Kataa Ndoa School of Thought, ni upi mtazamo wenu juu ya Masuala haya?

muktadha wa dini huo, sio kila mtu anafuata

familia bila ndoa inawezekana sana tu
Sijui unaposema dini una maanisha dini, ila Ndoa—kwa maana ya dhana ya Mwanaume na Mwanamke kutambulika kijamii kuwa katika makubaliano ya kuishi pamoja— zimekuwepo kabla ya dini. So, Suala la Ndoa ni la Asili ya mwanadamu na lina mizizi kwenye evolution ya mwanadamu, dini zimekuja kuchagiza tu.
 
Mkuu mimi sikatai kuzaa ila nakataa ndoa hivyo basi nitazaa na nitachukua watoto wangu nawalea mimi mwenyewe na hiyo ndiyo familia yangu. Mama zao wapambane na hali zao huko sifugi mwanamke ndani kwangu
Unadhani ni mfumo sahihi kulea watoto kwa kuzaa hovyo na kuwakusanya, bila Malezi na miongozo ya Pamoja ya Wazazi? Umechukua into account masuala mengine niliyoyainisha hapo juu kuhusu Umuhimu wa familia?
 
Ivi mnapata wapi muda wa kumjibu huyu, nyie muacheni yakimkuta ataludi tu hata na ID fake atoe ushuhuda.
Mkuu, nilishapitia Changamoto za masuala haya, lakini haiondoi umuhimu wa Ndoa kwenye jamii. Hakuna mfumo usio na Changamoto, kinachopimwa ni Faida dhidi ya Changamoto.
 
Ndoa sio lazima katika maisha
 
Mbona kuna watoto wametoka kwenye stable families lakini morality yao ni mbovu sana? na ni wengi tu sio wachache

Na kuna watoto wako disciplined balaa na wamelelewa na single parents
 
Mbona kuna watoto wametoka kwenye stable families lakini morality yao ni mbovu sana? na ni wengi tu sio wachache

Na kuna watoto wako disciplined balaa na wamelelewa na single parents
Ukweli huu. Ila inategemea pia na situation ikoje. Naweza lelewa vizuri ila nikakutana na tukio ambalo likanibadili somehow nikafanya yale nisiyofunzwa
 
Nijuavyo mimi, apes wote ni polygamous species, ikiwemo binadamu
Uko sahihi, lakin being Polygamous haizuii ndoa. Na huwezi fananisha Wanyama wengine na wanadamu katika namna ya kuyaratibu Maisha. We are social beings hivyo tunahitaji social setup ya kuweza kufanya maisha yawe na ustaarabu na utaratibu.
 
sio lazima ndoa, ili watoto walelelewe

si unaona single parents na co parents?
 
Mbona kuna watoto wametoka kwenye stable families lakini morality yao ni mbovu sana? na ni wengi tu sio wachache

Na kuna watoto wako disciplined balaa na wamelelewa na single parents
Ni kweli kabisa. Lakini, muulize Single Parent yeyote, atakuambia Sio rahisi kulea mtoto bila mwenza na angetamani ampate mwenza wa kusaidiana naye malezi.
 
Jamii gani? Iliweka utaratibu upi? Ulikubalika na kina nan?
Ilikubalikaje kuwa Baba ndiye awe Kiongozi wa Familia? Kuna utaratibu upi uliweka hilo? Ulikubalika na kina nani?
 
Mbona kuna watoto wametoka kwenye stable families lakini morality yao ni mbovu sana? na ni wengi tu sio wachache
Huwezi zaa watoto wote timamu lazima wehu wawepo, lakini Stable family humbeba huyo mwehu sababu ya upendo na umoja wa kifamilia.

Lakini, wengi hapa naona wanachanganya, Family & Marriage kama ulivyo mfumo wowote, its not PERFECT, lakini it's the best we got.
 
Kwa Asili ya Mwanadamu, Single Parenting is not a Desired & Preferred system ya kijamii but ni matokeo ya kufail kwa mfumo rasmi wa Ndoa na Familia.
basi kumbe tatizo lako ndo hilo, single parenting & co parenting zinazaa matunda

you're having biased prejudices, check them with facts
 
Watoto wana haribika kisaikorojia kulelewa na mzazi mmoja. Kwahiyo hiyo sio familia ni kikundi cha wahuni
 
Nimegundua kataa ndoa wengi wamelelewa na single parent kwahiyo walisha haribiwa kisaikorojia toka wakiwa watoto ndio maana wanaona wako sahihi bila kujua uzuri wa kulelewa na wazazi wote wawili
 
Ili ndoa idumu inatakiwa nyota ziendane.
Au nyote muiweke ndoa yenu kwenye misingi ya dini yenu.
Sababu watu hawafati misingi ya dini sahihi kufuata elimu ya nyota ili ujue tabia,majina yanayowezapatana.
Huwezi ukaweka paka na chui au nyoka chumba kimoja au Simba na kondoo lazima moto uwake ndani ikiwemo talaka baada ya nyege kuisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…