MORAL AUTHORITY especially when you are dealing with issues like these. Alichokifanya ni kutumia nyuklia kufanya kile anachodhani ni pre-emptive strike hajui kuwa silaha za Nyuklia ni deterance power ambayo ukitumia uwe tayari kwa possible selfdestruction (samahani kwa kizungu kingi).
Nakumbuka wakati wa mbio za Chimwaga JK alipokuwa anajaribu kuwasihi waache kuwatukana kina Mzee Malechela na Dr Salim matusi ya nguoni yaliyomfanya Mzee Malechela kupoteza umakini, walimwambia akae kimya na awaachie wao hiyo kazi kwani walijua kuwa kwao wao urais wa JK ndio salama yao.
Alichokifanya ndugu yangu Nchimbi aka Mpambanaji ni kuonyesha jinsi gani alivyo liability kwa wenye nchi kama aonekanavyo Amina Chifupa. Ni wazi moto aliowasha utapelekea ya kuwaunguza zaidi kaka zake katika mtandao na zaidi yeye binafsi. Kwa CCM ambayo ufuska ni hali ya kawaida isipokuwa habari kufika katika vyombo vya habari ndio dhambi kuu, Nchimbi tayari ni liability kwa mustakabali wa wengi ndani ya chama na chama chenyewe.
Anyway, sishangai sana kuona anatumia mbinu hizo kwani ameyafanya mengi ya kutisha kuliko hayo na anajua zaidi ya siasa chafu hana uwezo wa "kufanikiwa" kisiasa. Zaidi ya yote hii inaonyesha jinsi gani asivyo na uwezo wa kudhibiti umoja wa vijana kwani Amina alimshinda kumzuia wakati wa uchaguzi wa ubunge (baada ya kumbeba mwanzoni na kuonywa na wenziwe) na sasa inaonyesha kuwa aligundua kuwa hatoweza kumzuia na kuweka mtu anayedhani kuwa atamwezesha kuburuza umoja wa vijana CCM ambao anaona ndio unaompa umuhimu katika mtandano kwa remote. Sitashangaa kama ni kweli chaguo lake ni mwenyekiti wa vijana wa CCM wa Singida ambaye hata JK na uvumilivu wake wote alishindwa kumbeba ingawa alikuwa akifanya shughuli moja nyeti sana wakati wa mchakato wa urais ndani ya chama.
Ni wazi moto umewaka na ni mwendelezo wa yale yaliyotolewa kuhusu Waziri Magufuli ambaye naye wanamtandao waliamua kutumia gazeti lao la Rai kumtolea siri yake ambayo angalao walikuwa na ushahidi wa kutosha lakini watanzania wakaamua kuchagua utendaji wake zaidi ya mapungufu aliyonayo.

Tanzanianjema
 
Mzee Es u never stop amazing me. Nimekuwa nikifuatilia uchangiaji wako katika hili na umeniprove wrong maana unaonyesha ama umakini wa hali ya juu. Kwa hili nakupa big up kaka

Tanzanianjema
 
Masikini Nchimbi a.k.a mpambanaji!

Lazima ajue kuwa kuna kitu kinaitwa MORAL AUTHORITY especially when you are dealing with issues like these. Usipokuwa na moral authority ukiongela ama kutumia njia kama hizi ni ama watu wakudharau na kukukejeli ama kukugeukia wewe mwenyewe. Alichokifanya ni kutumia nyuklia kufanya kile anachodhani ni pre-emptive strike hajui kuwa silaha za Nyuklia ni deterrence power ambayo ukitumia uwe tayari kwa possible selfdestruction (samahani kwa kizungu kingi).

Nakumbuka wakati wa mbio za Chimwaga JK alipokuwa anajaribu kuwasihi waache kuwatukana kina Mzee Malechela na Dr Salim matusi ya nguoni yaliyomfanya Mzee Malechela kupoteza umakini, walimwambia akae kimya na awaachie wao hiyo kazi kwani walijua kuwa kwao wao urais wa JK ndio salama yao.

Alichokifanya ndugu yangu Nchimbi aka Mpambanaji ni kuonyesha jinsi gani alivyo liability kwa wenye nchi kama aonekanavyo Amina Chifupa. Ni wazi moto aliowasha utapelekea ya kuwaunguza zaidi kaka zake katika mtandao na zaidi yeye binafsi. Kwa CCM ambayo ufuska ni hali ya kawaida isipokuwa habari kufika katika vyombo vya habari ndio dhambi kuu, Nchimbi tayari ni liability kwa mustakabali wa wengi ndani ya chama na chama chenyewe.

