- Thread starter
- #21
Binafsi sijakuelewa Mkuu..Laba wewe ndiye hujaelewa..
Ni kweli Dubai ni moja ya Emirate (ufalme mdogo au ki - dola kidogo) zinazounda dola kuu ya kifalme inayoitwa United Arabs Emirates [UAE]..
Kama ilivyo ktk muungano wetu wa Tanganyika. & Zanzibar na kuunda kuunda dola kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) bila kujali kasoro zilizo ktk muungano wetu..
Katika JMT, bado ndani yake Kuna nchi mbili; ya Tanzania na Zanzibar na Kila nchi Ina mamlaka yake i.e mamlaka ya JMT na ile ya Zanzibar..
Vivyo hivyo huko UAE, iko mamlaka kuu ya muungano na vivyo hivyo hizi Emirates ndogo ndogo obviously ikiwemo ya Dubai zina mamlaka zao kamili.
Na bila shaka, hizi Emirates ndogo ndogo ikiwemo ya Dubai nazo zina mamlaka yake Kamili ikiwemo ya kuingia mikataba ya kimataifa kama huu dhidi ya Tanzania...
Ni ngumu mkoa usio na sovereignty as a state kuingia mkataba na sovereign State kama Tanzania...
Kama hii imefanyika, obvious itakuwa ni utapeli na uhuni wa kimataifa unaostahili kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu...
Na si hili tu, bali kama kweli ktk mkataba huu nchi yetu itakuwa imetiliana saini ya muhusiano ya kimataifa na nchi isiyo na sovereignty status halafu wanasheria wetu wakawa hawana ufahamu huu, basi si kosa kusema twaweza kusema kwa ujasiri kabisa kuwa, kumbe tuna wanasheria wajinga na wasio na uelewa wa mambo..!!
Kwa hiyo ni sahihi kuita Intergovernmental Agreement (IGA) kati yetu na Dubai au unamaanisha nini?