Kati ya AZAM na STAR TIMES, ipi itakayowafaa wazee wangu kijijini?

Kati ya AZAM na STAR TIMES, ipi itakayowafaa wazee wangu kijijini?

Kama unapesa ya kulipia kila mwezi Azam ni kizuri
Lakini kama huna Pesa ya kulipia kila mwezi basi Startime ndio kizuri Kwa sababu ndio king'amuzi Chenye Chanel nyingi nzuri za Bure.

Kam utakuwa na uwezo zaidi nunua vyote viwili kwani havizidi laki tatu
🙏🙏🙏
 
Japo ninatumia Azam ila hamna cha maana ukitoa issue za mpira unalipa kifurushi cha 25k huoni channels za maana zaidi ya michaneli sijui ya zimbabwe na Uganda haina hata program nzuri unaishia tu kuzima kama siyo mfuatiliaji wa mpira Azam ni upuuzi tu
 
Mimi ni mfuatiliaji wa Azam two/osman, simba yule

Mpira wa bongo siasa nyingi

Ushauri kwa azam wapunguze gharama za vifurushi
 
Kwahiyo startimes wana kipi cha maana? Ukisema Azam ukitoa ligi ya bongo hawana cha maana inaonekana hujawahi hata kumiliki azam TV, kwa wapenzi wa mpira Azam inaonyesha ligi kibao NBC ya ndani, bundesliga,league 1, mechi 1 ya epl kila jumamosi, inaonyesha Saudi Pl ligi ambayo wapo kina Ronaldo,Neymar, sadio mane,benzema, kwa wapenzi wa movies zipo channel kibao, wapenzi dini zipo channel za dini tofauti, Kwa Tz azam ndo king'amuzi standard ambacho ukiwa nacho unaburudika.

Ukimiliki hiyo startimes unaona nini cha maana?
Hayo yote kasoro ligi ya bongo na ligi ya ufaransa viko star times.
 
Ukisema mbali na ligi ya bongo hawana cha maana inaonyesha hujawahi kutumia azam TV au labda ni chuki, azam anaonyesha ligi kibao, Epl mechi 1 kila wiki, anaonyesha bundesliga ya german mechi zote, League 1 ya france mechi zote, ligi ya ndani mechi zote, Saudi PL unamuona Ronaldo,mane,benzema,neymar kila wiki, bado kwa wapenzi wa boxing utaona vitasa kwenye movies zipo channel kibao, news channel kibao.

Hiyo startimes inakipi kipya cha kushindana na azam hapa ndani?
Azam haoneshi mechi zote za bundesliga. Ana bagua mechi hasa zile zinazo cheza muda wa jioni saa 10:30. Ana chukua mechi moja ndo ana onesha,kikubwa ni kuwa wana tangaza Kwa kiswahili lakini haoneshi mechi zote.kitu ambacho ni tofauti na Star times ambako mechi zikiwa nne Zina onenyeshwa zote. Ni chaguo lako tu uangalie ipi.

Kuhusu ligi ya ufaransa nayo anachukua mechi moja tu anayo itaka ndo anaonesha na siyo kwamba kila mechi ya ligi ya ufaransa ikiwepo anaonesha,Kuna siku siku nyingine Azam hawarushi mechi ingali muda huo Kuna mechi ligi ya ufaransa.

Kuhusu EPL hata Star times kila jumamosi wanachukua mechi moja na wana onesha.

Hiyo ligi ya Saudi Arabia hata Star times ipo.

Hujajumlisha La Liga.

Kuhusu CAF champions league Azam anaonesha lakini ana chagua mechi anayo itaka yeye hasa zikicheza timu za bongo mbali na hapo huoni mechi nyingine tofauti na Star times.

Azam watumiaji wanaongezeka Kwa sababu watu wanakigeuza kinga'amuzi kuwa Cha biashara Kwa sababu ya KINA MANDONGA ligi ya bongo na CAF champions league. Ambako ikitokea timu za bongo zikaondolewa kwenye mashindano hayo, CAF champions league haioneshwi tena Azam[emoji16].
 
Nikuambie tu ukweli Mkuu,

Wewe ni Mkristo bila shaka. Chukua StarTimes.

Azam imejaza Channel nyingi zenye maudhui ya Kiislamu. Hata movie nyingi zina lengo haswa la kueneza Uislamu.

Ambacho Azam wanakimudu vizuri ni mambo ya Soka la Bongo tu.

Startimes wana Channel za kila aina.
Wana Upendo TV, muda mwingi ni Injili na nyimbo za kuabudu na sifa. Channel za Kikristo zipo nyingi mno.

Kama mpira si sehemu ya wanachopenda wazee, opt for Startimes. Bei chee, mzigo mwingi.
Star Times 17,000 lakini Channels kibao wameondoa ikiwemo Clouds TV na Wasafi tv

Michosho tu
 
Kama unapesa ya kulipia kila mwezi Azam ni kizuri
Lakini kama huna Pesa ya kulipia kila mwezi basi Startime ndio kizuri Kwa sababu ndio king'amuzi Chenye Chanel nyingi nzuri za Bure.

Kam utakuwa na uwezo zaidi nunua vyote viwili kwani havizidi laki tatu
Chanel gani nzuri za bure kwenye statimes??
 
Hiyo wasafi,TvE, lazima ulipie,,,,,lkn clouds na wadogo zake ITV zipo.
Nimelipa kifurushi cha Mambo sh 17,000 lakini hakina channels za awali zaidi ya 10 Clouds TV, Wasafi Tv, Zile za kuhindi zote nk

Kikiisha kifurushi hiki nahamia Azan au DStv
 
Nikuambie tu ukweli Mkuu,

Wewe ni Mkristo bila shaka. Chukua StarTimes.

Azam imejaza Channel nyingi zenye maudhui ya Kiislamu. Hata movie nyingi zina lengo haswa la kueneza Uislamu.

Ambacho Azam wanakimudu vizuri ni mambo ya Soka la Bongo tu.

Startimes wana Channel za kila aina.
Wana Upendo TV, muda mwingi ni Injili na nyimbo za kuabudu na sifa. Channel za Kikristo zipo nyingi mno.

Kama mpira si sehemu ya wanachopenda wazee, opt for Startimes. Bei chee, mzigo mwingi.
Kwenye channel za dini mnyonge mnyongeni ila Azam ana channel nyingi sana za kikristo kuanzia Upendo TV hadi ile ya mwamposa
 
Nimesoma maoni yote mpaka hapa, nimefanya upembuzi wa maoni hayo kwa vigezo vya muhimu.

Hivyo kwa mamlaka niliyopewa kwa kuzingatia ibara ya 6(2) na kifungu kidogo cha (6) huku pamoja na vigezo vingine muhimu kigezo cha uchumi kikipewa uzito unaostahili, natangaza king'amuzi kinachofaa kwa mtiririko wa namba kama ifuatavyo.
1. AZAM
2. STARTIMES
3. DSTV

NB: Kama hukubaliani na matokeo haya, kata rufaa ndani ya masaa 6 tangu matokeo haya kutangazwa.

MENGINEYO:
Tutafute hela, king'amuzi ni DSTV.
 
🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom