Kasi ya utendaji ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa inatufuta machozi wazalendo

Huyu anafanya kazi kwa ajili ya kujionesha, Hana uchapakazi wowote, Ni one man show, kwanini wasiweke mfumo? Ni one man show ya kutafuta sofa, Majaliwa hafai
Hivi anapokea per diem, maana kila siku yuko safarini na anatumia usafiri wetu. Ni Mwalimu tu alikuwa hachukui per diem
 
Hivi anapokea per diem, maana kila siku yuko safarini na anatumia usafiri wetu. Ni Mwalimu tu alikuwa hachukui per diem
Tulia sindano ikuingie
 
Hakika mheshimiwa Majaliwa utendaji kazi wake ni wa kutukuka.
Mungu azidi kumpa afya tele aendelee kusafisha ofisi za umma dhidi ya uzembe na ubadhirifu wa fedha.
 
Amani iwe nanyi.

Kuna kauli mbalimbali ambazo zilitolewa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh Samia Suluhu Hassan zilizopelekea watanzania kuwa wamoja zaidi na kuifanya nchi kutulia mara baada ya msiba mzito wa kuondokewa na rais Magufuli.

Binafsi ninazo kauli mbili ,kama na wewe unazo weka hapq.
1. Mimi na Magufuli ni kitu kimoja.
Ikumbukwe mara baada ya kufariki rais Magufuli liliibuka kundi likiongozwa na Tundu Lisu na Lema likawa linashangilia kifo hicho, hali hiyo ilienea hadi kwa baadhi ya wabunge kama Nape na Makamba, badala ya kujadili bajeti wakawa wanajadili nani ni zaidi kati ya Magufuli na Samia.!
Hali hiyo iliwakera sana wazalendo wa nchi yetu na rasmi likaibuka kundi jingine lililobatizwa jina la walinda legacy ya Magufuli, moja ya watu wa kundi hili waliojitokeza hadharani kukemea ni mbunge Lusinde ,pia Lazaro Nyalandu aliyekuwa kada wa Chadema alikemea hadharani na kutangaza kuachana na Chadema kwa kitendo chao cha kumtukana alipohudhuria msiba Chato.
Katikati ya mvurugano huo aliibuka rais Samia na kuwachana live Wabunge na Chadema kwa ujumla kuwa yeye na Magufuli ni kitu kimoja na serikali yake ya awamu ya sita haijatokana na uchaguzi mbali imetokana yeye Samia kuaminiwa na hayati Magufuli na kufanywa kuwa makamu wa rais.
Kauli hii ya Samia ililifanya kundi la walinda Legacy kuibuka kidedea dhidi ya kundi la washangilia kifo hivyo nchi kutulia.

2. Wala rushwa ,wazembe majambazi na mafisadi kuendelea kubanwa.
Rais Samia alitangaza hadharani kwamba katika masuala ya rushwa atasimama imara na akamtumbua mkurugenzi wa bandari na kuagiza Takukuru wafanye uchunguzi BOT na wizara ya fedha.
Pia kuwajibisha wote waliojaribu kuchezea mifumo ya Tanesco ,TRA na bandari.
Hatua hizi zilifanya nchi kutulia kwa sababu watanzania wengi waliona rasilimali zao bado ziko salama kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya tano chini ya hayati Magufuli.
 
Serikali ina wasaidizi wengi tuu.
Raisi ana wasaidizi Makamo na waziri mkuu.
Halafu wanakuja mawaziri manaibu na makatibu.
Chini huko kuna wakurugenzi..

Sasa waziri mkuu anapotengua mkurugenzi kwa nini haoni kuwa waziri na msaidizi wqaziri na kaitbu mkuu wote ni wabovu.
Nadahni itolewe indhari ya kuwa raisi au makamo au waziri mkuu wakifanya ziara na kugundua madudu basi kuazia waziri , msaidizi waziri na katibu wajieleze au kutimuliwa.

Ndipo watakapo fanya kazi sawa sawa.
 
Uzalendo ni ule wa kusifia mkuu? Ama ni uzalendo wa kupenda nchi yako??Miaka ya awamu ya tano uzalendo ulipoteza maana! Maana yake ilikuwa kuisifia ccm na mwenyekiti wake!! Eti ndiyo uzalendo!! Shame on you!!
 
Kasi ya kupiga kiwi nyeusi kichwani mwake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…