Kati ya DED na DAS nani bosi wa mwingine?

DED ni mwajiri kwa ngazi ya halmashauri pia mkumbuke na DAS hawezi kuajiri. Hapa mkubwa ni DED.
 
 
Kwenye awamu hii wote wameteuliwa na rais.
Zamani TAMISEMI ilipokuwa ofisi ya waziri mkuu ndio ilikuwa DED anateuliwa na PM.

Siku hizi tamisemi IPO ofisi ya rais.

Zipo wilaya zenye halmashauri zaidi ya moja, DED -2, but DAS mmoja.

Wana majukumu tofauti, at one point DED anareport kwa DAS.
DAS anahudhuria vikao vya CMT kama mshauri, pia anahudhuria vikao vya baraza LA madiwani but hawajibiki kwao.

DAS line yake ya utendaji wa kila Siku iko sana kwa maafisa tarafa na wenyeviti wa vijiji/ vitongoji na mitaa , vyombo vyote vya ulinzi na usalama wilayani. He can surmon all government agencies in the district ( TRA,tanesco na taasisi nyingine zote kutoka wizara mbalimbali zilizo wilayani kwake) wakati DED anadeal zaidi na watumishi wa idara mbalimbali wakiwemo watendaji kata/ vijiji + madiwani. Na mamlaka ya DED yanaishia kwenye taasisi zilizo chini ya tamisemi tu.
Kisiasa imedeatelty juu ya DED yupo mwenyekiti wa halmashauri/ meya wakati kwa DAS yupo DC.

DAS yupo kidola zaidi wakati DED yuko kiutumishi/ umma zaidi.

DED ana nafasi kubwa ya kufa akiwa tajiri wakati DAS ana nafasi kubwa sana ya kufa maskini.
 
Hujamalizia mpunga DED anampunga mrefu kwamaana ya mapato na matumizi katika halmashauri lakini DAS hakusanyi na anamtegemea DED amsaidie akikwama
 
Ukiona hawaelewani juwa DC anaingilia kazi za Halmashauri, badala ya kuwasimamia
 
Cheo cha DC ni cha kisiasa zaidi kwa kweli Kimondoa,kwa hiyo ni kweli kinaweza kufutwa!Hata hivyo let us be realistic,katika mfumo wa vyama vingi, sidhani kama chama tawala(hapa simaanishi CCM,ni chama cho chote kile kilichoko madarakani), kinaweza kukubali kufuta cheo hicho, kwa kuwa kinasaidia chama husika kisiasa.
 
DED ni mwajiri kwa ngazi ya halmashauri pia mkumbuke na DAS hawezi kuajiri. Hapa mkubwa ni DED.
Mkuu DED anaajiri sawa, lakini yuko Halimashauri
(TAMISEMI ) na DAS yuko serikali kuu(UTUMISHI) kwa hiyo hawahusiani hawa.Nadhani swala la kuajiri halina tija sana,mfumo ndio unaompa mamlaka DED kuajiri,ila haina maana kwamba yuko juu ya DAS kimadaraka.
 
DC anateuliwa na Rais wa Jamhuri lakini DED anateuliwa na Waziri wa TAMISEMI. DC anakazi zake na DED anakazi zake, hawaingiliani.
Uko sahihi expert member. However, kiuhalisia DC anaweza kukwamishwa na DED kutekeleza majukumu yake. Nina mfano halisi, it's too bad
 
Or else halmashauri zijitosheleze kimapato sio kutegemea kwingine
 
Watumishi wote wa wilaya wapo chini ya DAS kwa hiyo DED yupo chin ya DAS
 
Or else halmashauri zijitosheleze kimapato sio kutegemea kwingine
Unajua mkuu,local governments ziliundwa upya mwaka 1982 baada ya kufutwa mwaka 1972.Nia ya kuzirudisha ilikuwa ni kupeleka huduma za serikali karibu zaidi na wananchi.Kwa kufanya hivyo ilitegemewa kwamba ingechangia na kuhamasisha zaidi maendeleo ya wananchi kwa haraka. This was never realized.Badala yake Halimashauri zikaendekeza ufujaji wa fedha za wananchi na kudumaza maendeleo yao.

Sasa tukisema Halimashauri zijitosheleze kimapato tuna maana gani,kwa kuwa Halimashauri hazina vyanzo vya mapato per se,zinategemea kuwachangisha wananchi.Tatizo kubwa la Halimashauri zetu ni kushindwa kutumia mapato yao kama inavyotegemewa.Mkuu sina sababu yeyote ya kuamini kwamba hata kama serikali ikiruhusu Halimashauri zibaki na mapato yao,hali itakuwa nzuri zaidi,kwa kuwa hata serikali kuamua mapato yapelekwe serikali kuu,halafu Halimashauri zigawiwe, ilikuwa kwa sababu ya upigaji.Hapana,
Halimashauri zimeshindwa kutimiza malengo yaliyo kusudiwa,tuzifute tu,kama tulivyofanya 1972.

NB:Ukitaka kujua historia ya serikali za mitaa Tanzania,google,"The history of local governments in Tanzania."
 
Ndio maana madai ya watumishi wa umma,mishahara ambayo haikulipwa Das ndo anaidhinisha ikishatoka kwa DED mfano,mtumishi akafariki mshahara ukatoka it means huo mshahara haukulipwa,DED ataurudisha kwa Das ambaye ataidhinisha na DAS atarudisha kwa RAS ambaye ataurudisha hazina au kama kuna watumishi wa halmashauri wanadai DED ataandaa madai yataidhinishwa na DAS ndo yaende kwa RAS na RAS ataidhinisha na kupeleka kwa katibu mkuu ndo yapelekwe hazina kwa hivyo kwa mlolongo huo DAS ni boss wa DED
 
Interesting! Tuendelee kujadili inawezekana kuna wenye hoja za kutuelimisha zaidi, ila kiukweli kuna shida. Namkumbuka DC wangu mpendwa ambaye DED wake alimbeza kwangu nikiwa na wageni wa Taifa jingine. I felt so bad.
 
Interesting! Tuendelee kujadili inawezekana kuna wenye hoja za kutuelimisha zaidi, ila kiukweli kuna shida. Namkumbuka DC wangu mpendwa ambaye DED wake alimbeza kwangu nikiwa na wageni wa Taifa jingine. I felt so bad.
Pole sana mkuu.Haya ndiyo kati ya mambo yanayotufanya tuamini kwamba Halimashauri zifutwe.Ni kweli kwamba mafungu DED waliyonayo yanawafanya wajione miungu watu na hivyo kudharau watendaji wengine wa Wilaya na kuwaona si kitu kabisa.Tabia hizi hazikubaliki kabisa mkuu.
 

Nimeshawishika na namna nzuri uliyoitumia kueleza hoja yako. Hongera sana mkuu. Kwa hoja ya nani anateuliwa na nani (kama ulivyoeleza ni kweli) basi huenda kweli DED yuko juu kiitifaki kuliko DAS, swali langu hapa ni je, ni lazima mtendaji aliyeteuliwa na Mamlaka ya juu awe juu kiitifaki kuliko yule aliyeteuliwa na mamlaka ya chini ?
 
Kwa dhana ya "Wilaya" dhidi ya "halmashauri," mimi nadhani DAS yuko juu kiitifaki kuliko DED kwa mchanganuo ufuatao:-

DAS ni mtumishi wa wilaya. (Wilaya moja, DAS mmoja).

DED ni mtumishi wa halmashauri (kwenye Wilaya moja kunaweza kuwa na halmashauri zaidi ya moja).

Kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba "Wilaya moja, DAS mmoja".

Na pia tunaweza kusema, "Wilaya moja halmashauri moja au mbili na hivyo DED mmoja au wawili"

Katika mazingira haya simuoni DED akiwa juu ya DAS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…