Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Matokeo yameshajulikana. hakuna Mtanzania ataempigia mtu kura kwa fedha zake, watu fedha watakula na Urais hawampi.

Nani ataekubali kuongozwa na mgonjwa asiyeweza hata kuweka maneno sawa? Labda ni misukule tu.



Ma Boss wako wanaingia uvungu wa kitanda kujificha wakiskia Rais Edward N Lowasa wewe unajitutumua
fox brown
tutaelewana tu October 25 asubuhi 2:30
 
Matokeo yameshajulikana. hakuna Mtanzania ataempigia mtu kura kwa fedha zake, watu fedha watakula na Urais hawampi.

Nani ataekubali kuongozwa na mgonjwa asiyeweza hata kuweka maneno sawa? Labda ni misukule tu.

Wewe ndiye mgonjwa unaetaka kutuaminisha upumbavu wako!! Huo ni wako baki nao mwenyewe, hakuna asiyejua CCM ni magumashi! Kura 8 za familia yangu ni kwa mzee lowasa japokuwa Mimi ni CCM, komeo lenu halipati kura yangu! CCM inafuga majizi wa mali ya umma
 
Ukweli haufichiki kamwe, sasa tumemjua mchawi nani. Na Lowasa kaweka wazi tu, toka andoke mbona mikataba mingi mibovu imesainiwa na hakuna mkubwa kama yeye aliejiuzulu au ni kivuli chake ndo kilisaini? Naamini hapa ni mwanzo tu ngoja angie ikulu tuyajue mengi.

Kuna haja basi ya wengine kutoka hadharani na kueleza uhusika wao. Hata Mwakyembe itambidi aeleze kile alichokificha wakati anasoma ripoti ya uchunguzi. Alimaanisha nini aliposema kama angesema kila kitu nchi ingetikisika.
 
Mimi nawaamini Watanzania wengi watakaopiga kura sio wajinga wa kulipa Jambazi lililobobea kura zao. Ati leo linauliza mwenye ushahidi aende mahakamani, kama ni hivyo kwa nini lilijiuzulu uwaziri mkuu. Hilo ni tosha a) Halina uwezo wa kuaminika b) Limekuwa kuwadi wa majizi menzake c)Litakufa kwa pressure d) Urais haliupati ng'oooooooooooooooooooooooooo
 
.....akatoka nje kuwasiliana kwa saa moja,kisha akarejea na kuniambia "nimewasiliana na mamlaka ya juu,na ameagiza mkataba huu usivunjwe"

POLENI WATANZANIA
kusoma hapa nilipasuka kwa kicheko.. ha ha ha
 
Kama kajibu swali gumu kwa njia rahisi hivyo! basi EL hana utetezi wenye uzito. Hv kwenye nchi nani next to the president? Yeye hawezi kupewa taarifa na mwanasheria, yeye ana uwezo wa kuongea na rais na kuhakikisha. Utetezi dhaifu sana.
 
Ni kweli tuna haki watanzania kulaumu alikuwa wapi kuyasema kama alikuwa akituhurumia watanzania lakini pia tunahaki ya kuhoji kwanini serikali haikuchua hatua ya kumshitaki alipotuhumiwa kama fisadi? Hapo pia akili ya kuambiwa changanya na zako.

Kwan wale waliodaiwa kurudisha pesa za EPA walishtakiwa?
 
Kama hakuhusika alipaswa iulizwa kwa kutosikilizwa kama waziri mkuu, kwa nini alisubiri hadi aambiwe jiulize hayo ndio maamuzi magumu ,,,
 
Wanajukwaa!

Muda umepita sasa tangu Waziri Mkuu aliejiuzulu Mh Edward Lowassa kujitetea kuhusu kashfa ya richmond.

Lowassa alisema bayana hadharani mbele ya waandishi wa habari na umma kwa ujumla akiwa 'live' ITV, kuwa alipokea maelekezo kutoka 'mamlaka za juu yake' kuwa mkataba wa richmond uendelee. Mamlaka ya juu yake maana yake ni bosi wake ambaye ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh, Dr, Prof Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa kuongea vile, Lowassa alijinasua na kashfa hii ya richmond na kumtupia zigo lote aliekuwa bosi wake. Ikumbukwe katiba inamtaka kutii, kutekeleza na kukamilisha maelekezo ya mamlaka ya juu yake. Ikumbukwe hapo kabla Lowassa hajawahi kujitetea hadharani kuhusu kashfa hii ya richmond!

Tujiulize:

1. Ni kwanini mamlaka ya juu yake hayakanushi hii kauli ya Lowassa? Mbona kurugenzi ya habari inayoongozwa na Ndg Salva Rweyemamu imekuwa ipo 'sharp' kukanusha masuala mbalimbali yanayoelekezwa kwa rais kama taasisi hata kama ukanushaji wake ni wa 'ukakasi'?

2. Kuendelea kumuita Lowassa fisadi ni kumtendea haki?, wakati tayari amesema ukweli na kuwekwa wazi?. Tena akaenda mbali kwa kusema yeyote mwenye ushahidi na apeleke mahakamani!

3. Kama hili la ufisadi kwa Lowassa 'si chezo' ni kwanini tume ya Mwakyembe haikumhoji kipindi kile? Kulikuwa na nini?

Ni ukweli gani na ni kwa kiasi gani mtu anatakiwa kusema ili asiendelee kutuhumiwa?!

Simple conclusion:
Kwa muktadha huu wale wanaondelea kumuita Lowassa fisadi badala ya kumuita Jakaya Kikwete fisadi ni wale waliopofuka kifkra! Ikulu yenyewe imekaa kimya kwa utetezi huu, wewe ndo uhangaike kumuita Lowassa fisadi! Umepofuka kifkra!

=====
Nimependa hii hoja ya Zemarcopolo na Jibu alilopewa na great thinker Kublai !

Let's assume kwamba alichosema Lowassa ni kweli.
Maana yake ni kwamba Lowassa alishirikiana na mamlaka kulitia hasara taifa.
Hiyo mamlaka haigombei urais. Anayegombea ni Lowassa.
Mtu aliyeshirikiana na mamlaka kulitia hasara taifa hafai kuwa Rais.
Kwenye Richmond tumemkamata, kuna mangapi kafanya hatujayashtikia.
Kiujumla utetezi alioutoa Lowassa kajimaliza mwenyewe kwa kukiri kuhusika. Mimi nilifikiri atasema hajahusika...

Chama kilichoshirikiana kulitia hasara taifa hakifai kutupatia rais. Lowassa aliwajibika, alijiuzulu hamna adhabu ingene yoyote unayoweza kumpa. Kwa mtazamo wako yeye ana Richmond, CCM na Magufuli wake wana eskrow, meremeta, epa, tangold, iptl, twin tower etc etc etc mlolongo mrefu sana na mengine chungu mbovu ambayo hatujayashtukia. Angalau Lowassa amekiri nyie CCM mmekiri nini? Au hamhusiki vyote hivyo alifanya Lowassa?

 
Sio kwa jambo kama hili, wala si kwa muda kama huu, na wala si kwa kiwango kama hiki! Ikulu wanajua ajaye ni Lowassa, Kikwete ndo anaondoka. Hivyo wanaweka akiba ya maneno! Umenielewa??!!

mnajua kujipa moyo
 
Ikulu haina ubavu wa kumjibu Lowasa maana kufanya hivyo watazidi kuchafua hali ya hewa
 
Back
Top Bottom