Kati ya AZAM na STAR TIMES, ipi itakayowafaa wazee wangu kijijini?

Kati ya AZAM na STAR TIMES, ipi itakayowafaa wazee wangu kijijini?

Nikuambie tu ukweli Mkuu,

Wewe ni Mkristo bila shaka. Chukua StarTimes.

Azam imejaza Channel nyingi zenye maudhui ya Kiislamu. Hata movie nyingi zina lengo haswa la kueneza Uislamu.

Ambacho Azam wanakimudu vizuri ni mambo ya Soka la Bongo tu.

Startimes wana Channel za kila aina.
Wana Upendo TV, muda mwingi ni Injili na nyimbo za kuabudu na sifa. Channel za Kikristo zipo nyingi mno.

Kama mpira si sehemu ya wanachopenda wazee, opt for Startimes. Bei chee, mzigo mwingi.
Ona hili cchizzi na chuki zake_!!
 
Mimi sijawahi kuona Azam Tv wakitaja neno Xmass wala Pasaka! Kimsingi wako biased kwenye mambo ya dini, hata hizo channel chache za kikristo wanalazimika tu kuziweka kwa shingo upande. Mimi Azam TV nilikuwa nayo nimeiacha kwa sababu ni mpira wa bongo tu ninaofaidika nao ambao sasa ivi niko DSTV naenjoy mipira
Wambie Tec wafungue TV yao
 
Azam haoneshi mechi zote za bundesliga. Ana bagua mechi hasa zile zinazo cheza muda wa jioni saa 10:30. Ana chukua mechi moja ndo ana onesha,kikubwa ni kuwa wana tangaza Kwa kiswahili lakini haoneshi mechi zote.kitu ambacho ni tofauti na Star times ambako mechi zikiwa nne Zina onenyeshwa zote. Ni chaguo lako tu uangalie ipi.

Kuhusu ligi ya ufaransa nayo anachukua mechi moja tu anayo itaka ndo anaonesha na siyo kwamba kila mechi ya ligi ya ufaransa ikiwepo anaonesha,Kuna siku siku nyingine Azam hawarushi mechi ingali muda huo Kuna mechi ligi ya ufaransa.

Kuhusu EPL hata Star times kila jumamosi wanachukua mechi moja na wana onesha.

Hiyo ligi ya Saudi Arabia hata Star times ipo.

Hujajumlisha La Liga.

Kuhusu CAF champions league Azam anaonesha lakini ana chagua mechi anayo itaka yeye hasa zikicheza timu za bongo mbali na hapo huoni mechi nyingine tofauti na Star times.

Azam watumiaji wanaongezeka Kwa sababu watu wanakigeuza kinga'amuzi kuwa Cha biashara Kwa sababu ya KINA MANDONGA ligi ya bongo na CAF champions league. Ambako ikitokea timu za bongo zikaondolewa kwenye mashindano hayo, CAF champions league haioneshwi tena Azam[emoji16].
Mpaka hapo Bora Star times
 
Mkuu, Star Times ndiyo inayoongoza kwa kuwa na watumiaji wengi, ikifuatiwa na AZAM. Wapo, na wanaendelea kuongezeka.
Unajidangaya,watu wengi wameachana na startimes wamenunua Azam,hizo takwimu ni za zamani kabla Azam haijaja.Kwa hiyo watu wengi Wala hawavilipiii hivyo ving'amuzi vya Startimes vimekaa kama mapambo nikiwemo mimi
 
Unajidangaya,watu wengi wameachana na startimes wamenunua Azam,hizo takwimu ni za zamani kabla Azam haijaja.Kwa hiyo watu wengi Wala hawavilipiii hivyo ving'amuzi vya Startimes vimekaa kama mapambo nikiwemo mimi
Punguza siasa, tembelea takwumu za TCRA
 
Wakuu, nawashukuruni sana kwa ushauri wenu! Niliufanyia kazi.

Siku chache baada ya kuupandisha huu uzi, nilimfungia dishi la AZAM, na hakika, anaenjoy.

Mniwie radhi kwa kutokuuleta mrejesho mapema.

Asanteni sana🙏🙏🙏
 
Si mpenzi wa mpira wala vipindi vinavyofanania mpira, n.k., labda wajukuu wake, lakini siweki kwa ajili yao ila bibi yao.

Mlengwa anapendelea vipindi vya kwaya na mahubiri ya Kiswahili na "movies" zenye maudhui ya Kiafrika, hasa ya Kitanzania, lakini zinazozingatia maadili .

Nilishajaribu ZUKU lakini hawajakidhi vigezo. Ninataka nichukue mojawapo kati ya AZAM na STAR TIMES. Ni ipi kati ya hizo mbili ina vipindi vingi vinavyohitajiwa na mlengwa?

Kumbuka, kipaumbele ni GOSPEL SONGS, MAHUBIRI YA KISWAHILI na MOVIES za Kiafrika, lakini hasa hasa, za Kitanzania, kwa ajili ya urahisi wa kuzielewa (za lugha ya Kiswahili). King'amuzi ipi itakayomfaa?

Nashukuru🙏🙏🙏
Nawashukuruni kwa ushauri wenu! Nilihitaji kwa ajili ya mama yangu mzazi. Nilimchukulia AZAM, na ameifurahia. Amekiri kuwa ni nzuri.
 
Nimesoma maoni yote mpaka hapa, nimefanya upembuzi wa maoni hayo kwa vigezo vya muhimu.

Hivyo kwa mamlaka niliyopewa kwa kuzingatia ibara ya 6(2) na kifungu kidogo cha (6) huku pamoja na vigezo vingine muhimu kigezo cha uchumi kikipewa uzito unaostahili, natangaza king'amuzi kinachofaa kwa mtiririko wa namba kama ifuatavyo.


NB: Kama hukubaliani na matokeo haya, kata rufaa ndani ya masaa 6 tangu matokeo haya kutangazwa.

MENGINEYO:
Tutafute hela, king'amuzi ni DSTV.
Watu tunatumia Internet TV za Fiber , nyie bado mnahaha na madecoder ?
 
Back
Top Bottom