Wewe muite hata Billgates lakini kama huna Mipango haisadii chochote.
Babu yangu alikuwa tajiri sana wa enzi zao, na utajiri wake mkubwa ni mifugo, ilikuwa kila mwanaukoo anayetaka kuowa basi mahari anakwenda kuchukuwa kwa babu yangu yani Ng'ombe.
Sasa basi kwa imani utajiri ujirudia unakuta familia moja baba anawapa majina mpaka Watoto watatu jina moja la yule Babu yangu kwa imani yao kwamba kwenye ukoo lazima kutatokea mtu mwenye jina lake na atakuwa tajiri mkubwa kama Babu.
Basi ukija kijijini kwetu utacheka ukiuliza unamtafuta Fulani ni lazima useme mtoto wa Fulani na bado ndani ya familia hilo jina wanatumia Watoto watatu, imebidi vijana wenyewe wa kisasa lile jina wakalichakachuwa sasa hivi kila mtu ana utambulisho wake kwa jina hilohilo kama vile Mohammed, Muddy na Mo.