Kati ya hawa mmojawapo anaweza kuwa Rais 2025

Aisee nimefikili na wewe umejiweka kwenye orodha hiyo, kazi yako kuwa orodhesha wengine kweli we mjinga aisee!.
 
Mkuu, mimi umeniweza kabisa; nimesoma nikitarajia utaliweka na lile kanyabwoya la chadema, nikaambulia parupu!
 
Acheni Agrarian mentality , fikirieni kumpata kiongozi tofauti na JIWE atakayekuwa na mawazo ya kuendeleza nchi kwa mawazo mapya yanayoendana na Dunia ya leo!! Hii leo kiongozi gani mwenye maono anafikiria kuongoza nchi kwa kujenga viwanda bila kuainisha information/ technological advancement inayoendelea duniani? Bila kumpata kiongozi mwenye maono kila siku tutakuwa tunafikiria kuchimba mashimo ya vyoo shuleni wakati wakina Mask na Bezos wanafikiria kuhamia MARS!!
 
Toa wakristo hao, ajaye ni muislamu
 
ungekuwa huna chama ungetaja ndugu zako bas..😎
 
Jafo gani tena jamani,??? Yaani akili za jafo ndo awe rais wa nchi??? Hebu mtupumzishe bwana, mtu ambae hawezi kusimamia anachokiamini hafai kuongoza hata familia
Jaffo au Ummy Mwalimu..
 
Kama ni kwa siri mbona tumejua ?
Ebu waambie wasubiri kwanza tufikie Tz ya viwanda
Au nasema uongo ndg zangu
 
Hali inaweza kuwa tofauti...
Lowassa anaweza kuwa rais na makamu wake mwinyi.
 
Hao wawili wa kwanza wote wape 50% kwa 50%. Hussein Mwinyi itategemea kama atakuwa tayari amepata mrithi wa kuaminika SMZ. Kama atakuwa bado basi ataendelea kwa miaka mingine mitano huku akiwa nafanya grooming ya mtu sahihi. Ikitokea hivyo hapo sasa Majaliwa itakuwa ni 100%. Zaidi ni kuwa Majaliwa ni mkali kuliko Hussein Mwinyi, na possibly kuliko hata JPM. Mwangalie vizuri. Kwa muda huu, nchi zetu zinahitaji marais wakali tu na si vinginevyo
 
2025 ni kati ya

1- Mr Madelu( Mwigulu)
2- Mkumbo
3-Doroth

Hawa watatu wana nafasi kubwa!!
Kumbuka Magufuli hataki watu wenye makundi!
3. Dorothy????
Huyu mwenda wazimu awe rais?!!!!!
Wizara tu inamzidi kimo
 
hapo sijaona hata mmoja anafaa kuwa rais. wote hao wanafanya kazi kwa bidii sababu rais aliepo sasa anawalazimisha kufanya hivyo haipo kwenye damu. JPM alikuwa mchapa kazi tangu waziri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…