Katavi: Kijana ajiua baada ya Mama yake kukataa kujiunga CHADEMA

Katavi: Kijana ajiua baada ya Mama yake kukataa kujiunga CHADEMA

kijana mjinga huyo
Hapana simjinga vijana wengi wako katika hali hiyo, kumbuka alitaka kusoma uwezo ikawa mdogo, hasira zote zikuwa ccm, alikuwa na msongo wa mawazo Mama angeliongea naye taratibu sio kumpigia Kofi, alikuwa tayari ana depression. Tuna vijana wengi wamemaliza vyuo hawana ajira kama wazazi tuwaangalie kwa huruma na kuwalinda wasibezwe.
 
Huyo kijana alikuwa na matatizo ya kiakili Kama ni kweli imetokea au propaganda za kisiasa.

Kwani mama yake alipomkataria kwanini hakukaidi, ina maana yeye maamuzi yake yote katika maisha anamtegemea mama yake?
 
Tukio la kujinyonga la kijana wa CHADEMA D kutokana na tofauti za KISIASA na mama yake mzazi ambae Ni CCM

Tukio hili la Chuki za KISIASA na UHASAMA ulio pitiliza umepelekea kifo

Najaribu kujiuliza huyu mama yake mzazi atatoa machozi msibani?

Najaribu kujiuliza CCM TAIFA au CCM Mpanda watampelekea kifuta jasho Cha kumpoteza mtoto Alie mzaa yeye mwenyewe?

Mama mzazi hato mwona Tena mwanae kisa itikadi za kisiasa hili Jambo linaumiza Sana itikadi za kisiasa...

Pengine mama aliamini kua mtoto Alie mzaa mwenyew hawezi kua na itikadi tofauti na zake pengine hapo ndio kweny mzizi wa hiki tukio

Somo la political torelance litolewe kwa raia wote na tuvumiliane tupendane.

Mungu Ibariki Tanzania

======

Kijana anayefahamika kwa jina la Twaybu Omary, 22, mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa Kata ya Nsemulwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amekutwa bafuni akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia waya mweusi, huku chanzo kikidaiwa ni baada ya mama yake kukataa kuwa mfuasi wa CHADEMA.

Kitanzi

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Abdi Isango amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema siku moja kabla ya kifo cha kijana huyo kulitokea tofauti ya majibizano ya kisiasa, ambapo marehemu alikuwa ni mfuasi wa CHADEMA na alikuwa akimshawishi mama yake kuhamia chama hicho ndipo mama yake ambaye ni mfuasi wa CCM akakasirika na kumpiga kofi mwanaye.

Akimzungumzia mtoto wake huyo aliyejiua, Mama mzazi wa marehemu Mariam Shamsha, amesema mtoto wake alikuwa anapenda kusoma lakini alishindwa kumtimizia ndoto zake kutokana na kipato chake kuwa kidogo.

"Mwanangu aliniambia nijiunge na CHADEMA, mimi nikakataa nikasema siwezi kujiunga, nikamuambia mimi nina uzalendo na nchi yangu", amesimulia Mama wa marehemu.

( Via Eatv.tv)
Pathetic, ignorant mother, CCM would love this, 90% of CCM followers are like this mother, ignorant never been to school, un informed. Being loyal to CCM doesn’t mean you are loyal to the country. You can be loyal to chadema and also loyal to your country!
 
Kuna dogo mmoja alitupa shida sana kumbembeleza baada ya Lowassa kushindwa. Alilia kama kafa mtu wa karibu. Leo nikimuuliza Bw. Mamvi yuko upande gani leo, anatoa macho tu.

Huwa sipendi kutumia lugha inayofanana na matusi, ila wewe mleta mada hauko sawa.

Yaani unamlaumu Mama kwa kujinyonga huyo kijana kwa sababu hiyo hapo juu?

Labda kuwe na lingine. Haiwezekani ukamlazimisha mtu akupende wala apende unachopenda wewe. Hata Mungu aliyetuumba mwenye uwezo wote hatulazimishi kumpenda yeye. Katupa uhuru wa kuamua. Vinginevyo asingeteketeza wanadamu na kumuacha Nuhu na familia yake.

Angelazimisha tu wampende na wafanye anavyotaka yeye, lakini aliwaacha waamue maisha yao. Hata Yesu hakuja kutulazimisha kumpenda bali kutushawishi kwa kutufundisha. Akatumia hadi miujiza ili watu waaamini waamue wenyewe.

Bahati mbaya huu ugonjwa wa kulamishana mahaba ya kisiasa hata humu upo sana. Muda bado upo, endeleeni kutushawishi.
 
