Kasi ya utendaji ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa inatufuta machozi wazalendo

Kasi ya utendaji ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa inatufuta machozi wazalendo

Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai
Hivi anapokea per diem, maana kila siku yuko safarini na anatumia usafiri wetu. Ni Mwalimu tu alikuwa hachukui per diem
 
Hivi anapokea per diem, maana kila siku yuko safarini na anatumia usafiri wetu. Ni Mwalimu tu alikuwa hachukui per diem
Tulia sindano ikuingie
 
Hakika mheshimiwa Majaliwa utendaji kazi wake ni wa kutukuka.
Mungu azidi kumpa afya tele aendelee kusafisha ofisi za umma dhidi ya uzembe na ubadhirifu wa fedha.
 
Amani iwe nanyi.

Kuna kauli mbalimbali ambazo zilitolewa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu Hassan zilizopelekea watanzania kuwa wamoja zaidi na kuifanya nchi kutulia mara baada ya msiba mzito wa kuondokewa na rais Magufuli.

Binafsi ninazo kauli mbili ,kama na wewe unazo weka hapq.
1. Mimi na Magufuli ni kitu kimoja.
Ikumbukwe mara baada ya kufariki rais Magufuli liliibuka kundi likiongozwa na Tundu Lisu na Lema likawa linashangilia kifo hicho, hali hiyo ilienea hadi kwa baadhi ya wabunge kama Nape na Makamba, badala ya kujadili bajeti wakawa wanajadili nani ni zaidi kati ya Magufuli na Samia.!
Hali hiyo iliwakera sana wazalendo wa nchi yetu na rasmi likaibuka kundi jingine lililobatizwa jina la walinda legacy ya Magufuli, moja ya watu wa kundi hili waliojitokeza hadharani kukemea ni mbunge Lusinde ,pia Lazaro Nyalandu aliyekuwa kada wa Chadema alikemea hadharani na kutangaza kuachana na Chadema kwa kitendo chao cha kumtukana alipohudhuria msiba Chato.
Katikati ya mvurugano huo aliibuka rais Samia na kuwachana live Wabunge na Chadema kwa ujumla kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja na serikali yake ya awamu ya sita haijatokana na uchaguzi mbali imetokana yeye Samia kuaminiwa na hayati Magufuli na kufanywa kuwa makamu wa rais.
Kauli hii ya Samia ililifanya kundi la walinda Legacy kuibuka kidedea dhidi ya kundi la washangilia kifo hivyo nchi kutulia.

2. Wala rushwa ,wazembe majambazi na mafisadi kuendelea kubanwa.
Rais Samia alitangaza hadharani kwamba katika masuala ya rushwa atasimama imara na akamtumbua mkurugenzi wa bandari na kuagiza Takukuru wafanye uchunguzi BOT na wizara ya fedha.
Pia kuwajibisha wote waliojaribu kuchezea mifumo ya Tanesco ,TRA na bandari.
Hatua hizi zilifanya nchi kutulia kwa sababu watanzania wengi waliona rasilimali zao bado ziko salama kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya tano chini ya hayati Magufuli.
 
UTENDAJI KAZI: MAJALIWA KASSIM MAJALIWA

Tarehe 10/4/2021 anafanya ziara kukagua ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji na kuwaahidi Watanzania kuwa ujenzi utaendelea kama kawaida na kumalizika kwa muda uliopangwa.

Tarehe 19/4/2021 anakwenda kuukagua mradi wa mabasi ya mwendokasi baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Ufanisi wa mradi huo, anakuta utendaji ni mbovu anamsimamisha kazi mkurugenzi wa fedha wa mradi huo Susana Steven Chaula.

Tarehe 19/4 /2021 anakwenda kukagua bandari ya nchi kavu Ubungo Baada ya magari ya mizigo kukwama kwa zaidi ya siku tatu..anafanya mazungumzo na madereva pamoja na watendaji wa bandari

Tarehe 19/4/2021 anafanya ziara kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichopo Kibaha, Pwani. Anawahakikishia wawekezaji hao kuwa Vijana wa kitanZania ni waaminifu. Siku kadhaa baada ya Spika wa bunge kunukuliwa akisema vijana wa Kitanzania SIO waaminifu.

