Kataa ndoa vs kubali ndoa (online poll)

Kataa ndoa vs kubali ndoa (online poll)

UNAUNGA MKONO VIJANA WAENDELEE KUOA?


  • Total voters
    140

Dr Count Capone

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Posts
1,878
Reaction score
3,263
13DA4598-987E-486B-AE52-3D3119691771.jpeg

Ashakutakia Happy Valentine? Kama bado Mambo yasiwe mengi, shikilia hapo hapo!

Waungwana kwa muda tumeona nyuzi baada ya nyuzi akina Liverpool VPN dronedrake na wenzao wakipiga kampeni kali kabisa kukataa ndoa huku wakitoa mifano ya visa vya kweli

Na mzee wa busara Mshana Jr na wengine tukikubali changamoto za ndoa na kuendelea kuhamasisha vijana waoe wasikimbie majukumu yao.

Sasa kutokana na kuwepo kwa maoni mseto humu ndani ni wakati sasa tupige kura ili tujue msimamo wa jumla wa wanachama wengi hapa JF kuhusu taasisi nyeti ya ndoa.

Bonyeza NDIYO ✅ kuunga mkono Ndoa
Bonyeza HAPANA ❌ kukataa ndoa

NB: Mods tafadhali sana msifute huu uzi
Hauendi kinyume na sera za JF!🙏
B337BDB4-1AD8-4E97-B456-6169A1D8CDD5.jpeg
BE38FB9E-CFA0-4492-96D1-E2645F20BE1E.jpeg



UPDATES

Mkuu Count Capone nna jambo la kushare kulingana na mfumo tulionao na tunaendelea kuishi nao.

Kwa wenye imani dini hasa ya kikirisito wanajua kuwa NDOA ni jambo jema na nimipango ya mola kufanya iwe hivyo.

Baada ya uumbaji mzee Adam alipewa jiko (bihawa) na kumwambia enendeni mkaitunze dunia na kuzaa pia huku mkiwa na Upendo kati yenu.

Baada ya hapo hadi leo kumekuwa na mparaganyiko, vikao vya kimataifa ikazaliwa (Beijing women conference) ikaja na agenda motomoto ambazo leo zinataka 50/50 na hiyo fifty-fifty imezaa wajukuu wanaolelewa kwa kuambiwa wanawake tunaweza tukiwezeshwa bila chenga.

Leo kitukuu kina nguvu na uwezo kinaamua sitaki kuishi na mke/mume hata mimi naweza kujimudu, isipokuwa Mwanamme hawezi kubeba mimba ila huyu wa 50/50 anaweza kubeba tena siyo lazima mimba iwe na baba.

Kwa nini NDIYO au HAPANA kwa Ndoa, matatizo yaliyopo ndani ya Ndoa yanapelekea vijana wengi hasa sa kike kuichukia ikiwemo uvumilivu na kusamehe, vifo na majanga yatokanayo na ndoa imewafanya wengi kuepa kuoa na kuolewa, taasisi za gizani, hidden societies zinazosimamiwa na NGO's zinasimama kuharibu mahusiano mazuri yaonekane ni ya ovyo.

Baadhi, ndugu, taasisi na wazazi nao wanasimama kuharibu mahusiano ya wanandoa, wanasahau NDOA ni one the biggest Institution inayoweza kuharibu na kuijenga dunia.”
- TODAYS
 
Duu issue ya
kataa ndoa-
jali afya ya akili.
Ndoa ni wizi
Ndoa ni utapeli.
Ndoa ni mzigo
Ndoa ni chanzo cha magonjwa na kukosa amani

Kubali ndoa
Ndoa baraka.
Ndoa ni uwekezaji wa uzeeni
Ndoa ni msingi wa maisha bora ya jamii
Ndoa ni heshima
Ndoa ni msaada wakati wa shida na uzee

PIga kura tuone lipi la msingi. Muhimu userious kwenye votes
 
Back
Top Bottom