Mfano taasisi ninayofanya mimi graduate anaanza na 2,030,000 na kuna posho ya nyumba na usafiri 400,000 kwa mwezi, na hapo haipo kwenye list. Kwa hiyo huenda zilizotajwa hapo wanaanza na juu ya hapo. Lakini hearsays ni nyingi sana humu huenda hata hizo zilizotajwa wana mishahara ya kawaida.
Pia watu wanasema kisa TRA wanakusanya kodi ndio wana mishahara mikubwa, hii pia sidhani kama kuna uhalisia. Wote tunajua watu wa TRA wana pesa chafu kwa sababu ya madili yao hasa enzi zile.
Hapo ulipo ndugu yangu ndio pana pesa nzuri, stori nyingine mwisho upambane ukute mshahara 1.5 M halafu ni mwendo wa mshahara hadi mshahara hakuna extra duty allowances wala safari. Tukae humo.