Tarehe 21/4/2021 anaenda kukagua ujenzi wa stesheni ya Treni ya umeme iliyopo Pugu Dar, anasema "Mradi utaenda kama JPM alivyoahidi.."

Tarehe 20/5/2021 anafanya ziara Tanesco. Anazungumza na uongozi wa Tanesco kuhusu tatizo lililojitokeza katika ununuaji wa LUKU lililopelekea wananchi washindwe kununua LUKU siku tatu mfululizo, anaamuru meneja Tehama na wenzake waendelee kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

Tarehe 28/5/2021 anafanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha, anakuta watendaji wa wizara hiyo wakijilipa posho ya zaidi ya billioni 1.6 kwa kazi zisizochukua hata nusu saa, anawasimamisha kazi watendaji wakuu saba.
Serikali ina wasaidizi wengi tuu.
Raisi ana wasaidizi Makamo na waziri mkuu.
Halafu wanakuja mawaziri manaibu na makatibu.
Chini huko kuna wakurugenzi..

Sasa waziri mkuu anapotengua mkurugenzi kwa nini haoni kuwa waziri na msaidizi wqaziri na kaitbu mkuu wote ni wabovu.
Nadahni itolewe indhari ya kuwa raisi au makamo au waziri mkuu wakifanya ziara na kugundua madudu basi kuazia waziri , msaidizi waziri na katibu wajieleze au kutimuliwa.

Ndipo watakapo fanya kazi sawa sawa.
 
2799136_1622926778129.png
 
Uzalendo ni ule wa kusifia mkuu? Ama ni uzalendo wa kupenda nchi yako??Miaka ya awamu ya tano uzalendo ulipoteza maana! Maana yake ilikuwa kuisifia ccm na mwenyekiti wake!! Eti ndiyo uzalendo!! Shame on you!!
 
UTENDAJI KAZI: MAJALIWA KASSIM MAJALIWA

Tarehe 10/4/2021 anafanya ziara kukagua ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere lililopo Rufiji na kuwaahidi Watanzania kuwa ujenzi utaendelea kama kawaida na kumalizika kwa muda uliopangwa.

Tarehe 19/4/2021 anakwenda kuukagua mradi wa mabasi ya mwendokasi baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya Ufanisi wa mradi huo, anakuta utendaji ni mbovu anamsimamisha kazi mkurugenzi wa fedha wa mradi huo Susana Steven Chaula.

Tarehe 19/4 /2021 anakwenda kukagua bandari ya nchi kavu Ubungo Baada ya magari ya mizigo kukwama kwa zaidi ya siku tatu..anafanya mazungumzo na madereva pamoja na watendaji wa bandari

Tarehe 19/4/2021 anafanya ziara kiwanda cha kuunganisha magari cha GFA kilichopo Kibaha, Pwani. Anawahakikishia wawekezaji hao kuwa Vijana wa kitanZania ni waaminifu. Siku kadhaa baada ya Spika wa bunge kunukuliwa akisema vijana wa Kitanzania SIO waaminifu.

Tarehe 21/4/2021 anaenda kukagua ujenzi wa stesheni ya Treni ya umeme iliyopo Pugu Dar, anasema "Mradi utaenda kama JPM alivyoahidi.."

Tarehe 20/5/2021 anafanya ziara Tanesco. Anazungumza na uongozi wa Tanesco kuhusu tatizo lililojitokeza katika ununuaji wa LUKU lililopelekea wananchi washindwe kununua LUKU siku tatu mfululizo, anaamuru meneja Tehama na wenzake waendelee kukaa pembeni kupisha uchunguzi.

Tarehe 28/5/2021 anafanya ziara ya kushtukiza wizara ya fedha, anakuta watendaji wa wizara hiyo wakijilipa posho ya zaidi ya billioni 1.6 kwa kazi zisizochukua hata nusu saa, anawasimamisha kazi watendaji wakuu saba.
Kasi ya kupiga kiwi nyeusi kichwani mwake?
 
Back
Top Bottom