Anyway, sishangai sana kuona anatumia mbinu hizo kwani ameyafanya mengi ya kutisha kuliko hayo na anajua zaidi ya siasa chafu hana uwezo wa "kufanikiwa" kisiasa. Zaidi ya yote hii inaonyesha jinsi gani asivyo na uwezo wa kudhibiti umoja wa vijana kwani Amina alimshinda kumzuia wakati wa uchaguzi wa ubunge (baada ya kumbeba mwanzoni na kuonywa na wenziwe) na sasa inaonyesha kuwa aligundua kuwa hatoweza kumzuia na kuweka mtu anayedhani kuwa atamwezesha kuburuza umoja wa vijana CCM ambao anaona ndio unaompa umuhimu katika mtandano. Sitashangaa kama ni kweli chaguo lake ni mwenyekiti wa vijana wa CCM wa Singida ambaye hata JK na uvumilivu wake wote alishindwa kumbeba ingawa alikuwa akifanya shughuli moja nyeti sana wakati wa mchakato wa urais ndani ya chama.

Ni wazi moto umewaka na ni mwendelezo wa yale yaliyotolewa kuhusu Waziri Magufuli ambaye naye wanamtandao waliamua kutumia gazeti lao la Rai kumtolea siri yake ambayo angalao walikuwa na ushahidi wa kutosha lakini watanzania wakaamua kuchagua utendaji wake zaidi ya mapungufu aliyonayo.

Kwa kifupi ni mwendelezo wa safari ya mwisho ya CCM. Mzee Karl Marx alituasa kuhusu mapambano yasiyokwisha katika tabaka tawala kuwa ni dalili tosha za kuanguka kwa tabaka hilo. Safari njema mradi mjitahidi kutuachia Tanzania yetu ikiwa nzima na si vipandevipande kama Barre alivyoiacha Somalia.

Tanzanianjema
 
Mzee Nyani,

Heshima mbele na strong points, lakini huyu waziri atafukuzwaje kama wananchi hatukuonyesha outrage yetu kwa kujadili hii ishu ipasavyo?

Halafu tutajuaje kuwa kuna wakati hao wabunge wawili waliwahi kufanya mapenzi ndani ya ofisi za bunge letu tukufu?

Kama haya mawili kwako ndio muhimu katika hiii deal nzima, basi lazima kufanyike majadiliano ya taifa baina ya wananchi ili kupata ukweli!

Mzee MMJ,

Ukweli ni kwamba tunajaribu kumpa some kind of heshima Mheshimiwa Zito so far, hasa kwa kuheshiku kuwa ni mjumbe wa hapa forum, na ni kiongozi kijana mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri, na kwamba umri wake unampa nafasi ya ku-turn the ishu arround,

ila unazi wako utafikia mahali utatuondoa heshima yetu kwa mbunge na hii ishu, then tutatwanga mawe kweli!

Yakhe, kujibu swali lako la kwanza, rudia tena kusoma rebuttal yangu kuhusu huyo waziri (naibu waziri?). Nimetumia neno kama (or if in English - to express an uncertainty/ cautious opinion) kuonyesha kuwa sina uhakika na yanayosemwa kuwa ni kweli. Kama ni kweli, je, aliiandika hiyo barua kama mtu binafsi au kama waziri (naibu waziri) kwa kutumia karatasi yenye anwani na jina la wizara yake (letter head)? Kama la kwanza ndio kweli basi mimi sina tatizo. Kama la pili ndio kweli hapo ndio nitakuwa na tatizo naye na nitakuwa bega kwa bega na wewe kuwa 'outraged'.

Swali lako la pili - hapa mazee nilikuwa nazungumzia nadharia ya tukio (hypothetical scenario) tu. Kama hiyo ndio ingekuwa issue, basi jambo hili lingekuwa ni la muhimu kulijadili kwa maslahi ya taifa kwa sababu hawa watuhumiwa wangekuwa wameligeuza bunge letu kuwa lidanguro fulani hivi. Unanipata mzee?

Mpaka sasa jambo hili mi naona ni la kibinafsi lisilo na umuhimu wowote zaidi ya kutuvutia na kutuburudisha. Zaidi ya hapo it is a non-issue. Na huu ndio mwisho wa mimi kulitolea maoni. Nyie endeleeni.
 
Mlalahoi,

Sijamlazimisha mtu kuchangia mada. Soma vizuri nilichoandika kabla ya kukurupuka.

Mwkjj.

Nakubaliana na wewe kilichoibiwa hakina hiari, lakini ktk hili alieibiwa ni Medi! unless uniambie ilikuwa "hiari" yake Medi kuwa Zitto ajilie.

Well somebody must take the lead, who is that in this saga? We need Zitto to come open.

Kama ni mtego Zitto kishauvaa cha kufanya ni kujinanusua, kula "tunda" Ujiji huko haimsaidii.

Ningekurupuka ningekupa salamu ya heshima?Nimekujibu vizuri baada ya kukusoma vizuri.Kutoafikiana kwenye hoja hakumaanishi flani amekurupuka.
 
