Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Ilikuwa ni mwezi february mwaka 2015 raisi Xi alipotangaza maono yake ya kujenga mji mpya mkubwa nchini China. Michoro na mipango yote ikakamilika mwaka 2017 na miaka sita imepita China wamekuja na mradi mkubwa wa kujenga mji mpya kabisa kutoka ardhini yaani "from scratch".
Mji huo utatiwa Xiongan na umeanza kujengwa kaskazini mwa Beijing ndani ya jimbo la Tianjin-Hebei na wagharimu dola za marekani $580 milioni.
Tayari ndani ya miaka sita miundombinu kama njia za usafiri wa barabara, reli mabasi, magari ya kukodi, uwanja wa ndege, mifumo ya maji na mifumo ya ekolojia tayari imejengwa.
Kituo cha reli cha Xiongan kikiwa tayari kwa matumizi katika jimbo la Hebei.
Mwaka 2020 tayari njia za reli ziitwazo Intercity railways za kutoka mji mkuu wa Beijing kwenda Xiongan zilikuwa zimekamilika na hizi zitawezesha wasafiri kutumia dakika zipatazo 50 tu badala ya saa moja na nusu kutoka Beijing kwenda Xiongan.
Wasafiri wa ndege watatumia dakika 19 tu kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Daxin mjini Beijing kwenda Xiongan.
Kufikia mwaka 2021 njia za barabara zikiwemo zile barabara kuu zenye urefu wa kilomita 500 zilikuwa tayari kwa matumizi. Majimbo mengine madogo yanozunguka Xiongan yote yameboreshwa na njia zote zafanya kazi.
Video ya hapo chini iilichukuliwa mwezi ulopita ikionyesha mji huo mpya kabisa ukiwa umekamilika kwa asilimia 90.
Yasemekana wajenzi na mafundi wanojenga mji huo wamekuwa kazini masaa 24!
Ama kweli akili ukiitumia uzuri haiwezi kukuangusha.