Kashfa za wizi na ufisadi zazidi kumuandama Mbunge Luhaga Mpina

Kashfa za wizi na ufisadi zazidi kumuandama Mbunge Luhaga Mpina

Wamemuundia zengwe hao CCM wenzake na hao wa mama ukiwaangalia wanavyoongea unajua kabisa wamesetiwa
 
Baadhi ya wavuvi waliochomewa nyavu zao wakati Mpina akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wameomba achukuliwe hatua na kuwalipa fidia.

Wakati hilo likiendelea baadhi wametaka CCM isimpe tena nafasi ya kugombea Ubunge mwaka 2025 baada ya kushiriki kupora ardhi zaidi ya hekari elfu moja na kujimilikisha yeye na marafiki zake.

Eneo la ardhi linalotajwa ni la maelfu ya familia masikini katika vijiji vya Dalla na Mbwade mkoani Morogoro.

Chanzo: Cheche Times
Mpina tunajua kati ya wezi waliopo ndani ya ccm wewe ni kasisimizi tuu wezi wakubwa wapo humo chamani na sii wezi wa mali tuu bali hata majambazi ya kupora uchaguzi.
Mpina kaamua kuweka hoja nzito bungeni zenye maslahi mapana dhidi ya wahuni wachache ndani ya serikali ndio wana muundia zengwe.
Kuna msemo unasema ukiona ccm wanakusifia tafuta mahali pa siri ujifiche umlilie sana Mungu akufubulie ni wapi ulipokosea.
Ccm jibuni hoja za Mpina bungeni acheni siasa za maji taka.
Kwa watawala weusi mwekezaji ni mweupe tu kwa kuwa ni rahisi kumtaka rushwa ila kwa mweusi mwenzao ni mwizi hata kama uwekezaji wake una tija mara elfu ya mwarabu au mhindi .
 
Back
Top Bottom