Kataa kabisa urafiki au mahusiano ya kawaida na Askari Polisi

Polisi wenyewe hawataki ushkaji ndo maana wanakufanyia mabaya sasa wewe kwanini uwaze urafiki nao? Huwezi kuwa na urafiki na polisi kama huna tabia za kijipendekeza kwao ukiwa na mishe zako huo urafiki hauwezi kuwepo.
 
Polisi wenyewe hawataki ushkaji ndo maana wanakufanyia mabaya sasa wewe kwanini uwaze urafiki nao? Huwezi kuwa na urafiki na polisi kama huna tabia za kijipendekeza kwao ukiwa na mishe zako huo urafiki hauwezi kuwepo.
Mkuu Lucha usiweke wote katika kapu moja kuna wengine ni wazuri kama zilivyo kazi zote kuna wabaya na wazuri.Never say never.
 
Mkuu Lucha usiweke wote katika kapu moja kuna wengine ni wazuri kama zilivyo kazi zote kuna wabaya na wazuri.Never say never.
Ni kweli najua hata siku moja binadamu hawawezi kuwa wabaya wote au wote kuwa wazuri , ndani ya familia moja tu hamuwezi wote kuwa watoto wema lazima atakuwepo mmoja anazingua .

Ila hoja ya jamaa ni kutokua na urafiki na polisi wote kwahiyo ndo maana nikasema kutokua na urafiki nao ni rahisi tu unakua na mishe zako tu ni ngumu sana yeye kukufata ili muwe marafiki kama wewe huhitaji huo urafiki.

Kwenye hizi jamiii tunazoishi wabaya wapo ndani yetu na hao hao ndo wanakuuza kwa polisi , ye polisi hadi ajue unavuta bangi na ndani umetunza ya kuuza atakae kuchomea ni huyo huyo jirani yako na usitegemee polisi wakija watakwambia kuwa jirani yako ndo katuambia.

Kwahiyo ni sisi sisi ndo tunajipendekeza kwao urafiki huwa hawauanzishi wao ila tunaanzisha sisi.
 
Yamekusibu mangapi, funguka ili tujue
 
Hawa ndugu zetu sjui nn kinawasumbua wakati kwao maisha ni mazuri may be Tamaa na roho mbaya zinawasumbua
 
Wana maisha Mabaya Chief??
Wanaishi kwa hali ngumu chief nadhani kwasababu ya machozi ya watu, kwenye kota zao wengine wanakatiwa hadi maji ya bomba kwa kutokulipa bili.

Wale wa barabarani kwenye check point wanachukua hadi buku kwa madereva kwa kuomba kwa kung'ang'ania.

Bado hujaona wengi walioshastaafu.
 
Naunga mkono hoja, Polisi ni watu wa hovyo kupata kutokea.
Nakumbuka mnamo mwaka 2018 hapa Mbeya nilijipata nikiwa urafiki uchwara na polisi mmoja tena mbaya zaidi jamaa yupo kitengo cha uchunguzi wa makosa ya jinai (CID). Aisee jamaa alinisababishia matatizo makubwa sàna ikiwemo kuniletea gari isiyosajiliwa hizo IT za kwenda Zambia ambazo zinapigwa U turn, baada ya kuniletea gari nimelipa kila kitu akasema hatonikabidhi gari hadi afanye usajiri aisee ilikuwa patashika jamaa alinitumia sana watu waniangamize, aisee Victor alaaniwe sana popote alipo, gari nikatapeliwa na pesa zangu nyingi tu nikaishia kuishi maisha ya ajabu sana ila MUNGU ni mwema nilivuka hilo jaribu nikabarikiwa mara dufu. Tangia hapo sina urafiki na polisi nawachukia sana
 
Embu acha habari zako za kutunga tunga humu Kuna watu wazima tuna akili zetu na tunajua Kila kitu hivi unafikiri ni rahisi hivyo kugusa mwili wa ocd jaribu kama haujachakaa sura eti Zanzibar unaizungymiza Zanzibar ipi hiyo ni hii hii ninayokaa Mimi ya tanzania au ipi
 
CCM na TanPol ni mapacha, ndiyo maana wewe unawakubali.
Mwezi mchanga umekaribia nini? 1/4 ya rafiki zangu ni askari polisi, tunakunywa nao pombe tunafurahi pamoja ispokuwa endapo unavinasaba vya uizi polisi utawaona sumu kali.
 
hamna ndugu mimi ndugu yangu wa damu akiwa polisi mimi na yeye hatuivani kabisa labda mwanajeshi ila sio polisi
Nashukuru Mungu ndugu yangu aliyekuwa amebaki peke yake polisi amemaliza shahada yake ya sheria na amefaulu shule ya sheria na kwa sasa ni wakili anayezunguka kwenye vituo vya polisi na mahabusu kutafuta watu wa kuwasaidia.

Kilichomvuta kusoma sheria ni huo ukatili wa polisi aliokutana nao miaka 12 yake ya kutumikia TanPol.
 
Kuna mgeni toka nchi za magharibi...alisema polisi ya Tanzania kuna haja ya ku I reform...shida inaanzia CCP.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…