Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu ni uthibitisho wa ubovu wa Katiba ya 1977

Yaan Akili zenu cjui huwa mnaziacha wapi..
Mfano ingekuwa hvyo unavyotaka Hakuna mpinzan alogombea nae na watu wakapga kura za Hapana yeye na mkewe tu wangepiga za Ndyo Mbunge angekuwa nani?...
Hapa ndo mnapofeli Kutaka ktk mpya ktk maeneo ya Siasa tu wananch wanaona Mna Wivu mna visasi
 
Mfano ingekuwa hvyo unavyotaka Hakuna mpinzan alogombea nae na watu wakapga kura za Hapana yeye na mkewe tu wangepiga za Ndyo Mbunge angekuwa nani?...
Ktk duru za kidemokrasia hakunaga kupita bila kupingwa mkuu. Isome mada uilewe muktadha wake halafu urudi hapa.
 
Wananchi wamekataa kukuchagueni katika uchaguzi uliyopita sasa mnatafuta pa kufia kwa kisingizio cha katiba mpya

Hivi inamaana katiba yote inazungumzia uchaguzi tu wa raisi na wabunge maana sijawahi kukusikieni mkiongelea katiba katika nyanja nyingine

Ni ushahidi tosha kuwa mnadai katiba kwa tamaa zenu za madaraka na sio kwa ajili ya watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi wamekataa kukuchagueni katika uchaguzi uliyopita sasa mnatafuta pa kufia kwa kisingizio cha katiba mpya
Kama unaamini ulichokiandika sema "Su!" Na kama siyo kweli basi ufe kifo cha aibu. Haya sema "Su!"
 
Mi nimechoka eti raisi Samia,anaapishwa,anamteua makamo wake wa raisi,anateua baraza la Mawaziri,huku Majaliwa akiwa bado waziri mkuu,.....vichekesho hivi
 
Hapa ndo nashindwa kukuelewa mtoa mada.

Huo ni ubovu wa katiba kusema "mbunge wa kuchaguliwa" au ni ubovu watu kutokufuata katiba ?

katiba inasema waziri mkuu awe amechaguliwa na wananchi alafu watu wakamuweka waziri mkuu ambaye hajachaguliwa na wananchi

unadhani shida ni katiba au shida ni watu ambao hawajafuata katiba hiyo inavyosema ?

Kwa hiyo hapa tubadili katiba ili iseme "hata mbunge ambaye hajapigiwa kura na wananchi anawexa kuwa waziri mkuu" ?

Au tuwahimize watu wafuate katiba inayosema waziri mkuu lazima achaguliwe na wananchi ?

Ndugu Sexless
 
au ni ubovu watu kutokufuata katiba ?
Katiba isingekuwa mbovu ingejilinda na kujitetea yenyewe. Hapa namaanisha kila ambaye angejaribu kuivunja ingemng'ata kweli kweli.

Lkn kwa kuwa ni mbovu ndiyo maana inavunjwa kama ilivyotokea kwa akina Majaliwa kuwa W/mkuu wakati hakuchaguliwa na wananchi kama ambavyo katiba inataka.

N.B. Katiba nzuri huwa inaogopwa na watu
 
Sasa ubovu wa katiba katika kipengele hiko ni upi ?

Katiba imeelekeza watu ilikuwa wafuate,lakini watu hawajafuata.

Naomba unifahamishe katika kipengele hiko katiba ijitetee vipi baada ya kuwa katiba hiyo imeshakwisha fanya kazi yake ya kusema w.mkuu achaguliwe na wananchi ?
 
Maza nae Kwa katiba hiyo hiyo amepita bila kupingwa
 
Wewe ni mbogamboga au ni sampo yao?
 
Katiba haifanyi kazi kwa kipengele ni kama ilivyo kwenye mifumo ya uendeshaji wa gari ama mfumo wa chakula wa mwanadamu.

Ikitokea wakashona sehwmu ya haha kubwa utazuia mfumo mzima wa uchakataji chakula. You will abort the whole system of digestion just by blocking the colon (esp the anus).

Kwahiyo katiba yetu imempa mamlaka makubwa sana rais na kumfanya Mungu mtu anayeiyumbisha hata mihimili mingine iliyopaswa kuitetea katiba. Sasa endapo rais huyu atapendezwa na uvunjifu fulani wa katiba nani atazuia uvunjifu huo?

Majaliwa ameteuliwa na rais, mtu ambaye yuko juu ya katiba unategemea nn?
 
Hivi katiba mnafikiri ni mzimu, malaika au shetani! Au katiba ni Mungu?
Hakuna katiba nzuri Africa kama ya South Africa! Je! Imemzuia Mr. Zuma kujenga Nkadla, au Bwana Magashule wizi? Je! Imewazuia Guptas kuikamata serikali ya RSA? Na kama habari hizo huzijui, acha kuzungumzia katiba maana huna reference nzuri ya katiba. Katiba siyo kila kitu. Hawa wanaodai katiba mpya, hawana hoja yoyote ya kuwazodoa nayo serikali maana matakwa yote ya wananchi serikali wanayashughulikia vema.
 
Huyu bwana Kitimoto kazi yake nikutoa dislike kwenye kila comment 😂😂
bilashaka huyu atakuwa Ni devil
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…