Zitto: Nimejeruhiwa lakini sijakata tamaa
KASHFA ya ufuska inayowaandama wabunge wawili vijana, Zitto Kabwe wa CHADEMA na Amina Chifupa wa CCM, imebadili kwa kiasi kikubwa mwenendo wa maisha yao, kila mmoja kwa staili yake.
Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, ambaye hivi karibuni alikaririwa na gazeti hili akieleza kuwa atapambana kwa uwezo wake wote kukabiliana na wimbi la tuhuma zinazoelekezwa kwake, zikimhusisha kuwa na uhusiano usiofaa na Amina, sasa anaonekana kukata tamaa.
Katika kile kinachoonekana kuelemewa, Zitto tayari amekwishaanza maandalizi ya kukiacha kiti cha ubunge na amesisitiza kauli yake aliyoitoa mapema mwaka huu akiwa mkoani Shinyanga kuwa hatagombea tena ubunge, ingawa amesema hakusudii kuachana na siasa.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, juzi katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kutohusika na tuhuma hizo, Zitto alisema katika kipindi kifupi cha tuhuma hizo, ameshuhudia mchezo mchafu na wa kusikitisha wa siasa za hapa nyumbani za kuchafuana kwa lengo la kuwania madaraka.
.........Taarifa zisizo rasmi licha ya kutolewa na watu wa karibu na Amina zimeeleza kuwa, kwa siku kadhaa sasa amekuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na amezuiliwa katika chumba maalumu nyumbani kwa wazazi wake.
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/5/20/habari2.php