Kutokana na upotoshaji ambao umekuwa unaendelezwa na viongozi wetu, binafsi kama raia nimeshindwa kuvumilia.
Hii imekuja baada ya leo kumsikia tena Mh. Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu, kusema kilichopitishwa na bunge ni makubaliano kati ya nchi mbili. Nchi ya Tanzania, na nchi ya Dubai! Huu ni upotoshaji ambao hatupaswi kuufumbia macho kabisa kama raia.
Kwa hili nilichogundua ni kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa hawana upeo mkubwa wa kuelewa na kubaini mambo endapo suala dogo tu la kubaini Dubai ni mji na wala siyo nchi limewashinda. Na hapa tunaongelea kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni!!
Kwa bahati mbaya pia, hata Mkuu wa muhimili wa Bunge; Mh. Tulia Acson, amekuwa anairejelea Dubai kama nchi na siyo Mji!! Na hapa tunamzungumzia msomi wa ngazi ya PhD!
Kwa kweli, kwa haya yanayozidi kujidhihirisha, inabidi taasisi yetu nyeti ya TISS, iwe inajiridhisha kwanza na upeo wa viongozi wetu kwanza kabla ya kuaminiwa kupewa majukumu makubwa.
Maana hii ni hatari sana kwa Taifa, kuongozwa na viongozi wenye upeo finyu wa mambo.
Nimalizie kwa kusema kuwa; Dubai ni mojawapo ya majimbo 7 yanayounda Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates). Makao makuu ya UAE yapo Abu Dhabi kama ambavyo yetu yako Dodoma. Hivyo endapo viongozi wetu wakishupaza shingo, basi nchi yetu ya Tanzania itakuwa inaingia makubaliano kati yake na mji mmojawapo wa nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Niko pale, nasubiri marekebisho kama kuna sehemu nimekosea.
Ee Mwenyezi Mungu, sisi watoto wako wa Tanzania huwa tunakosea wapi linapokuja suala la kuchagua viongozi wetu?!
Amina.