Kati ya AZAM na STAR TIMES, ipi itakayowafaa wazee wangu kijijini?

🙏🙏🙏
 
Japo ninatumia Azam ila hamna cha maana ukitoa issue za mpira unalipa kifurushi cha 25k huoni channels za maana zaidi ya michaneli sijui ya zimbabwe na Uganda haina hata program nzuri unaishia tu kuzima kama siyo mfuatiliaji wa mpira Azam ni upuuzi tu
 

Mimi ni mfuatiliaji wa Azam two/osman, simba yule

Mpira wa bongo siasa nyingi

Ushauri kwa azam wapunguze gharama za vifurushi
 
Hayo yote kasoro ligi ya bongo na ligi ya ufaransa viko star times.
 
Azam haoneshi mechi zote za bundesliga. Ana bagua mechi hasa zile zinazo cheza muda wa jioni saa 10:30. Ana chukua mechi moja ndo ana onesha,kikubwa ni kuwa wana tangaza Kwa kiswahili lakini haoneshi mechi zote.kitu ambacho ni tofauti na Star times ambako mechi zikiwa nne Zina onenyeshwa zote. Ni chaguo lako tu uangalie ipi.

Kuhusu ligi ya ufaransa nayo anachukua mechi moja tu anayo itaka ndo anaonesha na siyo kwamba kila mechi ya ligi ya ufaransa ikiwepo anaonesha,Kuna siku siku nyingine Azam hawarushi mechi ingali muda huo Kuna mechi ligi ya ufaransa.

Kuhusu EPL hata Star times kila jumamosi wanachukua mechi moja na wana onesha.

Hiyo ligi ya Saudi Arabia hata Star times ipo.

Hujajumlisha La Liga.

Kuhusu CAF champions league Azam anaonesha lakini ana chagua mechi anayo itaka yeye hasa zikicheza timu za bongo mbali na hapo huoni mechi nyingine tofauti na Star times.

Azam watumiaji wanaongezeka Kwa sababu watu wanakigeuza kinga'amuzi kuwa Cha biashara Kwa sababu ya KINA MANDONGA ligi ya bongo na CAF champions league. Ambako ikitokea timu za bongo zikaondolewa kwenye mashindano hayo, CAF champions league haioneshwi tena Azam[emoji16].
 
Star Times 17,000 lakini Channels kibao wameondoa ikiwemo Clouds TV na Wasafi tv

Michosho tu
 
Chanel gani nzuri za bure kwenye statimes??
 
Hiyo wasafi,TvE, lazima ulipie,,,,,lkn clouds na wadogo zake ITV zipo.
Nimelipa kifurushi cha Mambo sh 17,000 lakini hakina channels za awali zaidi ya 10 Clouds TV, Wasafi Tv, Zile za kuhindi zote nk

Kikiisha kifurushi hiki nahamia Azan au DStv
 
Kwenye channel za dini mnyonge mnyongeni ila Azam ana channel nyingi sana za kikristo kuanzia Upendo TV hadi ile ya mwamposa
 
Nimelipa kifurushi cha Mambo sh 17,000 lakini hakina channels za awali zaidi ya 10 Clouds TV, Wasafi Tv, Zile za kuhindi zote nk

Kikiisha kifurushi hiki nahamia Azan au DStv
Mie nalipiaga 18, 000
 
Nimesoma maoni yote mpaka hapa, nimefanya upembuzi wa maoni hayo kwa vigezo vya muhimu.

Hivyo kwa mamlaka niliyopewa kwa kuzingatia ibara ya 6(2) na kifungu kidogo cha (6) huku pamoja na vigezo vingine muhimu kigezo cha uchumi kikipewa uzito unaostahili, natangaza king'amuzi kinachofaa kwa mtiririko wa namba kama ifuatavyo.
1. AZAM
2. STARTIMES
3. DSTV

NB: Kama hukubaliani na matokeo haya, kata rufaa ndani ya masaa 6 tangu matokeo haya kutangazwa.

MENGINEYO:
Tutafute hela, king'amuzi ni DSTV.
 
🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…