Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu ni uthibitisho wa ubovu wa Katiba ya 1977

Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu ni uthibitisho wa ubovu wa Katiba ya 1977

Katiba haifanyi kazi kwa kipengele ni kama ilivyo kwenye mifumo ya uendeshaji wa gari ama mfumo wa chakula wa mwanadamu.
Kwa kipengele kile ambacho ulikitoa hakina shidaa kabisa kipo sawa,lakini shida ni kwamba hakuna vipengele vingine vya kuipa nguvu kipengele hiki.

Naomba nitajie mfano wa vipengele ambavyo ilitakiwa viwepo ili kukipa nguvu kipengele kile ulichokitla kwenye uzi.
Ikitokea wakashona sehwmu ya haha kubwa utazuia mfumo mzima wa uchakataji chakula. You will abort the whole system of digestion just by blocking the colon (esp the anus).
Mfano wale wabunge 19 wa chadema tunaambiwa ilitakiwa wavuliwe ubunge kwa mujibu wa katiba lakini mpaka leo wapo

jee katiba ilitakiwa ipate kifungu gani cha kutetea kifungu kinachosema wabunge wasio na vyama watolewe ubunge ?

Unadhani wale wabunge 19 wapo bungeni mpaka sasa kwa sababu hakuna kipengele tetezi kwenye katiba ?

Hiko kipengele tetezi kingekuwaje kwa mfano ?

Au ni kwa sababu haktiba haijafuatwa ipasavyo ndio maana wako pale M
 
Huyu maza yeye katiba imeeleza wazi kabisa nn Cha kufanya endapo rais aliyeko madarakani atafariki. So, kwa maza binafsi naona hakuna shida, katiba yetu mbovu ilizingatiwa.
Kama aktiba imeeleza wazi nini cha kufanya...

Kuna haja gani ya hiko kilichoelezewa wazi kipate mtetezi wakati hiko bado kinajitosheleza kwa kuweka wazi huko ?
 
Katiba ni muhimu sana lakini Katiba ya mashinikizo ya vikundi hayana faida kamwe maana hata likiundwa Bunge la Katiba watapemda hoja zao pekee zipite kinyume na hayo watagoma kwa kigezo Cha mambo yetu hayamo na wataaminisha watu kwamba Kuna kasoro kubwa hivyo basi muda,pesa kupotea Bure ndiyo maana Umoja wa mataifa unasisitiza Sana kukubali kutokukubaliana.

Hapa Kuna kundi kubwa lililoshawishiwa kuitaka Katiba mpya pia lipo kundi kubwa lililoshawishika kwamba Katiba mpya isubiri kitakachofuata ni msugano na cheche zikitoka kama upande wako utashinda shukuru Mungu na KAZI iendelee.

Swali ni kweli tumewatuma mfanye hayo?

Ni kweli mnadhamira ya dhati kupigania hayo mnayodhani ni matakwa ya wananchi?
 
Hakuna katiba nzuri Africa kama ya South Africa! Je! Imemzuia Mr. Zuma kujenga Nkadla, au Bwana Magashule wizi? Je! Imewazuia Guptas kuikamata serikali ya RSA?
Una habari Zuma kahukumiwa miezi 15 jela? Hapa Tanzania unaweza hata kumshitaki rais? Kwann hili haiwezekani Tanzania lkn limewezekana RSA?

Ni kwasabb katiba yao ni nzuri, na katiba nzuri ina tabia ya kujilinda na kujitetea. Halafu sifa nyingine ya katiba nzuri Ni kwamba hakuna aliye juu yake.

Hizo kashfa zote mpk wewe wa kwa Mtogole umezifahamu ni kwasabb Kuna taasisi imara zinazombana yeyote. Hapa Magufuli alikuwa anabadilisha Kijiji cha Chato kuwa jiji hatuna Cha kumfanya.

N.B. Unaongea na mtu mwenye akili nene. Rudi tena.
 
Kama aktiba imeeleza wazi nini cha kufanya...

Kuna haja gani ya hiko kilichoelezewa wazi kipate mtetezi wakati hiko bado kinajitosheleza kwa kuweka wazi huko ?
Sijalipata vizuri swali lako
 
Utuambie wewe kwanza una elimu gani Bila kusahau umri wako.

Kazana zaidi kwenye physics lakini pia basic maths, haya mengine utayakuta ukikua.
Ungemsaidia kumuonyesha kifungu cha sheria ili improve wrong
 
Kwahiyo katiba yetu imempa mamlaka makubwa sana rais
Hayo mamlaka makubwa ulitaka apewe nani kisha raisi awe na mamlaka madogo madogo ?


na kumfanya Mungu mtu anayeiyumbisha hata mihimili mingine iliyopaswa kuitetea katiba
Mfano TAKUKURU ikapewa mamlaka ambayo raisi alikuwa nayo,yaani takukuru sasa yale mamlaka makubwa ambayo alikuwa nayo raisi kapewa mkuu wa takukuru.

Nipe sababu kwa nini mkuu wa takukuru asiwe Mungu mtu katika taasisi yake kwa huku kupewa mamlaka makubwa haya zaidi ya raisi ?
anayeiyumbisha hata mihimili mingine iliyopaswa kuitetea katiba.
Kama hiyo mihimili mingine ikipewa nguvu kubwa zaidi ya raisi na hiyo mihimili ikavunja katiba nani atasimama kuitetea ?

Usiniambie haiwezekani kwa sababu sasa hivi tunaona watu wenye mamlaka ya kufanya jambo wao ndo kwanza wanalivunja na hakuna mtu naaweza fanya hivyo swali langu lijibiwe kwa sababu ndio uhalisia.
Sasa endapo rais huyu atapendezwa na uvunjifu fulani wa katiba nani atazuia uvunjifu huo?
Na endapo mihimili ya kutetea katiba ikapendezwa na uvunjifu wa katiba nani atasimama kuitetea katiba hiyo ?

