Kassim Majaliwa: Tuache tabia ya kuwatengenezea viongozi migogoro, unaweza kupambana sana ukitaka ukae ukakuta anakaa mwingine

Kassim Majaliwa: Tuache tabia ya kuwatengenezea viongozi migogoro, unaweza kupambana sana ukitaka ukae ukakuta anakaa mwingine

siasa chafuchafu, siasa za propaganda, siasa za kijingajinga, siasa takataka... NCHI HAIWEZI KUENDELEA KWA KUENDELEA KUACHA PUMBAVU ZILIPIGA PIGA KELELE NA SIASA ZA HOVYOHOVYO.....
Daaah
 
Katika hali isiyodhaniwa na wengi Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Majaliwa Khassim Majaliwa amfunda Mhe Job Yustino Ndungai kuhusu nafasi ya Urais,


===========

Kassim Majaliwa: Madaraka yote yanatolewa na mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amepanga kila kitu nani atakuwa nani katika kipindi gani.

Hata ukilazimisha kutaka nafasi hiyo, huwezi kama mwenyezi Mungu hajasema nenda na wala usitumie njia yoyote ya kumuathiri mwenzako ili apate madhara eti atoke hapo wewe uende, nani amekwambia wewe utakwenda hapo?

Tuache tabia ya kuacha viongozi ya kuwaacha viongozi wafanye kazi yao ya kuwahudumia watanzania na kuwatengenezea migogoro kila siku tena mingine ni ya kusingizia tu.

Kama mwenyezi Mungu hajasema hutakuwa, utatumia mihela mingi itapotea tu, utakwenda na mambo mengine ya giza huko hutamudu, mwenyezi Mungu amesema huyu ni huyu.

Tuheshimu walioko kwenye nafasi za kuwatumikia watanzania wafanye kazi yao kwa weledi.

Uongozi wa sekta yoyote ile unaongozwa na mwenyezi Mungu, unaweza kupambana sana unataka ukae, ukakuta haukai anakaa mwingine.

Kwahiyo utaanza kuwaathiri wote hao wanaokaa hapo kwasababu wewe unataka kumbe mwenyezi Mungu hataki, lazima tujue kwamba, madaraka yoyote yanatolewa na Mwenyezi Mungu.


>>Msikilize kwa makini<<<


View attachment 2064822
Busara za PM
 
Hakika Rais Samia ameletwa Tanzania kuliponya Taifa,

Kitendo cha kukutana na Tundu Lissu Brussels Ubelgiji ni kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo kwa Taifa,

Tumuunge mkono Rais wetu kwa haya kwani anastahili sana,
 
Hakika Rais Samia ameletwa Tanzania kuliponya Taifa,

Kitendo cha kukutana na Tundu Lissu Brussels Ubelgiji ni kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo kwa Taifa,

Tumuunge mkono Rais wetu kwa haya kwani anastahili sana,
Hana uwezo wa kuongoza bado.Ebu muangalie Dr Mwinyi uongozi wake zanzibar utaona hapa hamna kitu.Nafikiri anaweza kuondolewa.
 
Back
Top Bottom