Huyu mama hawezi kusema ukweli halisi kuhusu hili tukio. Kuna mambo ataficha.
Mkuu mbona ukweli ushajulikana?

Mama ni kada wa CCM na alikuwa anatumikishwa sana ( [emoji738][emoji738]) na viongozi wa CCM.

Kijana hakuipenda aibu hiyo, hivyo alikuwa anatumia muda mwingi kumuonya mama bila mafanikio.

Kashindwa kuhimili kaona bora ajiondekee tuu na kumuachia mama matanuzi yake
 
Mama nae angejiua kwa sababu kijana kagoma kujiunga ccm chama alichomkuta nacho mama ake na kilichomlea huyo mtoto ingekuaje??
Unafikiri watu wa CCM ni wajinga CCM hua hatugaw bangi sis Hua tunauza Sera
 
Nani hakujui huku JF?
Naona umemaliza likizo yako bhnaa,njoo uone watu walivyonamapenzi na wagombea wao hadi tuko tayari kuutoa uhai wetu
 
Huyo kijana alikuwa na matatizo ya kiakili Kama ni kweli imetokea au propaganda za kisiasa.


Kwani mama yake alipomkataria kwanini hakukaidi, ina maana yeye maamuzi yake yote katika maisha anamtegemea mama yake.??
Kwa sababu wewe huna elimu unalo jibu rahisi kama walivyo CCM wenzi. the boy was inspired by TL the leader, Tundu is Inspirer

kijana kajiua Kwa masikitiko kuwa Kwa nini mama yake akili mgando? Ignorant
God bless his soul and rest him in peace,

the mtyr
 
Hawa ndio mashahidi wa kweli wa CDM, wafia CDM na kijana huyo atapewa hesma zote za kitaifa za CDM kwa msimamo imara na nia ya dhati ya kueneza chama kila mahali hata ikibidi kufa.
kijana mjinga huyo
Ni ngumu kuamini sababu hiyo pekee ndio iliyopelekea jamaa ajinyonge.


Let's meet at the top, cheers 🍻
Hapa hakuna sababu ya kulaum chama, familia hiyo ndo ina matatizo hasa kijana.
Duuh! Amna namna siku zake zimefika😢
Nimesikia habari kwa juu juu kwenye magazeti kuwa yupo kijana mmoja aliyejiua kisa ni mabishano ya kisasa yaliyozuka kati yake na mama yake mzazi.

Tunaomba mods au yeyote mwenye hiyo habari kwa ukamili atujuze maana hii nayo ni ya aina yake!
Tuwafundishe watoto wetu wasitumie madawa ya kulevya km hichi chama
Huyo mzee wenu ameshasuguliwa?
Chadema mashabiki wao wengi ni wanafunzi walio maliza vyuo hawana A wala Z wao wanaamin Elim zao zilikua ni pesa nyingi na wao ni matajir ila sababu ya serikal wao ni Maskin hii inawapelekea wao kuamin kua mwana siasa atawabadilishia maisha yao
Wazaz wakat huu wa kampen Mnatakiwa muwe Makin Sana na vijana wenu kwa Hali iliopo Sasa na mpaka walipo fikia inaonesha ni Jinsi Gani wamesha jikatia Tamaa

Vijana wengi wa Chadema Wana Matumain ya kwamba mwenye funguo ya Maisha yao ni Mwanasiasa na wanaamin kua ili wao wafanikiwe ni Lazima Mwanasiasa awapambanie na kitu kibaya Zaid ni pale mwana siasa anapo jitokeza hadharan na kuwa ahid kua endapo watampa uongoz ataondoa kero zao na kufanya Maisha yao Kua Mazur kitu Ambacho sio kweli

Wazaz kuwen Makin na watoto zenu hasa Wafuas wa Chadema pia jitaidim kua mnaangalia mwenenndo wa Akil zao
Pale mtapo tulia Mashaka ni Bora uripot Police

Vijana wengi wamesha Anza kuuona ukweli mpaka kufikia Hatua ya kukata Tamaa Maana Mgombea wao Amesha onesha dalili ya kushindwa
"Mwana mpumbavu, Ni kilio Cha mamaye"
Maneno ya biblia hayo sio yangu jameni.
Kibaraka wa uovu akihudumu hapa JF!
Umesoma mpaka darasa la ngapi? Unatumia simu ya aina gani?
 
Kinachosikitisha ni kuwa huyo mama ameshindwa kumsomesha mwanaye na mwanaye kwa uchungu mkubwa anaona ni kutokana na sera mbovu za CCM ameona ujinga uliokithiri kutoka kwa mama yake mzazi.

