Kashfa ya Trilioni 1.5 Bwawa la Nyerere mbona Zitto Kabwe uko kimya kulikoni?

Kashfa ya Trilioni 1.5 Bwawa la Nyerere mbona Zitto Kabwe uko kimya kulikoni?

Nchi hii Ina Shida Sana, speculation za kufa mtu Kila siku na hakuna kinachofanyika.

Kwa uelewa wangu makato ya ucheleweshaji kazi "Liquidated Damage" (LD) yanakatwa pale muda wa mkataba wa kazi unapoisha na asikubaliwe kuongezewa muda zaidi wa kazi wakati mkandarasi hajamaliza na kukabidhi kazi.

LD inayoongelewa na Mpina inaweza kuwa haipo kama aliomba kuongezewa muda na kukubaliwa ambacho inaweza kuwa kweli kwa sababu ya corona kwa kuwa wote tumeona athari zake lakini kama hakupewa nyongeza ya muda Ina maana LD inaweza kukatwa katika certificate zake za mwisho ili kutoathiri utekelezaji wa mradi.

Kwa hiyo Ile zana ya ufisadi huo inayoenea inakuwa imekufa kifo Cha kawaida.
 
BUNGE jana limeibua Kashfa ya upigaji wa zaidi ya trilioni 1.5 kwenye mradi wa bwawa la nyerere lakini tangu jana tuhuma hizo zimeibuliwa bungeni na mbunge wa kisesa, luhaga mpina nilitegemea zito kabwe ungetoa tamko juu ya suala hilo.

Ukimya wa Zitto Kabwe kwenye mambo mazito kama haya yanapotokea nchini kwetu inaleta tafasiri gani kwenye mustakabali wa demokrasia ya nchi yetu au wizi na ufisadi sio ajenda ya wapinzani?

Naomba tujadili hoja hii ya Zitto kujitoa kwenye mambo mazito kama haya.
Huyu mwamba ni bonge la mnafiki. Ukitaka kujua basi gazeti liandike uchafu wa awamu ya 5. Atasema kwa msisitizo sana ila likitamka uozo wa awamu hii ya asali, mdomo na mikono vinatiwa pingu hakuna kuwa movable
 
Zitto maana yake ni baa hiko ujerumani
IMG_0387.jpg
 
Back
Top Bottom