Kati ya baba na mama ni yupi mmiliki halali wa mtoto?

Kati ya baba na mama ni yupi mmiliki halali wa mtoto?

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,469
Natumai mmeamka salama wanajamvi.

Wakuu hili jambo la nani ni mmiliki halali wa mtoto kati ya baba na mama limekua likinitatiza sana hata nikaona vema kushare nanyi ili tulijadili kwa marefu na mapana...

Kwa mtizamo ulozoeleka tunajua baba ndo mmiliki wa mtoto but utata wangu huja kwa kujiuliza ikiwa fertilization hufanyika kwa kukutana yai la mwanamke na mbegu ya kiume, why mwanaume ndo awe mmiliki wa mtoto na si mwanamke ambae hu-play part kubwa katika process ya upatikanaji wa mtoto?

Karibuni tujadili kwa facts.
 
Nadhani wote ni wamiliki ila mmiliki halali ni mama maana ndo anaejua ukweli kuhusu mtoto na baba wa mtoto
Kivipi mkuu, ushawahi ona mtoto anaitwa ubin wa mama??
 
KWA MTAZAMO WANGU HAKUNA MTU ANAWEZA KUMMILIKI MTOTO ILE SIO BIDHAA AU MALI, ILA WAZAZI WANAKUWA KAMA WAMEPEWA JUKUMU LA KUMLINDA NA KUMUONGOZA HADI ATAKAPOJITAMBUA NA KUANZA KUJITEGEMEA
Hapana mkuu fikiria tena uje
 
yuzazifu, Wote sio wamiliki bali ni wazazi tu.

Katika hatua ya uzazi, hakuna aliye na haki zaidi ya mwenzake kwa sababu wote wanategemeana katika kukamilisha hatua za utengenezwaji wa mtoto (uzazi). Maana yake wote wanategemeana, baba au mama peke yake hawezi kuzaa mtoto.

Hivyo hata katika malezi, wote wanapaswa kuwajibika kwa mtoto kwa sababu ni matokeo ya wote wawili, na wote hawana budi kuhusika katika malezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binti akipata mimba wanamuuliza hio mimba ni ya nani!!
Mtoto ni wa mwanaume siku zote
Kwa nini asiwe mama anaeshare vingi kuanzia yai, anavuta pumzi moja na mtoto mda wote awapo tumboni, anamlisha chakula awapo tumboni na hata baada yakumzaa then hata malezi sehem kubwa ni mama??
 
Doppelganger,
Ahsante bt mkuu hata wewe hata wewe ukiulizwa kwenu wapi utasema ubabani na si umamani hapo huoni baba umempa haki ya umiliki?
 
ahsante bt mkuu hata wewe hata wewe ukiulizwa kwenu wapi utasema ubabani na si umamani hapo huoni baba umempa haki ya umiliki?
Kuna makabila ambayo mama ndiye mwenye familia, ambapo watoto ni wa ujombani.

Huo ni utaratibu tuliojiwekea tu.

Kumbuka, mtoto akishaziwa wazazi mna jukumu la kulea tu. Mtoto "anamilikiwa" na Jamhuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna makabila ambayo mama ndiye mwenye familia, ambapo watoto ni wa ujombani.

Huo ni utaratibu tuliojiwekea tu.

Kumbuka, mtoto akishaziwa wazazi mna jukumu la kulea tu. Mtoto "anamilikiwa" na Jamhuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
rejea hata maandiko yanampa umiliki baba maana yanaeleza uzao kwa kufuata mlolongo wa majina ya ubabani
 
Back
Top Bottom