Mwanao alikuwa na ndoto ya kusoma ila kutokana na ufukara wako umeshindwa kumsomesha na bado unaunga mkono CCM. Acha kijana aondoke maana amekosa tumaini kutoka kwako ukiwa kama mzazi!
Huyo kijana ni mpumbavu sana! Anaamini Lisu ndio mwenye maisha yake kama ya MO.
 
Kwa sababu wewe huna elimu unalo jibu rahisi kama walivyo CCM wenzi. the boy was inspired by TL the leader, Tundu is Inspirer

kijana kajiua Kwa masikitiko kuwa Kwa nini mama yake akili mgando? Ignorant
God bless his soul and rest him in peace,

the mtyr
Hayo ndiyo matatizo ya akili kushindwa kudhibiti mihemuko.

Yaani mtu nijue kisa chama cha siasa???
Halafu kwani angekaidi amri/ katazo la mama yake ndiyo ingekuwa njia bora zaidi.
 
Wazaz wakat huu wa kampen Mnatakiwa muwe Makin Sana na vijana wenu kwa Hali iliopo Sasa na mpaka walipo fikia inaonesha ni Jinsi Gani wamesha jikatia Tamaa

Vijana wengi wa Chadema Wana Matumain ya kwamba mwenye funguo ya Maisha yao ni Mwanasiasa na wanaamin kua ili wao wafanikiwe ni Lazima Mwanasiasa awapambanie na kitu kibaya Zaid ni pale mwana siasa anapo jitokeza hadharan na kuwa ahid kua endapo watampa uongoz ataondoa kero zao na kufanya Maisha yao Kua Mazur kitu Ambacho sio kweli

Wazaz kuwen Makin na watoto zenu hasa Wafuas wa Chadema pia jitaidim kua mnaangalia mwenenndo wa Akil zao
Pale mtapo tulia Mashaka ni Bora uripot Police

Vijana wengi wamesha Anza kuuona ukweli mpaka kufikia Hatua ya kukata Tamaa Maana Mgombea wao Amesha onesha dalili ya kushindwa
Umeanza vizuri ila umeharibu mwisho
 
Unakuta hawa vijana wanashinda wakitukana mtandaoni huku wakidai demokrasia.

Nimesikia habari kwa juu juu kwenye magazeti kuwa yupo kijana mmoja aliyejiua kisa ni mabishano ya kisasa yaliyozuka kati yake na mama yake mzazi.

Tunaomba mods au yeyote mwenye hiyo habari kwa ukamili atujuze maana hii nayo ni ya aina yake!
 
Ninachojiuliza na kushangaa sana kwa Tume, na polisi, hivi huyu mtu anaitwa Lissu hajajenga Fryover, hajanunua ndege,hajajenga jengo lolote la kiserikali, hajazindua mradi wowote kwa mbwembwe hana kwanza hiyo nafasi, hajajenga barabara hata robo mita tu, Lakini!!Lakini!!! Jamaa anawasumbua vibaya mnoo!! Kila sehemu akienda nyomiii!! Kila anapopita haitwi Lissu bali ni Raisi!! Hii inawauma sana ccm hilo tunafahamu ila kiukweli jamaa anapendwa na raia huo ndio ukweli maana katika mikutano yake yote hakuna tisheti za bure zinazogawiwa, maana kwanza chama hakina pesa za kufanya hivyo watu wanaenda kwa miguu yao na kwa ridhaa yao sio kufatwa fatwa na kupewa tisheti na kabuku 10 kama maji kama wafanyavyo upande wa pili.Kweli mzee baba umetisha. Mwaka ni wako huu.
Kama hadi sasa bado watu wanadanganywa kwa kupewa buku 10 na kupewa fulana za bure tena za CCM na kwenda kujazana kwenye jua kwenye mikutano ya CCM wakishangaa wasanii wa muziki, basi watanzania bado hawajajitambua na hivyo CCM itaendelea kuwepo sana tu.
 
Hayo ndiyo matatizo ya akili kushindwa kudhibiti mihemuko.

Yaani mtu nijue kisa chama cha siasa???
Halafu kwani angekaidi amri/ katazo la mama yake ndiyo ingekuwa njia bora zaidi.
Wanao siyo wawe wanamuskiliza wewe tu, wasiwe watumwa wako. Let them be free! Listen to them. What they just need to do is the right thing.

Watoto ni rafiki
 
Hilo haliwezi kuwa chanzo, huyo mama lazima anajua zaidi kilimsibu kijana.
 
Back
Top Bottom