Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

Hivi na yule mkurugenzi wa jiji la dar naye ni district executive director (DED)? je dar ni district?
 
Katibu tawala yeye ni kutawala na mkurugenzi yeye ni shughuli za maendeleo . Hilo jina tawala linatosha kwamba Das anamtawala mkurugenzi .
 
Kimaslai na marupurupu na kimafungu nani yupo juu ya mwingine kumbuka masurufu na mafungu ndio nguvu ya Kiti na Cheo.Hivyo mi naona DED ndio kila kitu hao wengine ni vyeo vya kisiasa zaidi.
Mishahara na marupurupu wapo ngazi moja.
 
Hivi na yule mkurugenzi wa jiji la dar naye ni district executive director (DED)? je dar ni district?
Mkurugenzi wa Miji yaani City Director (CD). Huyu anamshahara mkubwa kuliko DAS. Huyu anateuliwa na Rais wa Jamhuri. MaDED na Town Directors na Municipal Directors wanateuliwa na Waziri wa TAMISEMI (Pia wanaweza kuteuliwa na Rais ila atafanya hivyo kwa capacity ya Waziri mwenye dhamana ya TAMISEMI kwa kuwa Wizara ipo Ofisi ya Rais).
 
Kama ni hivyo nafasi za madiwani nazo zifutwe
 
Katibu tawala yeye ni kutawala na mkurugenzi yeye ni shughuli za maendeleo . Hilo jina tawala linatosha kwamba Das anamtawala mkurugenzi .
Ni kweli kwamba Katibu Tawala ni mtu anaesimamia utawala yaani Rasilimali watu au tuite Afisa Rasilimali Watu. Lakini si kweli kwamba anamtawala Mkurugenzi. Hana madaraka hayo. DAS yeye ni msimamizi wa ofisi ya DC. Chini yake kuna Afisa Tawala na Maafisa Taarafa. Pia wapo RITA (vizazi na vifo), anafungisha ndoa za Serikali na kazi za kiulinzi na usalama.

DED ni utaalam tupu. Chini ya DED kuna Wakuu wa Idara na chini ya wakuu wa Idara kuna wataalam wa kada zote ukiondoa wale wa vyombo vya ulinzi na usalama. Hawa ndiyo wanaotekeleza miradi, huduma za Jamii na utendaji wa Serikali kwa ujumla. DED ndiyo accounting Officer wa fedha zote zinazoenda kwenye Halmashauri. Ndiye mwajiri wa watumishi wote walioko kwenye Halmashauri.
 
Kama ni hivyo nafasi za madiwani nazo zifutwe
Binafsi huwa sipendezwi kabisa na nafasi ya madiwani hii inatokana na utendaji usioridhisha wa mabaraza ya madiwani. Lakini hawezi kufuta madiwani kwakuwa itakuwa ni kwenda kinyume cha dhana ya ugwatuaji madaraka (devolution and decentralization) au wengine wanaita bottom up approach.

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa dhana ya ushirikishaji Jamii inamanufaa kuliko dhana ya kutoa maagizo kutoka juu.
 
Mbona pesa yote ya wilaya inapitia kwa katibu tawala? Hata fungu la mkuu wa wilaya analo yeye sana sana labda mkuu wa wilaya agome kusaini matumizi lakini hana mamlaka na pesa.Mimi sio mwana siasa ila nabahatisha tu hivyo anaejua zaidi atujuze .
 
 
mimi madhani kama nchi tungepiga sana hatua kama katika halmashauri kuwe na mojawapo kati ya aidha wakurugenzi au DAS / RAS cheo kimoja wapo kifutwe

halafu hiki cheo kinacho itwa Sijui mkuu wa wilaya sijui mkoa. vifutiliwe mbali havina maana zaid ya ulaji tu na siasa chafu na za kishamba usimamizi wa ulinzi na usalama libaki kuwa jukumu la MA RPC na OCD
 
Mbona pesa yote ya wilaya inapitia kwa katibu tawala? Hata fungu la mkuu wa wilaya analo yeye sana sana labda mkuu wa wilaya agome kusaini matumizi lakini hana mamlaka na pesa.Mimi sio mwana siasa ila nabahatisha tu hivyo anaejua zaidi atujuze .
Si kweli kwamba pesa yote ya Wilaya inaenda au inasimamiwa na DAS. Pesa inayoenda kwa Katibu Tawala wa Wilaya ni ile tu inayohusu ofisi hiyo tu. Zingine zote zinaenda kwa DED.

Pesa inakuwa chini ya accounting officer kiswahili Afisa Masuhuli. Mfano Wizarani ni Katibu Mkuu siyo kwa Waziri. Mkoani ni Katibu Tawala wa Mkoa siyo kwa Mkuu wa Mkoa, Wilayani ni kwa DAS siyo kwa DC na Halmashauri kwa Mkurugenzi siyo kwa Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri. Hali kadhalika kwenye kata na mitaa ambako kuna Maafisa Watendaji, madiwani na wenyeviti wa Mitaa.
 
Nyongeza Mkuu..kunaweza kuwepo DAS mmoja kwenye wilaya yenye maDED zaidi ya watatu..hivyo tafsiri ni kuwa DAS yuko juu kuliko DED.
 
Kama kweli tumekusudia kubana matumizi hapo kuna kazi zinaingiliana, ikumbukwe ndani ya ofisi ya DC yupo pia mtu anaitwa DAO = District Administrative Officer.
 
DED = District Executive Director, DAS = District Administrative Secretary & DC = District Commissioner. Wote hao ni kuteuliwa na kutumbuliwa wakati wowote. Nani mkubwa hapo
Kuna kipindikulitokea mgogoro Wizara ya mambo ya ndani kati ya Waziri au naibu waziri nafikiri (sikumbuki vizuri details)na presidentialappointees wa jeshini huku polisi.

Ikawa Wizarani wanakoromea jeshini,jeshini nao wanakoromawanasemana wao ni presidential appointee.

Kesi ile ili expose ubovu wa mfumo wetu.

Rais ana appoint Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Polisi, na makamishna wa polisi.

Siku likitokea tifu hapo, kila mmoja anaweza kumvimbia mwenzake akamwambia "I serve at the pleasure of the president".

Ukitaka kuniadabisha wewe huwezi, mwambie rais aliyeniteua.

Ni mapungufu ya mfumo ambao rais anateua kila cheo, kuanzia Waziri Mkuu mpaka mfagia choo wa chekechea aliyepewa jina la kum glorify
 
U tried
 
Kama kweli tumekusudia kubana matumizi hapo kuna kazi zinaingiliana, ikumbukwe ndani ya ofisi ya DC yupo pia mtu anaitwa DAO = District Administrative Officer.
DC, DED, DAS, DAO X namba ya wilaya za nchi.

Hivi vyeo vingine vya kupandiana watu wanatengeneza largesse tu.
 
Mmmh!
 
Kwa sasa yule anayejipendekeza sana kwa mkulu ndio boss wa mwingine bila kujali protocal. Mfano Bashite na PM.
DC ni boss wao wote nadhani. Anauwezo wa kuwaita na kuwachimba mikwara wote maana yeye ni muwakilishi wa Rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…