Kati ya baba na mama ni yupi mmiliki halali wa mtoto?

Kati ya baba na mama ni yupi mmiliki halali wa mtoto?

Nadhani wote ni wamiliki ila mmiliki halali ni mama maana ndo anaejua ukweli kuhusu mtoto na baba wa mtoto
Mmiliki wa mtoto ni baba wa mtoto na mama wa mtoto.

Hayo mengine stori.
 

Kama huyo mtoto ni wa baba halali, otherwize mmiliki wa mtoto ni mama.

Ndio maana wapwa (ma -uncle au mtoto/watoto wa dada) huwa wanapendwa sana wajomba zao, maana wanaamini huyu kweli ni damu ya dada yangu, lakini mtoto wa kaka! mmmh! 50/50.(jokes....)
 
Mama humiliki mtoto kwa miezi tisa tuuh badaa ya hapo Ni wangu!!!

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 
Hakuna kama Mama! Mama anagharamia zaidi watoto in term of muda, upendo, kujali,hela e.t.c kwa hiyo anapaswa kuwa mmiliki halali wa watoto
 
Hivi nikinunua mbuzi nikamfuga, mbuzi huyo akizaa mtoto, kiumiliki huyo mtoto ni wa mbuzi au ni wangu??

Ninachojua mtoto ji wa mama ila wote ji mali ya baba maana ndo aliyewaleta. Hapo ndo logic ilipo. Tipic over! [emoji41][emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtazamo wangu

Mtoto huwa anamilikishwa kwa baba ili kukamilisha umiliki wa mtoto,kwa sababu mtoto yeyote ni lazma amilikiwe na wazizi wawili,na hakuna doubt ya nani mama wa mtoto maana yeye ndie aliyebeba mimba na kumzaa lakini baba anaweza asijulikane maana hakuna athari yeyote.

Kwa mfano
Ikitokea mwanmke anamimba na haijulikani ni nani aliyempa,ni lazima ataulizwa ni mimba ya nani ili kukamilisha umiliki wa mtoto maana ni lazima kuwe kuna baba wa mtoto.
Kinyume chake hakuna maana huwezi kugeuza swali kwa mwanaume kwani hakuna mwanaume atakayemiliki mtoto ambaye hakuwa mimba na kuzaliwa.

Hivyo mtoto anapozaliwa huwa tayari ni milki ya mama ila hunasibishwa kwa baba ili kukamilisha umiliki.Hayo mengine ya nani anaishi na mtoto ni malezi tu ila milki ni ya wote.
 
Natumai mmeamka salama wanajamvi.

Wakuu hili jambo la nani ni mmiliki halali wa mtoto kati ya baba na mama limekua likinitatiza sana hata nikaona vema kushare nanyi ili tulijadili kwa marefu na mapana...

Kwa mtizamo ulozoeleka tunajua baba ndo mmiliki wa mtoto but utata wangu huja kwa kujiuliza ikiwa fertilization hufanyika kwa kukutana yai la mwanamke na mbegu ya kiume, why mwanaume ndo awe mmiliki wa mtoto na si mwanamke ambae hu-play part kubwa katika process ya upatikanaji wa mtoto?

Karibuni tujadili kwa facts.
Wote ni walezi tu, mmiliki ni Mwenyezi Mungu

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
MUNGU

Ndio maana huwa tunasema Bwana ametoa na Bwana ametwaa!!! 😛 😛
 
Umiliki wa mtoto unategemea na tamaduni na malezi.

Zipo jamii kama watu wa kusini ambao mtoto ni mali ya Mama, Na zipo jamii nyingine ambazo mtoto ni mali ya Baba.

Hili la Baba kuwa mmiliki (yaani kumpatia mtoto ubini ) limekaa kimtego sana japo wengi wetu huwa tunaamini (nikiwemo na mimi) kuwa hii ndio njia sahihi.

Lakini tujiulize je umewahi kusikia Mwanamke akisingiziwa ujauzito? Na je ni nani mwenye mchango mkubwa kwenye process nzima ya kutungwa mimba hadi kuzaliwa mtoto?

Tukiyajibu hayo tutagundua kuwa haiwezekani Mwanamke kusingiziwa ujauzito.

Pia Mwanaume ni Donor wa mbegu kwenye yai la mwanamke ili kukamilisha mtoto kuumbwa ndani ya tumbo la mwanamke.

Pia katika malezi, Baba hutoa ulinzi na mahitaji kwa mtoto, lakini mama anaweza kutoa hayo yote na zaidi ni mwalimu wa kwanza kwa mtoto wake, hili hupelekea mtoto kuwa Loyal kwa mama yake(mara nyingi).

Hivyo ninaamini kuwa wanaosema mtoto ni wa mama wako sahihi zaidi ya tunaosema mtoto ni wa Baba. ( Hapa tumweke MUNGU pembeni) kwani hakuna mtoto anaechkua ubini wa MUNGU) Japo tunasema wote ni wa MUNGU.

In vino Veritas(In Wine there is truth)......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni mambo za matrilineal na patrilineal societies.
Baadhi ya jamii husema mtoto ni wa mama (matrilineal) na Baadhi husema mtoto ni wa baba (patrilineal).

Ukija ki imaani mtoto ni wa wote baba na mama kwa sababu ametokana na maji ya kuchupa (manii kutoka kwa baba) na ikaenda kurutubisha yai (uzazi wa mama) kisha baada ya hatua zoteee ndio hupatikana mtoto.
So, inategemea wewe upo upande upi kati ya pande hizo 3.
1. Matrilineal
2. Patrilineal
3. Religion.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili swali ni sawa na kuuliza kati ya kuku na yai nani mkubwa au kilianza kipi
 
Hivi wazazi kwanini wanaamua kukuleta duniani? Ulishawahi kujiuliza swali kama ilo?
 
Anaeweza kumiliki ni yule sio mimii [emoji23][emoji23][emoji23]
IMG_20200508_095344.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom