Kataa ndoa tunakemea ufungaji wa ndoa, kipindi hiki kikali cha talaka na mgawanyo wa mali

Kama unawaza talaka badala ya kuishi pamoja hadi kifo kiwatenganishe basi utakuwa una bahati mbaya kwenye selection yako

Vijana mkubali wazee wenu tuwachagulie wake wa kuoa na waume wa kuolewa nao, kwani tunakuwa tumeshafanya screening ya kutosha kumhusu huyo mke/mume mtarajiwa

Nyie kama mtaoa kwa kuangalia ukubwa wa Nyashi lazima mdaiane talaka baada ya miezi 6 ya ndoa

Au Mdada kukubali kuolewa kisa amekutana na kijana ananukia harufu nzuri ya perfume ama ana kifua kizuri kilichojengwa gym lazima baada ya mwaka mmoja wa ndoa arudi kudai talaka
 
Nawaomba tu hawa vijana wangu, hii movement ya kataa ndoa isije kuleta mambo mengine. Unakataa ndoa then what, unaishije, mwenyewe? Sogea tuishi? Unazalisha tu? Au unataka kuishije!!

Tusije kuzalisha mambo ya ajabu kwenye jamii, tusije kufikia kwenye ushoga tu jamani, ni tahadhari tu!!
 
Sogea tuishi, zalisha kisha hudumia iko fresh, au ndoa za pre nuptial agreement ziko bomba.
 
Ndoa kilio nenda waulize wenzio, ikikukaba husiki au kutaka lolote๐Ÿ˜…
 
anaekataa ndoa ndio anadhani ndoa ni mbaya gentleman,kumbe sivyo,
na akiona ndoa moja tu ya walioigiza wakati wanaona ikisambaratika, anadhani ni ndoa zote ziko hivyo,

hayo ni mawazo potofu, na ya kimaskini sana kuishi kwa kudhani gentleman,

ndoa nyingi zilizo kwenye masuluhisho ya kisheria hazikua ndoa halisi bali maigizo ama drama za kuonekana umeoa au kuolewa.

waliosema ndoa si lelemama hawakukosea gentleman.
na sheria ziko, na zitaendelea kuwepo dhidi ya hao wanaofanya ndoa za maigizo. hakuna namna nyingine hapa.
lazima pawepo ustahimilivu na subra kwenye ndoa la sivyo mgawane mali kadiri mlivyozichua na muachane kwa amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