Kataa kabisa urafiki au mahusiano ya kawaida na Askari Polisi

Askari na jambazi ni watu sawa wenye mwelekeo tofauti.

Uelekeo wake utategemeana na muda(usiku au mchana) au amekutana na wewe mazingira gani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Sasa Mzee unawakataaje ndugu zako ambao ni askari
 
Mzee pole kwa yaliyokukuta. Ila mi nakushaur katika life jitahid kila engo una mtu. Police,uhamiaji,jeshin, advocate, Dr, maofisin,nk kila eneo. Ni muhim maana hata bible imeandika Mungu ameziumba pia siku mbaya kwaajili ya wabaya. Yaan kuna eneo hupataki lakini unajikuta kwenye harakat ushafika hapo. so we cha msingi ili kurahisisha Life basi huyo rafiki awe wa ngaz flan ya maamuz ili akipiga cm moja huko chini mambo yanajiseti yenyewe. Wabongo pia tunatikiwa kujua hakuna kitu cha bure dunian. Ukiona nchi kuna aman ujue kuna watu wako mahali either wamekesha kwaajili yako au wanaua watu kwaajili yako ndio unauona huu utulivu. So mi askari kuna wakati nawaelewa na sio askari tu hata usalama jeshi nk. Kudeal na mwanadamu ambao katikat yao kuna wezi vibaka magaid wasomi wajinga nk. Sio ishu ndogo. Ukitaka kujua ugumu wa hiyo kaz nenda kituo cha polisi ukae nao watu waanze kuleta kesi zao pale ni shida tupu. So siwaungi mkono kwenye ushenz ila nakupa angalizo tu. Banian ni mbaya ila kiatu chake ni dawa.
 
Kuna demu mmoja mjeda (police) kanizimikia balaa, unataka kuniambiaje weye.!! alinikamata kosa la barabarani kutoka hapo yaani nataka kuoa kabisa kabisa maana si kwa mambo yale aisee !!
..uoe polisi..? nakutakia safari njema ya kuelekea kwenye matatizo lukuki mpaka utamani bora kufa
 
Polisi hawezi kutoka kwenye kituo chake cha kazi akaja kumfuata raia bila sababu. Binadamu ndiye kiumbe hatari na kamwe usimwamini.
acha ujinga we polisi.. hii mnafanya mara nyingi tu
 
Uko sahihi lakini utekelezaji wa majukumu yao umegubikwa na matukio mengi ya uonevu na mauji, cha msingi polisi mweke mbali katika cycle yako ya maisha, kutana nae pale inapojitajika kufanya hivyo, baada ya hapo jikatae, hawafai
sahihi
 
mkuu kumpenda police wa kike.. labda wanawake wote duniani waishe abaki yeye tu! akishavaa zile gwanda anakuwa na kiburi na dharau kwa kiwango cha juu kbs!
 
Mwezi mchanga umekaribia nini? 1/4 ya rafiki zangu ni askari polisi, tunakunywa nao pombe tunafurahi pamoja ispokuwa endapo unavinasaba vya uizi polisi utawaona sumu kali.
..we endelea nao tu si hauna vinasaba vya wizi? siku moja utaleta mrejesho hapa
 
mjinga huyo hayajamkuta.. polisi tz sio watu wa kuwa nao karibu
 
Polisi wa vyeo vya chini wengi wanazengua ila wakubwa wao hawana shida kivile.

Kuanzia nyota tatu kupanda juu ni nadra sana kukuta wenye tabia ambazo sio za kiproffessional.
hakuna polisi mwenye nafuu... walio muuwa mfanyabiashara wa madini na kumfukia karibu na kiwanda cha dangote ni wa vyeo vya chini? we vp
 
tafuta hela mkuu.. ukiwa na hela hao woote watakuwa karibu na wewe Ila ukaribu na polisi no!
 
Polisi wa vyeo vya chini wengi wanazengua ila wakubwa wao hawana shida kivile.

Kuanzia nyota tatu kupanda juu ni nadra sana kukuta wenye tabia ambazo sio za kiproffessional.

Senioue Officers wengi hawana hizo tabia sababu ya aina ya majukumu waliyonayo, hawakutani na mara kwa mara na watu halaf ukishafika levels hizo mentality unabadilika
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…