Dhima ya kuanzishwa NFRA ni ili kuweka hifadhi ya chakula pale endapo mvua zinakuwa za kutosha na mavuno yanakuwa mengi kuliko mahitaji, ili endapo msimu ujao kunatokea upungufu wa mvua, basi NFRA wanauza chakula kwa bei ya soko ili kuziba pengo, na endapo uzalishaji utaendelea kuwa mkubwa msiku unaofuata basi utaratibu unafanyika kukiuza chakula nchi jirani zenye uhaba wa chakula kama Kenya , Uganda na Sudan kusini.
Hivyo basi, ni jukumu la NFRA kulinda wakulima kwa kuwahakikishia soko ili wapate nguvu na uwezo wa kulima mwaka hadi mwaka, hilo ndio jukumu la NFRA.