Kati ya Gari ya Diesel na Petrol, ni ipi inatumia Mafuta sana?

Kati ya Gari ya Diesel na Petrol, ni ipi inatumia Mafuta sana?

Mkuu mafuta yakishachomwa hayarudi tena labda unieleweshe vizur hapo lakini usichanganye na hydrolicky
Gari zinakuwga na return pipe ambapo mafuta yale yaliyosukumwa na pump alaf hayakwenda kuchomwa yanarud kwenye tanka tena
 
Mkuu kwahiyo brevis n mark x ipi ina mbio
Mark X ina speed zaidi lakini Brevis ina comfortability hata ukiwa upo speed sana!..
Kuna muda ukiwa speed na Mark X unaanza iona kama inainuka hivi haitulii, wakati kwenye Brevis inakuwa nyepesi lakini inatulia!..
 
1082179
 
Labda ni Mimi sijaelewa, ila trekta, kwenye tank lake la mafuta kuna pipe mbili: moja juu kabisa ya tank ambayo ni return pipe, na moja ipo chini kabisa ambayo inapeleka mafuta kwenye injini.

Na niliaambiwa yakichomwa yanarudi
Alicho kwambia ni kweli. Hii kwasababu pampu husukuma mafuta mengi kuelekea kwenye injini na yanayotumika ni kidogo sana.... yale yanayobaki hurudi (ndio return)
 
Brevis 1JZ huyo anakamua wese kama kichaa

Yeye amezungumzia magari yenye mfumo zaidi wa umeme mfano harrier hybrid ina engine ya cc 3300 petrol ila inaenda hadi km 18 while harrier ya kawaida cc 2400 petrol inaenda km 12 sasa hiyo ya brevis ni engine ya kawaida c ya umeme mwingi
 
Labda ni Mimi sijaelewa, ila trekta, kwenye tank lake la mafuta kuna pipe mbili: moja juu kabisa ya tank ambayo ni return pipe, na moja ipo chini kabisa ambayo inapeleka mafuta kwenye injini.

Na niliaambiwa yakichomwa yanarudi
Yanayorudi si yale yaliyochomwa.... Mafuta yanayonyonywa toka kwenye tenki ni mengi kuliko yanayohitajka kwa wakati husika. Kabyureta (Petroli) inector pump (Diesel) inachukua kiasi kinachohitajika nankukipeleka kuchomwa, kile kilichozidi ndo hicho kinarudi kwenye tenk kurudia mzunguko. Lakini yakishaingiamkwenye kuchomwa hayarudi
 
Yeye amezungumzia magari yenye mfumo zaidi wa umeme mfano harrier hybrid ina engine ya cc 3300 petrol ila inaenda hadi km 18 while harrier ya kawaida cc 2400 petrol inaenda km 12 sasa hiyo ya brevis ni engine ya kawaida c ya umeme mwingi
Jamani msipotoshe. Hybrid zina electric motor. Kwenye speed below 60kph inatumia electric motor. Ikiwa above 60kph inatumia petrol kwa kiwango kile kile cha kawaida. Sema ukichukua combine mileage electric+petrol ndio unaweza kupata hizo km nyingi per litre.
Ila hata teknolojia iweje cc4500 petrol haiwezi kukupa 18km/litre.

Chukua hio Hybrid ya cc4500 linganisha na Hybrid ya cc2000. Usilinganishe na conventional petrol engine.
 
Mm sikutaja kabsa hapo cc 4500 maana sina ushahid na hilo nimetolea mfano gari hizo ninazozifahamu hiyo ya 4500 atakuja kueleza anayejua
 
Ujinga wa diesel inapenda sana kutiwa vidole na mafundi. Trip za kwenda garage kwa gari ya diesel ni za mara kwa mara!
Ambacho hujui ni kwamba...mfumo wa diesel ndo imara na wakudumu zaidi ya mfumo wa petrol.

Diesel ni kwaajili ya heavy duty machines. Na petrol ni kwaajili ya mashine nyepesi.

Mfumo wa diesel sio sumbufu kama petrol na unavumilia matatizo zaidi,

Mfumo wa diesel ni bei kubwa kuliko petrol (gari ya petrol ina bei ndogo lakini gari hiyo hiyo ikiwekwa injine ya diesel inapanda bei!)

Uliza bei ya jenereta la petrol na ufananishe na bei ya jenereta la diesel lenye uwezo huohuo, 'utahisi unaibiwa!
 
Back
Top Bottom