Si mpenzi wa mpira wala vipindi vinavyofanania mpira, n.k., labda wajukuu wake, lakini siweki kwa ajili yao ila bibi yao.
Mlengwa anapendelea vipindi vya kwaya na mahubiri ya Kiswahili na "movies" zenye maudhui ya Kiafrika, hasa ya Kitanzania, lakini zinazozingatia maadili .
Nilishajaribu ZUKU lakini hawajakidhi vigezo. Ninataka nichukue mojawapo kati ya AZAM na STAR TIMES. Ni ipi kati ya hizo mbili ina vipindi vingi vinavyohitajiwa na mlengwa?
Kumbuka, kipaumbele ni GOSPEL SONGS, MAHUBIRI YA KISWAHILI na MOVIES za Kiafrika, lakini hasa hasa, za Kitanzania, kwa ajili ya urahisi wa kuzielewa (za lugha ya Kiswahili). King'amuzi ipi itakayomfaa?
Nashukuru🙏🙏🙏