Katambi avunja ngome ya Upinzani Ushetu amwombea kura mgombea wa CCM Comred Emmanuel Peter Cherehani

Katambi avunja ngome ya Upinzani Ushetu amwombea kura mgombea wa CCM Comred Emmanuel Peter Cherehani

Katambi avunja gome ya Upinzani Ushetu " Tunahamia CCM hatuwezi kubaki kwenye chama kinachosusia kila Uchaguzi " Je Nani ni Nani leo kati ya ACT-Wazalendo na CCM-Tanzania​

"Tutampa Rais Samia ushindi mnono kama shukrani yetu kwake -wapigakura "​


Katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Hayati Elias John Kuandikwa alishinda kwa Ushindi mwembamba baada ya kupata 56% ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake wa karibu Bw Isaya Simon Bukakiye akiambulia 44% ya kura zote,Jimbo na Ushetu liliitesa sana CCM kwa kipindi kirefu hatimaye leo Katambi na viongozi wengine akiwemo Shaka Hamdu Shaka Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi,Crde Kenani Kihongosi Katibu Mkuu wa UVCCM-Taifa,Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati kuu Mizengo Kayanza Peter Pinda,Mbunge wa Viti Maalum Mariam Ditopile (Dogo Janja ),Iddy Khassim Mbunge wa Msalaa na Hussein Bashe Mbunge wa Nzega Mjini na Viongozi wengine wa Jimbo, Wilaya na Mkoa wameuzika rasmi Upinzani Ushetu hakika ni habari mbaya sana hii kona za Ufipa,

Patrobas Katambi mwanasiasa kijana machachari na mchamungu anayezifahamu vema siasa za kanda ya ziwa ( Usukumani) lakini pia ni kiongozi anayeufahamu Upinzani nje ndani amekuwa mwiba mkali hasa kwa Chadema-Tanzania na kuifanya CCM kuwa na mtu hatari zaidi kwa Upinzani kanda ya Ziwa na hapa Chadema lazima mkubali ukweli mchungu mmepoteza kijana kiungo namtakumbuka niyeye kuhamia kwake CCM kuliwarudisha wengine wengi CCM hili sote tunalifahamu,

Akitumia lugha ya kisukuma katika kumwombea kura ya ndiyo Mgombe wa CCM Ndg Emmanuel Peter Cherehani kwa wakazi wa jimbo la Ushetu Patrobas Katambi amedhihirisha unguli wake wa siasa kwa kuzoa mamia ya wanachama wa Upinzani jimboni humo waliolalamikia Chama chao kususia kila Uchaguzi huku wakishindwa kususia Uchaguzi Mkuu,

Katika Uchaguzi huu mdogo wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Hayati Elias John Kuandikwa utakaofanyika trh 09|10|2021 Upinzani mkali ni Kati ya Mgombea wa ACT-Wazakendo Ndg Julius Nkwabi Mabula na Mgombea wa CCM Ndg Emmanuel Peter Cherehani Mkt Mstaafu wa Chama kikuu cha Ushirika KACU chama kilichovunja rekodi ya kununua Pamba kwa bei ya juu tangu tupate Uhuru wa nchi hii ambayo ni Tshs 1,900 rekodi ambayo inambeba Cherehani kuweza kushinda katika jimbo lolote la Uchaguzi kanda ya ziwa,


#Kazi iendelee



View attachment 1968875

View attachment 1968876

View attachment 1968877

😍
 
Yaani maCCM bila kuitaja CHADEMA hayaridhiki na hayana mvuto.
CHADEMA hawashiriki huo uchaguzi, lakini CCM wako busy kuishutumu CHADEMA. Hii inatupa picha kubwa kuwa, CHADEMA ni tishio kubwa la kisiasa hapa Tz, hata kivuli chake kinatosha kuisambaratisha mapema sana CCM.
Machadema hayashiriki huu uchaguzi kwani Mbaya wao Magu bado yupo?
 
Vijana wote wenye akili walishahama Chadema tumebaki wazee tu na vijana wasiojiweza,Katambi mimi namfahamu ni mtu hatari sana kwa hoja, Sisi Chadema kila uchaguzi mbiooooooduu
hahaha hatari, achana na hao nazichadema
 
Komredi P.P.Katambi ndio kiboko ya CHADEMA....

BAK ,Mmawia na ERYTHROCYTE wakimuona huyo jamaa wanatimua mbio balaa.....wanaishiwa hoja zao zote za ubishi.....🤣🤣
 
Niko sawa kabisaa. Hao Chadema watasimamishaje mgombea wakati wanaogopa?
Kwani hoja ya kutokusimamamisha uliielewa Mkuu?
Nani anasimamia uchaguzi?,

Refa au wa kwenu, mnataka wake mashindanoni na MUAMUZI Ni wa kwenu.
Ndio maana Wanadai Time huru. Ili kuendelea kuwa relevant na madai hayo, wameamua kutogombea ambapo bado sio Lisa.
Kwenye kpeni Sasa mbona mnawataja Sana kuliko mnaogombea nao jimboni, ACT?
 
Jamani jamani, mbona chadema haipo kwenye huo uchaguzi lakini CCM mnazungumzia chadema badala ya mnayepambana naye ACT!! Maajabu haya, uchaguzi ni ccm na Act lakini mjadala ni Chadema
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanini hawajasimamisha mgombea?
Ni kweli hujui sababu??

Wanataka Tume Huru Kwanza, mgogoro wa refa utatuliwe ndio mechi ianze. Kwa Sasa wanasema refa wa Yanga, so Sina haiingizi timu uwajani. Simple!
 
Back
Top Bottom