Binafsi nashangazwa na watu wasiopendezwa kuona hii ishu inaendelea kujadiliwa.Wapo wanaofikia hatua ya kutuita "mibaba mizima tunaopoteza muda kwenye kompyuta zetu kujadili so and so..."Hivi mmelazimishwa kusoma kinachoandikwa na wengine?Kwani mada iko moja tu mpaka muishikie bango hii pekee?Acheni watu tukate ishu,kama kuna mtu anakereka na aanze kwa mbele.
Kuna kijitabia kinachokera ambacho baadhi ya waungwana flani wanajiona wana mamlaka ya ku-dictate nini tujadili na nini tusijadili.Hili sio gazeti la Uhuru au Mzalendo ambapo siku zote ni sifa kwa CCM na viongozi wake.Forum ni ukumbi wa kutoa mawazo.Niliwahi kumshauri mwanabodi mmoja huko nyuma kwamba once akikuta mada ambayo hadhani inastahili kuchangiwa the way it does then anaweza kufanya moja kati ya yafuatayo
1.Kuchangia
2.Kuisoma na kisha kukaa kimya
3.Kuipuuza

Ifahamike kuwa pongezi kwa mtu mmoja inaweza kuwa tusi kwa mwingine,and vice versa.Mada inayoonekana ni ya kipuuzi kwa mtu flani inaweza kuwa hot kwa mwingine.Kwanini msi-censor mawazo yenu ya kizembe kabla ya kufikiria kuleta censorship kwenye mawazo ya wengine?
 
[
Mpaka sasa jambo hili mi naona ni la kibinafsi lisilo na umuhimu wowote zaidi ya kutuvutia na kutuburudisha. Zaidi ya hapo it is a non-issue. Na huu ndio mwisho wa mimi kulitolea maoni. Nyie endeleeni.[/quote]

Mimi naona hili swala sio la kibinafsi kama Nyani anavyodai. Tupende tusipende wahusika ni public figures na ni viongozi wa wananchi. Viongozi kama hawa ni kiyoo cha jamii na ni wawakilishi wawatu. Tendo lolote linalofanywa na viongozi au mtu mwenye influence kwa jamii lina impact. Nakmbuka Zumma alipotoa stetment yake kuwa alinawa baada ya kufanya ngono na mwenye virusi vya ukimwi watu na wanaharakati wengi walipiga kelele kwani walijua madhara yake kwa wanajamii. Hivyohivyo kwa viongozi kama akina Zitto wanaweza wakawa na influence kwa jamii issue tuu sio uzinzi lakini pia wahusika wanauzito tofauti na mtu wakawaida. Kila mtu anajua Ukimwi ni janga la kitaifa, tunategemea kuona viongozi wanakuwa mfano hata kama ni swala la upimaji wawe mbele kupima na wawe ndio mabalozi wa kupiga vita ukimwi. Taifa linateketea sasa viongozi wetu hawa kama wanakuwa hivi hata mabint zetu huko mashuleni na wake zetu si watawamaliza? Tutake tusitake lililofanyika ni Kosa na kama ni kweli limefanyika, Basi wahusika wameliaibisha bunge na taifa kwa ujumla. Anyway tunamambo mengi ya kujadili kuhusu maendeleo ya taifa letu lakini hata hili nalo linahusu maendeleo ya taifa letu kwanamna moja au nyingine. Najua kuna watu hapa hawataki kusikia hii mada tena inajadiliwa lakini kila mtu yupo free kuijadili au kuacha kuijadila au hata kutoisoma kabisa.
 
Kwa muda nimefuatilia mada hii na huu ni wakati muafaka kutoa mchango wango, Big Up Mzee Es, MKJJ na wengine kwa kuonyesha ukomavu wa kufikiri, na kwenda mbali zaidi ya ishu ya ngono[tuhuma] kati ya ac na Zeeee

hii ishu ni muhimu iendelee kujadiliwa kwani kuna mafunzo yanapatikana ndani yake.

Maadili kuna Kipindi mama teri aliwahi kupiga kelele kuhusu maadili ya hawa waheshimiwa, bila subira aliitwa mbele ya kamati ya bunge, si shaka amekwisha hukumiwa kwani siku hizi hasikiki kabisa, tukijadili kwa nguvu suala hili liaweza kuwa chachu ya maadili kwenye taifa letu.

Siasa chafu kuna uwezekano kuwa tuhuma hizi ni za kutunga [kila kitu kinawezeka kutokna na kukua kwa technologia] zinaweza kupingwa picha na ikatengenezwa clip ya video kutengeza ushaidi, ili kuumalizana kisiasa, suala hili lililamikiwa tokea kampeni za 2005, tuliona jinsi, SAS alivyohusishwa na sultan na picha zake kutolewa kwenye mageti, ili hali ilikuwa ni usanii mtupu

Wana JF tusiwe wavivu wa kufikiri, wakati mwingine ni vyema kufikiri nje ya box, na tuondokane na kasumba ya kufikiri ndani ya box
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom