Kassim Majaliwa, elewa Dubai siyo nchi, bali ni Mji

Kassim Majaliwa, elewa Dubai siyo nchi, bali ni Mji

unataka kusema zanziba ni mji si nchi mbona zanzibar imejiunga na tanganyika na kua tanzania na zanzibar ina weka mikataba yake na nchi za nje, kwa nini dubai nayo isiwe ni nchi wakati ina mfalme wake na inapolice wake na mavazi ya polisi ni tofauti na abudhabi nchi iliyojiunga nayo UAE ni nchi 7 zilijiunga pamoja na kuwa nchi moja lakini kila sehemu mpaka sasa ina mfalme wake mfano, majuzi mji mkuu walipitisha mapumziko ya wiki yawe jumapili badala ya ijumaa wote wakakubaliana ila nchi moja katika nchi 7 inaitwa sharjah ikagoma wao sharjah wakaendelea kuwa ijumaa kuwa siku ya mapumziko hizi ni nchi zilizoungana na bado zinawatawala wake
Kama Zanzibar ina Mamlaka kamili, kwanini ilipotaka kuwa mwanachama wa OIC tuliipiga pini??
 
Shida yote ilianzia hapa 👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼👇🏼 , najuta kabisa kuwasanua hawa jamaa

Hata Zanzibar sio nchi lakini inaingia mikataba tofauti vile vile
Mikaba ya kibiashara au ya kiserikali? Yaani kati ya serikali ya Watu wa Marekani na Zanzibar!
Na sio kati ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na USA
 
Kutokana na upotoshaji ambao umekuwa unaendelezwa na viongozi wetu, binafsi kama raia nimeshindwa kuvumilia.

Hii imekuja baada ya leo kumsikia tena Mh. Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu, kusema kilichopitishwa na bunge ni makubaliano kati ya nchi mbili. Nchi ya Tanzania, na nchi ya Dubai! Huu ni upotoshaji ambao hatupaswi kuufumbia macho kabisa kama raia.

Kwa hili nilichogundua ni kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa hawana upeo mkubwa wa kuelewa na kubaini mambo endapo suala dogo tu la kubaini Dubai ni mji na wala siyo nchi limewashinda. Na hapa tunaongelea kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni!!

Kwa bahati mbaya pia, hata Mkuu wa muhimili wa Bunge; Mh. Tulia Acson, amekuwa anairejelea Dubai kama nchi na siyo Mji!! Na hapa tunamzungumzia msomi wa ngazi ya PhD!

Kwa kweli, kwa haya yanayozidi kujidhihirisha, inabidi taasisi yetu nyeti ya TISS, iwe inajiridhisha kwanza na upeo wa viongozi wetu kwanza kabla ya kuaminiwa kupewa majukumu makubwa.

Maana hii ni hatari sana kwa Taifa, kuongozwa na viongozi wenye upeo finyu wa mambo.

Nimalizie kwa kusema kuwa; Dubai ni mojawapo ya majimbo 7 yanayounda Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates). Makao makuu ya UAE yapo Abu Dhabi kama ambavyo yetu yako Dodoma. Hivyo endapo viongozi wetu wakishupaza shingo, basi nchi yetu ya Tanzania itakuwa inaingia makubaliano kati yake na mji mmojawapo wa nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Niko pale, nasubiri marekebisho kama kuna sehemu nimekosea.

Ee Mwenyezi Mungu, sisi watoto wako wa Tanzania huwa tunakosea wapi linapokuja suala la kuchagua viongozi wetu?!

Amina.
Mshangao kwangu, sio kwamba Waziri mkuu, eti hajui kuwa Dubai sio nchi.

Mshangao kwangu ni:-
mtu mwenye hadhi ya PM, Kukutwa hajui kuwa MAKUBALIANO NI MKATABA NA MKATABA NI MAKUBALIANO.,,!!?.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kutokana na upotoshaji ambao umekuwa unaendelezwa na viongozi wetu, binafsi kama raia nimeshindwa kuvumilia.

Hii imekuja baada ya leo kumsikia tena Mh. Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu, kusema kilichopitishwa na bunge ni makubaliano kati ya nchi mbili. Nchi ya Tanzania, na nchi ya Dubai! Huu ni upotoshaji ambao hatupaswi kuufumbia macho kabisa kama raia.

Kwa hili nilichogundua ni kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa hawana upeo mkubwa wa kuelewa na kubaini mambo endapo suala dogo tu la kubaini Dubai ni mji na wala siyo nchi limewashinda. Na hapa tunaongelea kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni!!

Kwa bahati mbaya pia, hata Mkuu wa muhimili wa Bunge; Mh. Tulia Acson, amekuwa anairejelea Dubai kama nchi na siyo Mji!! Na hapa tunamzungumzia msomi wa ngazi ya PhD!

Kwa kweli, kwa haya yanayozidi kujidhihirisha, inabidi taasisi yetu nyeti ya TISS, iwe inajiridhisha kwanza na upeo wa viongozi wetu kwanza kabla ya kuaminiwa kupewa majukumu makubwa.

Maana hii ni hatari sana kwa Taifa, kuongozwa na viongozi wenye upeo finyu wa mambo.

Nimalizie kwa kusema kuwa; Dubai ni mojawapo ya majimbo 7 yanayounda Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates). Makao makuu ya UAE yapo Abu Dhabi kama ambavyo yetu yako Dodoma. Hivyo endapo viongozi wetu wakishupaza shingo, basi nchi yetu ya Tanzania itakuwa inaingia makubaliano kati yake na mji mmojawapo wa nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Niko pale, nasubiri marekebisho kama kuna sehemu nimekosea.

Ee Mwenyezi Mungu, sisi watoto wako wa Tanzania huwa tunakosea wapi linapokuja suala la kuchagua viongozi wetu?!

Amina.
Daah!! Kwamba hawajui kua lile ni jiji ama wameamua tu? Au kwakua watanzania washaonwa ni dormant wanajua wabongo wataamin!!
 
Tatizo wabongo wanajiona wanajua sana kumbe hamjui kitu… Kuna Dubai Emirate ambayo inajitegemea pia na pia kuna Dubai ambayo city.Mnalishana matango pori huko kwenye vijiwe vya kahawa halafu manakuja humu kuongea pumba mkidhani ni wasomi kumba ugumbaru tu.
 
Shida ya Tanzania ni elimu

Emirate maana yake ni (state, country au nchi).

Ndio maana kuna aina mbili ya katiba duniani.

1. Unitary constitution zinazochukulia miji na sehemu yote ya mipaka ni sehemu moja ya nchi na kuna central government inayoamua kila kitu.

2. Federal constitution, ukiona nchi inatumia katiba hiyo maana yake ‘nation of nations’ waliomo humo ni sovereign states in their own rights.

Katiba zote za federal states aziwezi lingana depending na devolved matters walizoamua states zilizoungana kujiamulia.

Hata US NY, California, Texas na states nyingine zote ni nchi technically. Ndio maana states zote zinabendera zao rasmi 👇.

Federal Constitution ya USA maswala ya kibiashara za kimataifa na ulinzi yamewekwa chini ya federal government.

Sasa badala ya watu kusoma ‘federal constitution’ ya UAE on devolved matters walizonazo Dubai emirates kama wanaweza ingia IGA watanzania wanakwambia Dubai ni mkoa.

Just appalling our education system, 90% ya wachangiaji wa siasa hawana ata abc ya foundation ya siasa zenyewe.

Ifike wakati tuambizane ukweli, uwezo wa ufahamu wa mambo ni mdogo kwa average person elsewhere duniani.
 
Shida ya Tanzania ni elimu

Emirate maana yake ni (state au nchi).

Ndio maana kuna aina mbili ya katiba duniani.

1. Unitary constitution zinazochukulia miji yote ni sehemu ya nchi moja ya nchi na kuna central government.

2. Federal constitution, ukiona nchi inatumia katiba hiyo maana yake hizo waliomo humo ni states au nchi in their own rights.

Katiba zote za federal states aziwezi lingana depending na devolved matters za katiba zilizozipa states zilizoungana. Hata US NY, California, Texas na states nyingine zote ni nchi technically.

Federal Constitution yao maswala ya kibiashara na ulinzi yamewekwa chini ya central government.

Sasa badala ya watu kusoma ‘federal constitution’ ya UAE on devolved matters walizonazo Dubai emirates kama wanaweza ingia IGA watanzania wanakwambia Dubai ni mkoa.

Just appalling our education system, 90% ya wachangiaji wa siasa hawana ata abc ya foundation ya siasa zenyewe.

Ifike wakati tuambizane ukweli, uwezo wa ufahamu wa mambo ni mdogo kwa average person elsewhere duniani.
Kuna watu hawaelewi hili jambo na history ya UAE lakini wanaongea kwa kashfa na kejeli. Hizi Emirates 7 zilkuwa zinajitegemea kabla ya kuungana na kuwa na UAE lakini kuna madaraka yaliachwa local kwa hizi emirates mpaka sheria za ndani hawafanani ni mambo yao ya ndani ila yako mambo ni ya Federal state na wako wafanyakazi wa ndani na wako wa Federal state, moja ya kanuni zao kuwa Rais siku zote atatoka Abudhabi na Makamu/ Waziri mkuu kutoka Dubai kwa sababu ya mchango wao mkubwa katika budget ya Federal state. Lakini hizi emirates zina mipaka yake ndani ya UAE na ukivuka mipaka hii unaanza kufuata sheria za emirate uliyoingia. Kama kipindi cha corona kila emirate ilikuwa na sheria zake na ilikuwa ukitoka Dubai kuingia Abdudhabi ilikuwa lazima ufanye PCR. Pia kila emirates ina mtawala wake kama Dubai ni yakina Makhtoom na Abudhabi ni kina Nahyan wana police wao na sheria zao za ndani kwa maana yako mambo ya federal na yako ya emirates na kuna Budget ya Dubai na iko ya Federal na sera zao hazifanani za kiuchumi kila emirates in sheria zao. Hii UAE wana katiba yao sasa hujui yote ya humo ndani mpka upitie usome ila mpaka mashirika sio ya fedral mfano tu Emirates airline, DP, sijui Emaar na mengi yu hay ni mali ya Dubai sio UAE wao wanachangia tu budget ya UAE(Federal) na Abudhabi wana Ettihad... Sharjah wana Air Arabia. Kila emirate wana own business zao ila federal state budget wanachangia japokuwa Abudhabi ndio wanatoa mchango mkubwa sana sababu ya utajiri wao. Ukiondoa Abdudhabi, Dubai na Sharjah kidogo emirates zingine hawana utajiri ni kawaida tu. Kujibu yes Dubai sio nchi lakini wana mamlaka yao based na katiba yao ni kama sisi tulivyowapa Zanzibar na wana limit pia.
 
Laba wewe ndiye hujaelewa..

Ni kweli Dubai ni moja ya Emirate (ufalme mdogo au ki - dola kidogo) zinazounda dola kuu ya kifalme inayoitwa United Arabs Emirates [UAE]..

Kama ilivyo ktk muungano wetu wa Tanganyika. & Zanzibar na kuunda kuunda dola kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) bila kujali kasoro zilizo ktk muungano wetu..

Katika JMT, bado ndani yake Kuna nchi mbili; ya Tanzania na Zanzibar na Kila nchi Ina mamlaka yake i.e mamlaka ya JMT na ile ya Zanzibar..

Vivyo hivyo huko UAE, iko mamlaka kuu ya muungano na vivyo hivyo hizi Emirates ndogo ndogo obviously ikiwemo ya Dubai zina mamlaka zao kamili.

Na bila shaka, hizi Emirates ndogo ndogo ikiwemo ya Dubai nazo zina mamlaka yake Kamili ikiwemo ya kuingia mikataba ya kimataifa kama huu dhidi ya Tanzania...

Ni ngumu mkoa usio na sovereignty as a state kuingia mkataba na sovereign State kama Tanzania...

Kama hii imefanyika, obvious itakuwa ni utapeli na uhuni wa kimataifa unaostahili kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu...

