Kataa katakata mkeo kutoa jina la mtoto wenu wa kiume

Kataa katakata mkeo kutoa jina la mtoto wenu wa kiume

Sio kila kitu usubiri kufundishwa mkuu, changamka. Yaani hata Kama mna watoto 100 wa kiume, majina yote yatolewe na baba. Sio mbaya mara mojamoja hapa na pale mke kutoa majina kwa watoto wa kike.

Nimeona mara kadhaa ugomvi wa kuvunja ndoa baada ya Kina baba kugundua asili ya majina ya watoto wao wa kiume waliopewa na mama zao.

Chukua tahadhari.

Hii mkuu inabadilisha nini? Maana ukute hata mtoto sio wako.....
wakati mwengine ni kuacha maisha yaendelee!!! Na tunawapa fursa kutoa jina kwasababu moja tu....
kuingia kule ndani yani (leba)nakutoka salama yeye na mtoto inatosha yeye kutoa jina kama itakupendeza lakini sio sheria kwamba lazima tutoe majina mkuu!!!

Tunatoa majina na watoto sio wetu ni ujuha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aaaah wapi..... from nowhere aanze tu kukusumbua ?.... Kuna namna hapo..😂😂😂
Kuna mazingira flan unaweza kuwa nayo kwa wakati flan yakawafanya watu kutamani kukupata?
 
Kuna jina moja la kiume nilipanga miaka mingi nitakapopata mtoto akiwa wa kiume lazima nimpe hilo jina.
Daah nilipompata mama chanja wangu nikagundua hilo ni jina la X wake.
Ndoto zangu za kumpa hilo jina mtoto wangu zikafa kifo cha mende.
Yaani mtoto akilia ambembeleze "nyamaza Michael wangu nakupenda sana " WTF?
 
Wanawake ni watu wa hisia sanaa…ukiwapa fursa ya kutoa majina utashangaa mtoto anaitwa Othiman Bey,ata haya majina ya ajabu sijui chausiku,chawote,cheupe,J4….ukute kapata shida kwenye kubeba mimba,mtoto akizaliwa anamwita shida…ahahaa

Naunga mkono hoja…
 
Kweli bana Kuna demu aliita jina la baba angu mzazi sasa siku mme akijua ataburuzwa sana
 
Mwisho wa siku watoto wanaishia kuimba nani kama Mama. Mna upuuzi kiwango cha SGR ,mtu ahangaike mimba miezi tisa uchungu juu kunyonyesha miaka miwili kisha unamnyima haki ya kutoa jina kisa your own inferiority


Nimecheka!

Mwingine anasema mke wake yeye ni kabati tu la kutunzia watoto!

Boys massaging their Egos.
 
Mnatusingizia tu. Ex wangu mwanae wa kwanza alimpa jina langu.

Mtuache tuwape watoto wetu majina, miezi tisa tuteseke then mtoe majina kweli😳😳😳😳
 
Yule dem n sngle mama mpka leo anatumia jna la mwsho la mwanae la kwangu hii ktu inanyima aman sana
Nje ya mada
 
Sasa mnachokataaa nn? Wee kumpa jina la ex wako mtoto wenu wa kike ni sawa, ila mkeo kumpa jina la ex wake mtoto wenu wa kiume ni vibaya?

Unafiki na ubinafsi huu.
Basi nitazaa mmoja na wewe umuite jina la ex wako.

Tuombe tu teknolojia iruhusu wewe kubeba mimba.
 
Kuna jina moja la kiume nilipanga miaka mingi nitakapopata mtoto akiwa wa kiume lazima nimpe hilo jina.
Daah nilipompata mama chanja wangu nikagundua hilo ni jina la X wake.
Ndoto zangu za kumpa hilo jina mtoto wangu zikafa kifo cha mende.
Yaani mtoto akilia ambembeleze "nyamaza Michael wangu nakupenda sana " WTF?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ndo ulichokuwa unakiwaza wee?? Bas utakufa uko hoi
 
Mi namuulizaga mke wangu akitoka kujifungua mtoto anaitwa nani anasema flani namwambia hayaaa..
 
Back
Top Bottom