Pre GE2025 KATAVI: Wajumbe wa Mkutano mkuu CHADEMA Taifa watangaza kumuunga mkono Tundu Lissu

Pre GE2025 KATAVI: Wajumbe wa Mkutano mkuu CHADEMA Taifa watangaza kumuunga mkono Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3191984
Katika historia ya CHADEMA na katika kipindi chote cha miaka 20 ya chaguzi na uwepo wa Mbowe madarakani ni kwa mara ya kwanza Watanzania tunashuhudia Freeman Mbowe akipingwa karibu kila Kona ya Tanzània kwamba imepotesha,

Ni swala la Mbowe mwenyewe na Wafuasi wake kuamua kunyoa au kusuka ila kama ni Uchaguzi umeshakwisha 90%

Soma pia: Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

VOX POPULI, VOX DEI
Unasemaje mbubujikwa na machozi ya furaha. Lucas Mwashambwa Sisi wafuasi wa lissu tuna bubujikwa na matumaini na maono na furaha na utukufu wa Mungu baba
 
View attachment 3191984
Katika historia ya CHADEMA na katika kipindi chote cha miaka 20 ya chaguzi na uwepo wa Mbowe madarakani ni kwa mara ya kwanza Watanzania tunashuhudia Freeman Mbowe akipingwa karibu kila Kona ya Tanzània kwamba imepotesha,

Ni swala la Mbowe mwenyewe na Wafuasi wake kuamua kunyoa au kusuka ila kama ni Uchaguzi umeshakwisha 90%

Soma pia: Tundu Lissu achukua rasmi Fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA

VOX POPULI, VOX DEI
Hivi Mbowe wa kweli ameenda wapi.Maana yule wa jana aliyekuwa anahojiwa na Kikeke anapata kigugumizi kidogo,hajiamini na anatoa majibu mepesi kabisa.
Hakika Dk Slaa aliifaa sana Chadema.Sasa hivi imepaya mno.
 
Kura ndizo zitakazoamua sio matamko koko yeyote popote

Kura ni siri ya mtu

Katiba izingatiwe
 
1735979338308.png

Hii ni mikoa mipya yote imetoa matamko tusubiri mingine
  1. Njombe ✍️
  2. Songwe ✍️
  3. Katavi ✍️
 
Mwamuzi wa nyakati ni sanduku la kura
Mbona timu Lisu mnahaha sana mnataka ushindi wa mezani bila kura haipo hiyo

Subirini tu sanduku la kura

Heshimuni katiba na demokrasia ya kura
Miaka ishirini madarakani bado unahitaji uchaguliwe kwenye Sanduku la Kura?
 
Back
Top Bottom