Usiniambie haiwezekani kwa sababu tunaona leo watu ambao wanatakiwa kupambana na rushwa wao ndo wanakula na hakuna kinachofanyika hivyo swala laangu lina uhalisia.
Majaliwa ameteuliwa na rais, mtu ambaye yuko juu ya katiba unategemea nn?
Mfano wa mambo aliyofanya mama samia ambayo yapo kwa mujibu wa katiba unadhani kayafanya mambo hayo kwa kuwa yupo chini ya KATIBA katika hayo mambo ?

Yapo mambo kafanya kafuata katiba na angeweza kufanya kinyume na hivyo.

Huko kuyafanya kwake mambo hayo ni kwa sababu yupo chini ya katiba ?
 
Sijalipata vizuri swali lako
Nafafanua mkuu.

Ulisema katiba imeeleza wazi katika kifungu fulani kipi kifanyike,tena imeeleza wazi kweli kweli kama ulivyosema.

Wewe unadai kwamba katika yenyeye haijitetei. Kwa maana katika inatakiwa ijitetee yenyewe.

Sasa assume vkwamba vile vipengele ambavyo vipo katika katiba hiyo kwa ajili ya kutetea vipengele vingine tuviite vipengele tetezi.

Swala linakuja hivi...

Kuna haja gani ya hiko kilichoelezewa wazi katika katiba kipate mtetezi wakati hiko kipengele kimeshaweza waaazi kabisa kipi kifanyike juu ya jambo fulani ?
 
Kwa mujibu wa Katiba yetu hii mbovu ktk ibara ya 52 (2).

(..)Rais atamteua mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi, kuwa waziri Mkuu (..)

N.B. Kila kwenye (..) kuna maneno nimeyaruka.

Sasa huyu mhe Majaliwa alichaguliwa na wananchi ktk Jimbo lake? Jibu ni HAPANA hakuchaguliwa na wananchi. Bali alipita bila kupingwa (maneno batili kabisa ktk demokrasia)

Hata kama alikuwa mgombea pekee ilipaswa wananchi wapige kura kumkubali ama la! Lkn haikufanyika hivo. Kwahiyo wananchi hawakushiriki kabisa katika kumchagua mtu huyu ambaye ndiyo waziri mkuu wa JMT. Pathetic!

Sasa kwann mhe Majaliwa amekuwa Waziri Mkuu ikiwa hakutimiza vigezo vya kikatiba? Jibu ni rahisi tu. Katiba yetu ina mianya mingi ya kupenyeza maovu yanayotokana na uvunjifu wa katiba.

Ndiyo maana tunaitaka katiba mpya itakayo ondoa ujinga huu katika demokrasia.
wewe umechanganyikiwa mkuu, hatuendi hivyo jenga hoja za msingi usitafutize mambo ambayo hayapo. Katiba mpya inakuja tulia
 
Hapa ndo nashindwa kukuelewa mtoa mada.

Huo ni ubovu wa katiba kusema "mbunge wa kuchaguliwa" au ni ubovu watu kutokufuata katiba ?

katiba inasema waziri mkuu awe amechaguliwa na wananchi alafu watu wakamuweka waziri mkuu ambaye hajachaguliwa na wananchi

unadhani shida ni katiba au shida ni watu ambao hawajafuata katiba hiyo inavyosema ?

Kwa hiyo hapa tubadili katiba ili iseme "hata mbunge ambaye hajapigiwa kura na wananchi anawexa kuwa waziri mkuu" ?

Au tuwahimize watu wafuate katiba inayosema waziri mkuu lazima achaguliwe na wananchi ?

Ndugu Sexless
Tatizo letu sisi Watanzania ni wajinga sana,ni kweli Katiba madhaifu sana tena ya kutosha lakini bado kuna mambo mengi yaliyomo katika Katiba hii mbovu Serikali imeyakandamiza lakini hakuna aliyewajibika.
Kuna mambo yamo katika Katiba hii ya kama hilo la Waziri Mkuu kichaguliwa lakini Wananchi tupo tu.

Kabla ya kukosoa ubovu wa Katiba lazima tukubali bado sisi ni tatizo,hata hayo mazuri yanaweza yakawekwa kwenye katiba yakasiginwa na bado tusifanye chochote.
 
Tatizo letu sisi Watanzania ni wajinga sana,ni kweli Katiba madhaifu sana tena ya kutosha lakini bado kuna mambo mengi yaliyomo katika Katiba hii mbovu Serikali imeyakandamiza lakini hakuna aliyewajibika.
Kuna mambo yamo katika Katiba hii ya kama hilo la Waziri Mkuu kichaguliwa lakini Wananchi tupo tu.

Kabla ya kukosoa ubovu wa Katiba lazima tukubali bado sisi ni tatizo,hata hayo mazuri yanaweza yakawekwa kwenye katiba yakasiginwa na bado tusifanye chochote.
Ndo nafanya mahojiano na mtoa mada hapa mkuu.

Maana sijamuelewa..
 
Mi huwa nashangaa Sana ,iyo slogan ya kupita bila kupingwa.kwa mara ya kwanza nimeisikia utawala wa Joker.wa tz 60mil apite bila kupingwa?.Cha ajabu Sasa waliopita bila kupingwa ,majimbo yao ukiyatembelea unaweza lia ugalegale kwa uchungu.miundo mbinu hovyo,shule zinamapungufu...yaani kila kitu hovyooooo.
Najua watakuja watasema Nmetumwa na chadema ,ila ukweli lazima muda mwingine tuutapike tu
 
Back
Top Bottom