Na si hili tu, bali kama kweli ktk mkataba huu nchi yetu itakuwa imetiliana saini ya muhusiano ya kimataifa na nchi isiyo na sovereignty status halafu wanasheria wetu wakawa hawana ufahamu huu, basi si kosa kusema twaweza kusema kwa ujasiri kabisa kuwa, kumbe tuna wanasheria wajinga na wasio na uelewa wa mambo..!!
Marekani Ina nchi ngapi
 
Kwa kweli, kwa haya yanayozidi kujidhihirisha, inabidi taasisi yetu nyeti ya TISS, iwe inajiridhisha kwanza na upeo wa viongozi wetu kwanza kabla ya kuaminiwa kupewa majukumu makubwa.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwl majaliwa ,yupo kwenye kundi

Linalolalamikiwa mudawote na mpwayungu village
 
Wewe punguani, hata Vatican ni nchi ndani ya nchi.

Usilolijuwa ni usiku wa kiza.

Hivi tunaokufundisha wote kuwa Dubai ni nchi unatuona wajinga?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Kwahiyo United Arab Emirates ni bara au
 
Kutokana na upotoshaji ambao umekuwa unaendelezwa na viongozi wetu, binafsi kama raia nimeshindwa kuvumilia.

Hii imekuja baada ya leo kumsikia tena Mh. Kassim Majaliwa ambaye ni Waziri Mkuu, kusema kilichopitishwa na bunge ni makubaliano kati ya nchi mbili. Nchi ya Tanzania, na nchi ya Dubai! Huu ni upotoshaji ambao hatupaswi kuufumbia macho kabisa kama raia.

Kwa hili nilichogundua ni kwamba viongozi wetu kwa sehemu kubwa hawana upeo mkubwa wa kuelewa na kubaini mambo endapo suala dogo tu la kubaini Dubai ni mji na wala siyo nchi limewashinda. Na hapa tunaongelea kiongozi Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni!!

Kwa bahati mbaya pia, hata Mkuu wa muhimili wa Bunge; Mh. Tulia Acson, amekuwa anairejelea Dubai kama nchi na siyo Mji!! Na hapa tunamzungumzia msomi wa ngazi ya PhD!

Kwa kweli, kwa haya yanayozidi kujidhihirisha, inabidi taasisi yetu nyeti ya TISS, iwe inajiridhisha kwanza na upeo wa viongozi wetu kwanza kabla ya kuaminiwa kupewa majukumu makubwa.

Maana hii ni hatari sana kwa Taifa, kuongozwa na viongozi wenye upeo finyu wa mambo.

Nimalizie kwa kusema kuwa; Dubai ni mojawapo ya majimbo 7 yanayounda Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates). Makao makuu ya UAE yapo Abu Dhabi kama ambavyo yetu yako Dodoma. Hivyo endapo viongozi wetu wakishupaza shingo, basi nchi yetu ya Tanzania itakuwa inaingia makubaliano kati yake na mji mmojawapo wa nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Niko pale, nasubiri marekebisho kama kuna sehemu nimekosea.

Ee Mwenyezi Mungu, sisi watoto wako wa Tanzania huwa tunakosea wapi linapokuja suala la kuchagua viongozi wetu?!

Amina.
Majaliwa hajui kichwa chake kiko wapi na mguu wake uko wapi.

Dubai ni Emirate, ni jimbo la UAE.

Hata serikali ya jimbo inaweza kusaini intergovernment agreement, hiki ndicho kilichofanyika kwa Dubai na Tanzania.

Huhitaji kuwa nchi kusaini inter government agreement, unahitaji kuwa na government tu.

Tumejadili kirefu kama serikali ya Dubai ina nguvu za kusaini IGA

Mjadala uko hapa Huu Mkataba siyo Intergovernmental, Dubai siyo Nchi
 
NY ni jimbo au nchi?

Why do you think billionaires are running away from NY and claim Florida as their permanent residency, for tax evasion purposes?
 
NY ni jimbo au nchi?

Why do you think billionaires are running away from NY and claim Florida as their permanent residency, for tax evasion purposes?
Sijakuelewa unamaanisha nini na dhumuni la kuandika hivyo ni nini katika muktadha wa mazungumzo haya.

Mfano wa NY unaweza kuwa tofauti sana na mazungumzo haya, kwa sababu serikali kuu ya Marekani ina vizuizi sana kuzuia majimbo yake kuingia mikataba ya kimataifa, kwa njia ambayo serikali ya UAE haina vizuizi hivyo.

Mabilionea wengi wanakimbia NY kwenda Florida kwa tax avoidance, si tax evasion.

There is a big difference.
 
Back
Top Bottom